Nimepita Instagram account ya Fiston Mayele kuna kitu sikielewi naomba nielimishwe

Nimepita Instagram account ya Fiston Mayele kuna kitu sikielewi naomba nielimishwe

PhD holder unashangaa kuona mcongo anazungumza kiswahili? Hujui kiswahili ni moja kati ya lugha rasmi za taifa nchini Congo?
Anyways Mayele kakulia Lubumbashi na Lubumbashi wanazungumza kiswahili.
Hivi umeelewa hata nilichoandika kweli au umekurupuka tu?

Hao kina Christian Bela na ngwasuma kwani wanaimba Kwa lugha gani?

Swali ni Kwa nini Wabongo ndio wanaocomment tu? najuwa miandiko ya Wacongo na kiswahili chao nakijuwa, kiswahili cha mbagala na Tandale kinajurikana vizuri tu.

Kwa kiswahili ya Congo wewe unatomboka na kuyamba tu.
 
Swali ni Kwa nini Wabongo ndio wanaocomment tu? najuwa miandiko ya Wacongo na kiswahili chao nakijuwa, kiswahili cha mbagala na Tandale kinajurikana vizuri tu.

Swali la kitoto kweli kwani wewe Mayele alikuwa maarufu bongo kwa sababu ya Yanga?

Wewe nenda katafute vivunja chungu tu mkuu kwenye kufanya reasoning bado u mtoto
 
Kwanza niweke wazi Mimi hiyo Instagram huwa natumia zaidi Kwa ajili ya kusoma magazeti Kwa Millard Ayo.

Ila baada ya Mayele kutrend na "majini" yake nimejaribu kupitiapitia account yake na nimeshangazwa na kitu kimoja.

Fiston Mayele NI Mcongoman na Kwa sasa ni mchezaji wa Pyramid ya Masri, lakini kilichonistaajabisha NI post au status zote za Mayele ni za Kiswahili na kifaransa lakini hakuna comments za Wacongo wala za Waarabu, NI Watanzania ndio zimejaa comment zao na shobo kama zote, status ya kifaransa comments za Kiswahili, shame.

Sasa kuna kitu hapa sielewi je ni Sisi Watanzania ndio hatujitambui na hatuna kazi za kufanya au Mayele ana account tofauti tofauti ambayo hii ninayoiona ni Maalum Kwa Tanzania Tu?

Lakini kama jibu ni hapana hiyo ndio official account ya Mayele basi nadiriki kusema Watanzania tujitafakari Sana, tuna zaidi ya tatizo tena hafadhali hata ya Mayele aliyetumia page yake kuandika anachojisikia kuandika.

Jobless imeharibu mifumo ya akili za Watanzania refer to GENTAMYCINE
Mayele ameamua kuwa mchezaji wa mitandaoni Kama edo alivyosema , Mpira Utakuwa umemshinda anatafuta sababu.
 
Back
Top Bottom