Behaviourist
JF-Expert Member
- Apr 8, 2016
- 39,926
- 95,626
Ametoroshwa na mwanaume wa hapa JF!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Na uishe tuKwahiyo mwaka unaisha hivihivi?!
Dah!...kweli unajua kuniumizaNa uishe tu
Fuatilia tu kama Yuko salama. Mengine hayakuhusu tafuta pesa,tafuta pesa tafuta pesa tafuta pesàaaaaaNafanya kazi mbali na ninapoishi kwa hiyo huwa ninalala huko ninakofanyia kazi ambako nimepanga chumba cha dharura.
Siku ya jtano wiki hii niliagana na mke wangu kuwa naelekea kazini na nitarudi siku ya alhamisi au ijumaa akaitikia na tukaagana vizuri.
Mshtuko wa moyo nilioupata ni pale nilipojisikia kurudi siku ya pili yake yaani Alhamisi baada ya kugonga mlango kwa muda bila majibu nikaamua niulize jirani aliko mke wangu, najibiwa jana ulipoondoka mkeo nae kasafiri ila funguo hizi hapa. Nilihisi kuishiwa nguvu lakini nilijikaza nikachukua ufunguo taratibu nikaingia ndani kiukweli sijaamini macho yangu hakukua na kitu chake hata kimoja zaidi ya kuniachia picha za ndoa.
Nimeumia sana na huo ulikuwa mwisho wa kupata usingizi hadi sasa. Nimempigia simu lakini haipatkani, ndugu zake hawajui yuko wapi ila leo hii Jumamosi mpangaji mmoja kanionea huruma kaniambia aliongea na mke wangu siku ya Alhamisi jioni na alimfahamisha kuwa anakaribia kufika kwao Chamwino Dodoma akitokea kwetu Mtwara.
Lakini kwao nikiuliza naambiwa haonekani na simu hapatikani, sijui cha kufanya kwanini mke wangu wa ndoa lakini amenitoroka. Naombeni mnishauri nini nifanye kwa kuwa suala hili limevuruga kichwa changu.
Mara ya mwisho kuwasiliana nae ilikuwa jioni Alhamisi kwa kum SMS kupitia private Facebook nikamuuliza uko wapi? Akanijibu kwa kifupi "my lovely husband ".Mpaka sasa simpati kwa simu.
Hali yangu kimaisha ni kawaida kwa kuwa nina kila chakula kinachohitajika nyumbani lakini pia huwa ninanunua samaki wanakuwepo kwa friji hadi anaondoka walikuwepo. Labda ana kitu moyoni lakini si angesema baada ya kufika kwao?Bro tuambie ukweli, jibu maswali haya:
1. Una hali ngumu kimaisha? (Kama ndio, Usijali ni mapito)
2. Ana kitu moyoni hakijamtoka? Labda mligombana
3. Wewe mwenye tabia zako ni zipi?
Ushauri: mtafute huyo mpangaji aliyepokea simu ya mkeo na kusema anakaribia kwao uongee naye vizuri....kwa vyovyote vile atakuwa kamwambia kwanini kaondoka. Wanawake hawana siri atakwambia tu....kama aliweza kukwambia hivyo basi kuna vingine anaficha. Ongea vizuri na mpangaji huyo.
Ikifika masaa 24 katoe taarifa polisi. Halafu kausha hao ndugu zake wasikusumbue-usipokee simu zao.
Pole brotherHali yangu kimaisha ni kawaida kwa kuwa nina kila chakula kinachohitajika nyumbani lakini pia huwa ninanunua samaki wanakuwepo kwa friji hadi anaondoka walikuwepo. Labda ana kitu moyoni lakini si angesema baada ya kufika kwao?
Mimi pia niligusia suala la pesa za matumizi kwenye comment yangu,napesa uliacha,kiufupi siri kubwa unayo wewe mwenyewe.kuna mlolongo wa mambo ulikuwa unahesabiwa bila wewe kujijua.Pesa niliacha na hakuchukua hata sent yangu.