Nimepigwa na mume

Nimepigwa na mume

nimezaa naye watoto watatu,mume wangu ni mtu wa manyara,wazazi wako hai,kosa alilonipiga nilimkosoa kwa alichokifanya ambacho hakikunifurahisha mimi
Sikia Dada sidhani kama hii ndio ya kwanza na hata kama ndio mara ya kwanza usikimbilie kwenye mitandao,ongea nae kama bado waeleze wazazi wake uwashirirkishe na wakwako,huyo ni mumewako wewe amekutoa kwa wazazi wako na ndoa yako ni ya halali, lia na mwenyezi mungu akupe subra na uvumilivu....
 
nimezaa naye watoto watatu,mume wangu ni mtu wa manyara,wazazi wako hai,kosa alilonipiga nilimkosoa kwa alichokifanya ambacho hakikunifurahisha mimi
Pole sana, mshitaki kwa wazazi wake, lakini usisahahu kuwaambia wazazi wako pia kuwa umepigwa na kisa cha kupigwa ni nini! Ikishindikana jaribu kuwashirikisha viongozi wenu wa kidini, Usiende Polisi wala Nyumbakumi.
 
Pole sana , cha kwanza nenda hospital kaangalie kama hujaumia kwa ndani na huna internal bleeding
 
Pole sana, mshitaki kwa wazazi wake, lakini usisahahu kuwaambia wazazi wako pia kuwa umepigwa na kisa cha kupigwa ni nini! Ikishindikana jaribu kuwashirikisha viongozi wenu wa kidini, Usiende Polisi wala Nyumbakumi.
nimemshitaki kwa wazazi wake wala hawana lolote lakunisaidia ndo maana naulizia sheria
 
achana na sheria we mvizie usiku kalala mwamshe ile akiitikia tu mdunde na marungu maeneo atakayo umia kirahisi .. ila mlango uwe wazi ukimbie asikukamate .. ila ujiandae kuachika

Hii mbinu hilo rungu likimkosakosa huyo jamaa, huyu dada ajiandae kuwa kibogoyo.
 
Mpeleke polisi, Kisha mahakamani na akafungwe Segelea ili hao watoto watatu ulee mwenyewe kwa muda atakaokuwa huko, Baada ya hapo, ninauhakika utakuwa umejifunza mengi, hutahitaji ushauri tena...
 
nimemshitaki kwa wazazi wake wala hawana lolote lakunisaidia ndo maana naulizia sheria
Kwani unataka kuachana naye? Kwani unaishi naye kwa sheria au mapenzi? Ukiingiza sheria manake mapenzi yameisha!
 
sitaki kuachananaye,naishi naye kisheria na kimapenzi ndo maana ndoa halali inatambulika kisheria na sitaki kumwacha kwa mapenzi niliyonayo kwake
 
Kwani unataka kuachana naye? Kwani unaishi naye kwa sheria au mapenzi? Ukiingiza sheria manake mapenzi yameisha!
kwahiyo unamaanisha kwa sababu naishi naye kimapenzi ndo nikubali unyanyasaji anaonifanyia?
 
Pole kwa kunyanyaswa, Sikuwa na maana mbaya isipokuwa kama wewe unampenda na yeye anakupenda basi kaeni chini mzungumze! Inawezekana alikosea au anahisi kama wewe unamfanyia dharau za makusudi, na mimi ninavyojua mtu anayekupenda hawezi akakupiga!!! Binafsi naona kama kumpiga mwanamke ni udhaifu mkubwa kwa mwanaume. Ongeeni kama mke na mume muyamalize.
 
mtafutie panya road ili wamshikishe adabu kidogo ila jiandae kuuguza !!
 
achana na sheria we mvizie usiku kalala mwamshe ile akiitikia tu mdunde na marungu maeneo atakayo umia kirahisi .. ila mlango uwe wazi ukimbie asikukamate .. ila ujiandae kuachika

Duuuu! Miss Chagga unatisha
 
Back
Top Bottom