Nimepoteza simu Polisi wameshindwa kunisaidia kabisa

mimi nilipoteza simu ile naenda chukua loss report polisi aliekuwa kwenye reception akaniomba rushwa walah nilichoka
 
Simu zangu mbili kwa nyakati tofauti nawakabidhi Polisi IMEI hazikupatikana hadi kesho, zaidi wanakusajili na kukuomba uwaachie mawasiliano yako ndo imetoka hivyo! Ifike mahala TCRA wapewe nguvu na wawe na ofisi kila Mkoa wadili na vitu kama hivi
 
Huwa nakua makini sana na simu, ikipotea ishu za kuanza kurusisha taarifa zangu huwa inanikera sana.

Ikiibiwa ndo basi imeenda hiyo, polisi pesa inakutoka na simu hupati.

Ila kuna uzi humu watu wanashuhudia walivyozipata simu zao kwa haohao polisi au watu wao wa karibu.

Search nyuzi kuhusu kupoteza simu si ajabu ukaambulia nondo mbili tatu.
 
Me yangu niliipata. Lkn nilitumia askari kanzu. Only 1 day...wakati huo polisi walishanizungusha zaidi ya week 2..na nilikuwa na kila kitu hadi risiti nilizonunulia na box la simu lenye sticker za imei namba.
Nilitoa kitu kdg kwa askari kanzu lkn na me pesa yangu ilirudi toka kwa mwizi wangu alokutwa nayo
 
Una bahati ,mi nimeenda polisi receptionist wa kike wana nyodo balaa ,nikasema siku wakijichanganya na mimi kuja ofisini kwangu wataona maana watz sisi ni wajinga sana mtu akishakuwa kwenye ofisi ya umma position fulani anaona wengine wote ni takataka
 
Tatizo hilo...
Me nilipofika tu nilikutana na mtu ninaemjua nikasaidiwa kulog complaint yangu fasta
Sema kwenye ufuatiliaji ndio ikawa kipengele mpk nilipotumia askari mwengine. Na siku ya pili tu akanipigia simu nikaenda kituo kilekile nilipopeleka taarifa. Mimi pia kutokana na kazi yangu najuana na watu wengi sana so sehemu nyingi nikienda sipati tabu
Mkuu hio ni Zenji lkn sio huko Dar kwenu...kwenye mambo mengi
 
Yaaaani JESHI la polisi Kwa ujumla sio lakuamini maana hawafanyi kazi Kwa ajili ya raia na mali zao, Bali wanafanya kazi Kwa ajili ya viongozi wa CCM na mali zao.
 
Ukipoteza simu usiwategemee police kweli. Mtu wangu wa karibu alienda police wakaipata na faini akapigwa ailiyoiba lakini simu hakurudishiwa na taarifa hkupewa. Siku akamkamata nayo huyo police
Duu! akamuachia?.
 
Wewe ulifanikiwa Kwa SABABU ya kujuana. Je Kwa mtu ambaye hajuani na mtu maana yake hawezi kupata huduma. Polisi wapo Kwa ajili ya kulinda viongozi na mali zoa ila sio Kwa ajili ya Raia na mali zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…