Nimerudi kazini sijamkuta mke wangu, nauliza majirani naambiwa ameondoka kwenda kwao

Nimerudi kazini sijamkuta mke wangu, nauliza majirani naambiwa ameondoka kwenda kwao

NADHANI WIMBO WA CHRISTIAN BELA UNAKUFAA

Ameondoka aah, huku nyuma hali yangu siyo shwari..

HALAFU AKIRUDI WEKA ULE

Amerudi analia eh...

USICOMPLICATE MAMBO, ISHI KIPWANI
 
Huyo kapata kidume kamdanganya cha muhimu toa taarifa polisi. Halafu punguza kupenda penda sana.
 
huyo asikuumize kichwa fikiria maisha yako.
We ungeweza kuvumilia,
Upate mkeo mzuri mzuri halafu ana wowowo kubwa zuri, mweupe peee.... Atoroke halafu aje mtu kukuambia kuwa uachane naye ufanye maisha yako, hivi utareact vipi.... ?? [emoji16] [emoji51] [emoji119] [emoji119]
 
Ameenda sehemu moja amazing ndiyo maana akakujibu
" my lovely husband "
Hivyo usiwe na shaka....
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] mwenzio anakwambia hapati usingizi halafu wewe unamdhihaki, aaamkuu

Na wewe unamwamini kuwa hapati usingizi kweli?? angewezaje kuandika uzi huu bila hata kosa moja??
Nenda na wewe kwenu hakuna maana kuangalia tu picha za arusi. Akikuandikia huko facebook nawe mjibu "my lovely wife wangu"
 
Pole mkuu nafikiria mawazo uliyo nayo juu ya swala hili,maumivu na wakati mwingine hasira.mapenzi yaacheni yenyewe maana yana nguvu kuliko mwako wa moto.

~Omba ruhusa kazin kwako,jaribu kwenda kwao hata kuwa ghafla utajua yupo au hayupo.si wote hawakuoendi kwenye hiyo familia wapo watakuibia sir.

~Mtafute rafiki ake wa ukweli muulize kwa upole na upendo,mbembeleze atakwambia tu ukweli wote na mipango namna ilivo kuwa.

~Kufunga ndoa na mtu hakumfanyi asifanye ujinga hapana ila kumbuka kuwa na mwanadamu na anakosea km ww.

~Tanguliza msamaha kwanza na ukumbuke kuwa ni mkeo.kwa hali yoyote,mahali popote utakapo mkuta na chochote utakachokuta anafanya UMSAMEHE.

~Nb;katika shida na raha,maradhi na uzima nk.tena hadi kifo kitutenge.ee Mungu tusaidie.(ukumbuke hiki kitanzi)
 
Ndoa hata mtoto bado unaniacha pekee yangu, Kwa nini usikae naye hilo geto la kazini? Mwache ajiondokee.
 
Mkuu mkeo ulipomuuliza uko wapi, si alikujibu kuwa yuko kwa "my lovely husband" sasa wewe unaulizia kwao wakati kakuambia kuwa yuko kwa mme wake anaempenda.

Jikaze bro endelea na maisha yako
 
Pole sana mwanajf mwenzangu!
Sijui mlikuwa na ugimvi kabla ya yeye kutoroka kama upo wala usiumie tafuta namna ya kumpata na kusolve lakini kama kaondoka kwa sababu zake binafsi mwache aende atarudi akichoka
Akichoka Arudi kwa nanii
 
Pole sana though ni ngumu kujua sababu kuu hasa iliyomfanya aondoke hapa tutaguess tu

By the way hamkuwa na migogoro??



Cc Smart911
 
Pole sana jomba, kama wengi walivyokushauri ripoti polisi ili isirudi kwako kinyume. Kingine kama kweli Hamna ugomvi wowote, ulikuwa unamtimizia yote mfano kumpatia penzi tamu kitandani, chakula, mavazi, malazi na afya safi?! Kingine kikubwa hukuwa na gubu naye... Basi nina mashaka jinsi mlivvo kubaliana toka mwanzo hadi kuoona. Je, alilazimishwa kwe mahusiano? Jicheki tu hapo. Pungufu ya hapo nina mashaka karudiana au kapata mume anayekuzidi hayo hapo juu niliyoanza nayo.
 
Kuna namna unawajibika katika hili, inaonekana hata wazazi wake na ndugu zake hawakupi ushirikiano, lazima unaangukia kati ya hivi vifuatavyo:

- Wewe bahili sana na humjali.
- Maisha magumu sana na imekuwa ngumu kumtimizia maitaji.
- U mgovi sana, umekuwa unamsulubu mtoto wa watu vibaya.
- Wewe ni muhuni sasa, kashindwa kukaa!

Kama haya yote sio sahihi, niambie then nitakushauri, ila sidhani!
Kama hakuchukua pesa ni ishara kuna ugomvi mkubwa na wewe ndiwe mkorofi, jirekebishe kwa kila unalomkwaza mwenzako. Usitumie ubabe, usimnyanyase, usimsimange, huyo ni ubavu wako wa pili.
 
Mkuu si alikujibu kuwa yupo kwa "her lovely husband" ila pole sana. Barnaba aliimba "mapenzi yanaumaaaa ehhh"
 
Mkuu mtwara upo sehemu gani Kuna Bar pale maeneo ya nangwanda inaitwa shooters, kesho Kuna Manchester united vs Manchester City saa 1 usiku, tujumuike pale pamoja Kupata ulabuu mkeo kwa kifupi tuu anatafuniwa Sasa na hii hali ya hewa za mvua mvua na anatafunwa huko alipo.
Hivi unafahamu ulichokiandika hapa? Hujakutwa na haya mambo mkuu bora ukae kimya
 
Back
Top Bottom