Nimerudi kazini sijamkuta mke wangu, nauliza majirani naambiwa ameondoka kwenda kwao

Nimerudi kazini sijamkuta mke wangu, nauliza majirani naambiwa ameondoka kwenda kwao

Ulitekeleza ahadi zako ulizomuahidi wakati wa uchumba?

Kama uliiga utendaji wa ccm usitegemee mkeo aonyeshe uzalendo.
Pambana na hali yako.
 
Kuna jinsi tu unawajibika kwa kuondoka kwake jitafakari
 
mke anauma bhana; yalishanikuta pole mkuu' mwombe mungu atasaidia, kama alikupenda atoweza kuishi kwaaman atarudi tu. kilicho mkimbiza ni upweke tu wa kulala mwenyewe, hapo choma nauli nenda kwao.
 
Mh Leo wewe in mtu wa pili naskia habari hizi...kama hujazaa nae..hapo mzee wa kazi Anza na corolla, Anza maisha upya huko Facebook ulikomuona mwambie asirudi, maana ana vinasaba vya ujambazi huyo..achana nae na hata akitaka kurudi au akirudi na wewe akute ushahama, mfano umeamia lindi.
 
Kama hakuchukua pesa ni ishara kuna ugomvi mkubwa na wewe ndiwe mkorofi, jirekebishe kwa kila unalomkwaza mwenzako. Usitumie ubabe, usimnyanyase, usimsimange, huyo ni ubavu wako wa pili.
Kweli kitendo cha kutochukua Pesa kina onyesha wewe unamkwaza mwenzako fanya umtafute ujirekebisha hakikisha anasema lilimkwaza msiyamalize juu juu tu
 
Nafanya kazi mbali na ninapoishi kwa hiyo huwa ninalala huko ninakofanyia kazi ambako nimepanga chumba cha dharura.

Siku ya jtano wiki hii niliagana na mke wangu kuwa naelekea kazini na nitarudi siku ya alhamisi au ijumaa akaitikia na tukaagana vizuri.

Mshtuko wa moyo nilioupata ni pale nilipojisikia kurudi siku ya pili yake yaani Alhamisi baada ya kugonga mlango kwa muda bila majibu nikaamua niulize jirani aliko mke wangu, najibiwa jana ulipoondoka mkeo nae kasafiri ila funguo hizi hapa. Nilihisi kuishiwa nguvu lakini nilijikaza nikachukua ufunguo taratibu nikaingia ndani kiukweli sijaamini macho yangu hakukua na kitu chake hata kimoja zaidi ya kuniachia picha za ndoa.

Nimeumia sana na huo ulikuwa mwisho wa kupata usingizi hadi sasa. Nimempigia simu lakini haipatkani, ndugu zake hawajui yuko wapi ila leo hii Jumamosi mpangaji mmoja kanionea huruma kaniambia aliongea na mke wangu siku ya Alhamisi jioni na alimfahamisha kuwa anakaribia kufika kwao Chamwino Dodoma akitokea kwetu Mtwara.

Lakini kwao nikiuliza naambiwa haonekani na simu hapatikani, sijui cha kufanya kwanini mke wangu wa ndoa lakini amenitoroka. Naombeni mnishauri nini nifanye kwa kuwa suala hili limevuruga kichwa changu.

Mara ya mwisho kuwasiliana nae ilikuwa jioni Alhamisi kwa kum SMS kupitia private Facebook nikamuuliza uko wapi? Akanijibu kwa kifupi "my lovely husband ".Mpaka sasa simpati kwa simu.
Pole sana
 
Back
Top Bottom