Nimepoteza uwezo wa kujiamini kabisa na sielewi hatma yangu

Atunusuru na kikombe hiki!?
Kwamba amnyakue jiwe?
 
Mbaya zaidi nimekuwa mtu wa kushinda ndani muda mwingi sana. Nimekuwa mpweke balaa.
Tatizo Lipo Hapo. Hakuna tatizo la mtu mmoja. Toka nje uone wenye matatizo wengine ili upate sababu ya kusonga mbele. Epuka sana kukaa mwenyewe kwani waweza dhani matatizo yote ya dunia umeyabeba wewe.
 
Pole bro. Iyo hali tumepitia wengi. Tena mengine zaidi ya hayo, kikubwa ni kusimamia kusudi au malengo uliojiwekea kabla ya hayo mapito. Be positive, stay focuse on your future..
Pia ni chanika maeneo gani upo?
Nipo chanika Videte, biashara unazofanya ndio nadili nazo pia. Kama itakufaa tufanye kitu, as a team
 
Kuna kaugonjwa kanaitwa The Fear of the unkonown.

kuna kitabu kjnaitwa Fear of the Unknown, jaribu kukitafuta online ukisome. Kitakusaidia
 
Mkuu ishu yangu Mimi na mambo ya siasa haviendani kabisa. Kwanza Mimi siamini km siasa zinaweza kuwa na muingiliano na utafutaji wangu.
Nisome vizuri ni kwamba hari yangu yaupambanaji imeshuka kwakiwango chakutisha. Pamoja na kuwa rasirimali Ninazo.
kwanza habari za hapo Zingiziwa maana kuna mdogo wangu maeneo hayo
Umeambiwa ni SIASA naomba uamini maana hilo dude ni kubwa kuliko wewe unavyolidhani kuwa mpaka uwe shabiki wa Chama fulani
Upepo wa kisiasa una mambo kwani kwa awamu ya kwanza hakukuwa na biashara za maduka kabisa yalikuwepo ya Ushirika
awamu zilizofuata biashara ilishamiri mpaka tukaweka pesa kwenye soksi
Kwa sasa biashara imebanwa ni kote sio kwako tu, tuelekepo kwa Siasa hizi wote watafunga wabaki wamachinga
Kwa vile una mke na watoto, tafuta chanzo kingine cha mapato, Kata kitambulisho ingia minadani kusanya kukuau mbuzi au hata mihogo hutakutana na hilo dude, Mkeo mfungulie mgahawa siku huendi shinda naye hata akiuza supu kodi hakuna
 
huna akili broo acha kumshauri ndg yetu vibaya....
 
muombe mungu mkuu yote yatapita.
 
Kusingizia siasa ni kuongeza ugonjwa mwingine. Ila nimeupenda ushauri wako wamwisho.
Asante
 
Kuna kaugonjwa kanaitwa The Fear of the unkonown.

kuna kitabu kjnaitwa Fear of the Unknown, jaribu kukitafuta online ukisome. Kitakusaidia
Tatizo kidhungu.
Km umekisoma nipe mistari. Ntashukuru mkuu
 
Chanika msumbiji kiongozi.
Asante sana.
 
Wewe sio level yangu.
Hata ivo ng'ombe hawezi kukonda hadi afanane na mbuzi.
 
watu wengi hawana furaha,watanzania wako very depressed awamu hii kwa sababu ya SIASA sasa we jifanye huijali ila asilimia 90 inasababisha haya matatizo tuliyopo
 
Daah...
 
watu wengi hawana furaha,watanzania wako very depressed awamu hii kwa sababu ya SIASA sasa we jifanye huijali ila asilimia 90 inasababisha haya matatizo tuliyopo
Hakuna nchi nzuri kisiasa km Tanzania.
Ukitaka kujua kwako kukoje angalia kwajirani
 
Hakuna nchi nzuri kisiasa km Tanzania.
Ukitaka kujua kwako kukoje angalia kwajirani
hao unaosema wanalia uchumi mbovu ushaawaambia hayo maneno?nchi nzuri sana tena sana tu watu wanalalamikia sera za awamu hii ushaona mtu analalamikia nchi ?
Nyie ndo wale Tundu lissu akimlaumu ndugai mnasema anaitukana nchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…