Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 17,048
- 22,790
Jana nimepoteza kaka yangu niliyekuwa namfuatia; yeye alikuwa anaishi kijijini ambako ameishi tangu aliporudi vitani mwaka 1980. Alikuwa mtu mzima sana; kinachonisikitisha zaidi ni sababu ya kifo chake.
Alikwenda kunywa pombe za kienyeji na kendelea kunywa kwa siku mbili mfululizo bila kula; aliporudi nyumbani baada ya siku hizo akaenda kulala na hakuamka tena.
Ndugu yangu huyo alikuwa na matatizo sana ya kuhimili pombe kiasi kuwa ukoo wote ulimkatia tamaa; kwa bahati mbaya sana yeye ndiye aliyekuwa amebaki mkubwa peke yake kwenye ukoo huko kijijini, kwa hiyo hakukuwa na mwenye sauti juu yake. Nimeanza kufikiri kuwa huenda mimi ningekuwapo mara kwa mara pale kijijini huenda asingepotoka kufikia kiasi cha kupoteza maisha yake kwa njia ya aibu namna hiyo.
Ukiwa na ndugu mwenye tabia za marehemu kaka yangu, jitahidi uwe unatenga muda wa kumshauri mara kwa mara kuhusu pombe asitumbukie kwenye janga lililotufika sisi.
Kazi ya Mungu haina makosa
Mungu ampumzisha roho yake anakosatahili