Nimepoteza uwezo wa kujiamini kabisa na sielewi hatma yangu

Kwaninavyo fikiri ni kuwa huna malengo kwa kifupi umeridhika pengine hapo ulipofika ndo ulipokuwa umejiwekea malengo kabla hivyo unajiona ushatimiza kila kitu. Jaribu kupanga malengo mapya naamini yatakupa msukumo wa kupambana zaidi ili uweze kuyatimiza
 

Pepo la mauti linakuandama, sikiliza mkuu jifunze kuacha kuwaza kujitoa roho maana sio solution, solution hapa nikulikabili tatizo, unavyojisikia ni kama bado unakosa kuwa mwanaume timilifu, hakuna mwanaume anaekata tamaa haraka bali uvumilivu na kupambana
 
Unajua kuwaza kukata tamaa ni udhaifu mkubwa sana mwanadamu kuwaza hivyo, unatakiwa uwaze mazuri juu ya maisha yako
 
Maandiko yanasema Mungu alikujua wewe ungali upo tumboni mwa mama yako, amekuleta duniani anajua u utakua mtu fulani, amekupitisha vikwazo vingi kama ungekua ni wa kufa ungekufa muda tu
 
Halafu jifunze sana kuwaza tofauti, mambo ya kuwaza marafiki wamekukimbia hao hawakuwa ni marafiki, ujue kabisa hao walikua sio marafiki, hakuna rafiki wa dhati akakuacha wakati wa shida, jaribu kuwa na marafiki wa faida sio rafiki mpaka uwe nacho ndiyo unamuona
 
Epuka sana muda wa kuwa peke yako, huo ni muda wa shetani, muda wa peke yako au upweke ni mbaya sana ni muda wa shetani kukutumia na kukujeuza kuwa mdhambi na kujiwazia vibaya
 
Hakuna mtu aliezaliwa tajiri watu hupambana, na matajiri wangekupigia stori zao mpaka wanafika pale ungeshangaa watu hupitia magumu kufikia mahali fulani, hakuna maisha marahisi
 
Hili ndio nalihisi. Kumbuka nimeshatafuta, nimejenga na Nina maeneo ambayo naweza kuyafanya mtaji ila nipo tu. Mwili na akili havinaushirikiano kabisa.
Hapa ndio unapokosea..ni kweli umerogwa na aliyekuroga ni wewe mwenyewe kwa imani na fikra yako hii.
Thought shape Reality, kama unaona umerogwa basi utaishi Hivyo hvyo maana we Create our own demons...
Hakuna kurogwa wala nini change mindset yako kwanza
 
Asante mkuu
 
Hakuna maisha marahisi mzee, tambua kuwa wewe ni mwanaume, na sifa kuu ya mwanaume ni kupambana mzee na sio kukata tamaa
 
Asante mkuu. Ila naanzia wapi? Mwili hautaki, akili haitaki, najitahidu sana kufanya mazoezi lkn wapi. Sina furaha kabisa
 
Jiulize mbona hujafa mpaka sasa kama kweli ulikua ni wa kufa,.... Nimekushauri kama utachukulia poa utajiangamiza
 
Mkuu ishu yangu Mimi na mambo ya siasa haviendani kabisa. Kwanza Mimi siamini km siasa zinaweza kuwa na muingiliano na utafutaji wangu.
Nisome vizuri ni kwamba hari yangu yaupambanaji imeshuka kwakiwango chakutisha. Pamoja na kuwa rasirimali Ninazo.

Kama hujui na kuamini kuwa shughuli zako zinaathiriwa na siasa unafikiri utajua hatma yako kama hujui jambo dogo kama hilo?

Hujui siasa ndio maendeleo?
Hujui siasa ndio hukuletea wateja au kukupunguzia?
Hujui siasa zinaweza kukufanya upate faida nyingi au ndogo katika biashara zako?

Wewe kama huoni hayo basi jua bado hujajitambua, na maisha yatakuendesha mpaka akili ikukae.

Mimi mijitu kama hii ikijaga kuomba msaada kwangu, huwa naiuliza maswali machache nikishajua naongea na punguani, nakufukuza kama paka shume upeleke upunguani wako huko.
 
Hakuna mtu aliezaliwa tajiri watu hupambana, na matajiri wangekupigia stori zao mpaka wanafika pale ungeshangaa watu hupitia magumu kufikia mahali fulani, hakuna maisha marahisi
Mkuu km umenisoma vizuri ni kuwa nimepoteza hari ya mapambano. Nimekuwa tofauti na asilia yangu. Moyo wangu umejawa na uoga na kutojiamini. Kiumri bado ni kijana na nimepambana vilivyo. Nilipotoka ni pagumu kuliko hapa nilipo. Na kwamtazamo wa wengi wanaonizunguka ( majirani) wananiona Mimi boss flan. Ila ukweli ndio huo hapo juu.
huwa siwezi kumwambia mtu undani washida zangu.
 
Wewe umeathirika na siasa ila siasa ni ajira za watu mkuu. Watu wanakunja 12m per month.
Siasa sio sababu ya Mimi kujifungia ndani. Matatizo yangu hayajaletwa na mbunge wala Rais.
Kwangu Mimi nchi ikiwa tulivu na amani basi ni bonge la fursa kwamwananchi.
 
Mkuu,tafuta msaada wa kiroho,iko shida na tayari roho ya uharibifu inafanya kazi,nitumie ujumbe 0624689136
Nitakusaidia
 


Sasa hiyo fursa mbona huitumii unakuja kulia lia huku kuwa biashara inafilisika? Alafu bado unajiona mzima, nenda kwa wataalamu wa saikolojia.

Kama ungekuwa na akili ungejiuliza hao wanaokunja hizo 12m per monthly nini kinawafanya walipwe pesa yote hiyo, lakini kwa upunguani wako unaona ni sahihi wakati wewe huna mbele wala nyuma.

Unalia biashara inafilisika na nina uhakika hata TRA Hawajaisajili hiyo biashara yako,
Hujui hata kodi inakuathiri vipi wewe kama mfanyabiashara,

Mkuu hawa wanaokufariji ndio hawajaelewa wanamfariji mtu wa dizaini gani. Mimi naomba uzidi kuchapika akili ikukae sawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…