Nakuunga mkono kwa hoja yako, lakini ndugu yangu kuna mambo mengi sana yasiyofurahisha ambayo hufanywa na wachumba wa pande zote mbili kwa siri kuchunga mchumba asiyajue, sasa hili limejulikana lakini kwa njia ya hila.
Ndiyo nikasema aweza akafumbia macho na pasiwe na madhara yoyote kama mchumba huyo ana upendo kwake usiotiliwa mashaka .
Na kwa teknolojia za kisasa kuhusu sayansi ya picha ipo advanced sana, kiasi cha mtu kushindwa kutofautisha ya kweli na ya uongo.
Lakini huyo mchumba kama ni shakubimbi kweli na ameridhika naye, kipimo cha kwanza kimekwisha kupita, ampime kwa mambo mengine sasa kisha achukue hatua nadhubuti.
Kwenye mabaraza ya usuluhishi wa ndoa, huwa hatutoi ushauri wa kuvunja bali wa kujenga.