Nimepoteza Kaka Yangu Niliyekuwa Namfuatia

Allah is great.
Pole sana kwa msiba.
Mipango ya mazishi inafanyikia wapi ?
 
Madhara ya vita sio lazima yatokee vitani. Vitani watu wanafanya mengi, wanafanyiwa mengi na wanaona Mengi. Inaweza kuchukua muda ... Kutafakari, kuapata maoni/maoni mapya nk.

Na kwa kubandika hapa, kunanini cha kujifunza, kwamba ukilewa utakufa usingizini?
Mimi nilikuwa naye kwenye sehemu kubwa ya maisha yake kabla sijalowea, na elewa kuwa hata mimi nilitumika vitani. Siwezi kuhusisha tabia iliyochukua uhai wake na vita ya aliyoshiriki na kumaliza mwaka 1980.

Mungu ampe mapumziko ya milele
 
Allah is great.
Pole sana kwa msiba.
Mipango ya mazishi inafanyikia wapi ?
Kazi ya Mungu haina makosa,

Mazishi ni huko huko kijijini na shughuli zimeshaanza, mwili wake utazikwa kwesho. Mimi sitahudhuruia kutokana na ufinyu wa muda, ila nitakwenda kuweka msalaba kwenye kaburi lake mwezi kesho.
 
Jana nimepoteza kaka yangu niliyekuwa namfuatia; yeye alikuwa anaishi kijijini ambako ameishi tangu aliporudi vitani mwaka 1980. Alikuwa mtu mzima sana; kinachonisikitisha zaidi ni sababu ya kifo chake.

Alikwenda kunywa pombe za kienyeji na kendelea kunywa kwa siku mbili mfululizo bila kula; aliporudi nyumbani baada ya siku hizo akaenda kulala na hakuamka tena.

Ndugu yangu huyo alikuwa na matatizo sana ya kuhimili pombe kiasi kuwa ukoo wote ulimkatia tamaa; kwa bahati mbaya sana yeye ndiye aliyekuwa amebaki mkubwa peke yake kwenye ukoo huko kijijini, kwa hiyo hakukuwa na mwenye sauti juu yake. Nimeanza kufikiri kuwa huenda mimi ningekuwapo mara kwa mara pale kijijini huenda asingepotoka kufikia kiasi cha kupoteza maisha yake kwa njia ya aibu namna hiyo.

Ukiwa na ndugu mwenye tabia za marehemu kaka yangu, jitahidi uwe unatenga muda wa kumshauri mara kwa mara kuhusu pombe asitumbukie kwenye janga lililotufika sisi.

Kazi ya Mungu haina makosa

Mungu ampumzisha roho yake anakosatahili
Pole sana ndugu!
 
Anapumzika kwa Amani kwani ameondoka baada ya kufanya kinachompa Raha katika maisha yake!
Usijutie na kujilaumu ya kuwa ungefanya hivi au vile, kama haukufanya akiwa hai, inasaidia nini kujilaumu sasa?
 
Madhara ya vita sio lazima yatokee vitani. Vitani watu wanafanya mengi, wanafanyiwa mengi na wanaona Mengi. Inaweza kuchukua muda ... Kutafakari, kuapata maoni/maoni mapya nk.

Na kwa kubandika hapa, kunanini cha kujifunza, kwamba ukilewa utakufa usingizini?
Somo kubwa hapa halijaeleweka kwa wengine. Ni kwamba ukiwa na ndugu mwenye tabia ya ndugu yangu huyo, mwimbie wimbo wa madhara ya pombe bila kuchoka; usimwache ajiamulie kila kitu kuhusu pombe freely hata kama ni mtu mzima.
 
Anapumzika kwa Amani kwani ameondoka baada ya kufanya kinachompa Raha katika maisha yake!
Usijutie na kujilaumu ya kuwa ungefanya hivi au vile, kama haukufanya akiwa hai, inasaidia nini kujilaumu sasa?
Ni kweli ameshapumzika

mengine ni machungu ya kuomboleza tu; binadamu hatupendi kuwapoteza ndugu zetu.
 
Kazi ya Mungu haina makosa,

Mazishi ni huko huko kijijini na shughuli zimeshaanza, mwili wake utazikwa kwesho. Mimi sitahudhuruia kutokana na ufinyu wa muda, ila nitakwenda kuweka msalaba kwenye kaburi lake mwezi kesho.
Hakuwa na ukaribu kabisa, unatarajia kwenda msibani mwezi baada ya msiba, halafu unaotaka kusema ungekuwa karibu ili umshauri jinsi anavyoishi maisha yake?!
 
Somo kubwa hapa halijaelewa kwa wengine. Ni kwamba ukiwa na ndugu mwenye tabia ya ndugu yangu huyo, mwimbie wimbo wa madhara ya pombe bila kuchoka; usimwaje ajiamulie kila kitu freely hata kama ni mtu mzima.
Hapo madhara yake ni nini, hujaeleza.
 
Kwa hiyo amerudia kijijini baada ya kutoka kulipagania Taifa ama sijaelewa mimi jamani?
Hili siyo swali la lazima sana; ila baada ya vita alianzisha biashara ya mbao akawa anazikusanya kutoka kwa wapuasaji mmoja mmoja huko vijijini na kuzisafirisha mjini. Kwa hiyo alijega maisha yake huko kijijini na alikuwa na maisha mazuri kabla pombe haijamtawala. Ndiyo maana ninapingana na wanaokimbilia kusema ni madhara ya vita.
 
Pole sana ingawa wajeda wana pension zao na hulipwa kila mwezi
Huenda ni mambo aliyoyaona na kupoteza marafiki zake akaamua kunywa tu
Muombee sana ingawa umemkashifu sana na kumsema
Ndugu yako ila hukuweka mda hata wa kukaa nae au kumchukua
Pole ila ungeufuta tu huu uzi haina haja ya kuandika yote hayo
 
Hili siyo swali la lazima sana; ila baada ya vita alianzisha biashara ya mbao akawa anazikusanya kutoka kwa wapuasaji mmoja mmoja huko vijijini na kuzisafirisha mjini. Kwa hiyo alijega maisha yake huko kijijini na alikuwa na maisha mazuri kabla pombe haijamtawala. Ndiyo maana ninapingana na wanaokimbilia kusema ni madhara ya vita.

Kaka yako alipata tatizo la Akili Alcoholic is mental illness.
 
Ni kweli alikuwa alchoholic,

Hilo ndilo tulilochelewa; Alchoholism inatibiwa kwa counseling, jambo ambalo hatukulifanya effectively. Tulimwacha ajiamulie maisha yake kuhusu pombe na ndiyo maana sasa hivi ninaomboleza hapa.
 
Back
Top Bottom