Nimerudi kazini sijamkuta mke wangu, nauliza majirani naambiwa ameondoka kwenda kwao

Mkuu umemuangalia ndani vizuri hayupo kabisa? Nakushaur tafta simu yake umchajie pengne imeisha charge ndo mana haipatkan.
 
Wkati unaandika haya kumbuka ni siku ya uhuru so kichwa chako nacho kiweke huru!
Mwanamke siyo ndugu yako, hujasema kama ulibahatika kupata naye mtoto/watoto kama jibu ni hakuna basi hakuna haja ya kumtafuta japo unaonekana kumpenda lkn yeye hakuthamini.
Kifupi ganga yajayo,narudia tena na wewe usimtafute
 
Nafanya kazi mbali na ninapoishi kwa hiyo huwa ninalala huko ninakofanyia kazi ambako nimepanga chumba cha dharula.Siku ya jtano wiki hii niliagana na mke wangu kuwa naelekea kazini na nitarudi siku ya alhamisi au ijumaa akaitikia na tukaagana vizuri. Mshtuko wa moyo nilioupata ni pale nilipojisikia kurudi siku ya pili yake yaani alhamisi baada ya kugonga mlango kwa muda bila majibu nikaamua niulize jirani aliko mke wangu,najibiwa jana ulipoondoka mkeo nae kasafiri ila funguo hizi hapa..!.Nilihisi kuishiwa nguvu lakini nilijikaza nikachukua ufunguo taratibu nikaingia ndani kiukweli sijaamini macho yangu hakukua na kitu chake hata kimoja zaidi ya kuniachia picha za ndoa. Nimeumia sana na huo ulikuwa mwisho wa kupata usingizi hadi sasa. Nimempigia simu lakini haipatkani,ndugu zake hawajui yuko wapi ila leo hii jumamosi mpangaji mmoja kanionea huruma kaniambia aliongea na mke wangu siku ya alhamisi jioni na alimfahamisha kuwa anakaribia kufika kwao Chamwino Dodoma akitokea kwetu Mtwara. Lakini kwao nikiuliza naambiwa haonekani na simu hapatikani,sijui cha kufanya kwani ni mke wangu wa ndoa lakini amenitoroka. Naombeni mnishauri nini nifanye kwa kuwa suala hili limevuruga kichwa changu. Mara ya mwisho kuwasiliana nae ilikuwa jioni alhamisi kwa kumsms kupitia private Facebook nikamuuliza uko wapi? Akanijibu kwa kifupi "my lovely husband ".Mpaka sasa simpati kwa simu.

Kuna namna unawajibika katika hili, inaonekana hata wazazi wake na ndugu zake hawakupi ushirikiano, lazima unaangukia kati ya hivi vifuatavyo:

- Wewe bahili sana na humjali.
- Maisha magumu sana na imekuwa ngumu kumtimizia maitaji.
- U mgovi sana, umekuwa unamsulubu mtoto wa watu vibaya.
- Wewe ni muhuni sasa, kashindwa kukaa!

Kama haya yote sio sahihi, niambie then nitakushauri, ila sidhani!
 
Yapo mambo tulikuwa tunatofautiana lakini huwa tunakaa sawa.Hiyo siku aliyoondoka hatukuwa na ugomvi kama sikosei.
-mke wangu hakuchukua pesa yoyote je nauli kaitoa wap?
-nahisi ndugu wanahusika ila kwa nini wananiulizia ndugu yao aliko?
-alimpigia simu mpangaji kuwa bado kidogo afike kwao,sasa kwa nini hawawi wakweli?
 
Chamwino yupo baba jessica bado, mwambie kwa kutumia njia zake waende nyumba kwa nyumba. Akirudishwa tu, hospitali kupima kila kitu kuanzia kichwa, utumbo, damu na kule mahala. Mnakaa miezi mitatu kila mtu na kitanda chake halafu mnarudi kupima tena. Ukijiridhisha yupo sawa, maisha yaendelee ila ukae ukijua, kama ni kichwa, hataacha ataendelea kutoroka tu.
 
Ushauri na majibu ya watu wengi kwenye uzi huu inaonesha ni jinsi gani watu wengi hawana utu na huruma pia inaonesha watu wengi ni wa mashala hata kwenye issue za msingi.
Sio vzr ndugu zangu, mna muumiza jamaa kwa majibu yenu ya kejeri hayo
 
The only solution ni wewe kwenda polis. Otherwise ndugu watakusumbua. Pia wagogo nawafahamu walivyo
 
Kwanza pole kwa matatizo mi nakushauri nenda polisi kwanza katoe taarifa baada ya hapo katoe taarifa kwenye vyombo vya habari. Ila jichunguze kwanza nahisi kuna something else unatuficha mtu aliyetimia akili hawezi tu kutoroka kama mwendawazimu.
 
Hivi mimi nitakuja kuwa na moyo wa kuhangaika hivi wakati mtu kafanya kitu cha kujitakia mwenyewe?

Maisha yalivyo magumu hivi halafu uanze kuumiza kichwa kumtafta mtu mzima?

Ushauri, toa taarifa serikali ya mtaa, polisi na kwa ndugu zake ikiwezekana andika maelezo polisi ili iwe reference halafu tulia upambane na maisha. Acha ujinga
 
Nafanya kazi mbali na ninapoishi kwa hiyo huwa ninalala huko ninakofanyia kazi ambako nimepanga chumba cha dharula.Siku ya jtano wiki hii niliagana na mke wangu kuwa naelekea kazini na nitarudi siku ya alhamisi au ijumaa akaitikia na tukaagana vizuri. Mshtuko wa moyo nilioupata ni pale nilipojisikia kurudi siku ya pili yake yaani alhamisi baada ya kugonga mlango kwa muda bila majibu nikaamua niulize jirani aliko mke wangu,najibiwa jana ulipoondoka mkeo nae kasafiri ila funguo hizi hapa..!.Nilihisi kuishiwa nguvu lakini nilijikaza nikachukua ufunguo taratibu nikaingia ndani kiukweli sijaamini macho yangu hakukua na kitu chake hata kimoja zaidi ya kuniachia picha za ndoa. Nimeumia sana na huo ulikuwa mwisho wa kupata usingizi hadi sasa. Nimempigia simu lakini haipatkani,ndugu zake hawajui yuko wapi ila leo hii jumamosi mpangaji mmoja kanionea huruma kaniambia aliongea na mke wangu siku ya alhamisi jioni na alimfahamisha kuwa anakaribia kufika kwao Chamwino Dodoma akitokea kwetu Mtwara. Lakini kwao nikiuliza naambiwa haonekani na simu hapatikani,sijui cha kufanya kwani ni mke wangu wa ndoa lakini amenitoroka. Naombeni mnishauri nini nifanye kwa kuwa suala hili limevuruga kichwa changu. Mara ya mwisho kuwasiliana nae ilikuwa jioni alhamisi kwa kumsms kupitia private Facebook nikamuuliza uko wapi? Akanijibu kwa kifupi "my lovely husband ".Mpaka sasa simpati kwa simu.
Mkuu Fanya kama sadaka hawa viumbe hawana shukran utambeba unavyombeba mwisho wa siku anakukimbia ndio hao kwa manung'uniko yako wanakutwa wamechinjwa kwenye mapagale na watu wasiojulikana.
 
Dodoma, Chamwino zipo mbili, kule ikulu ambako ni kwa wagogo na Ile ya mjini ambayo wamejaa warangi, kama ni mrangi huyo atarudi, Ila ujiandae kukaaaa, kama ni mgogo huyo sahau kesha olewa teyari
 
Katoe taarifa polisi na uchukue rb then weka mpira kwapan angalia maisha upande mwingine mzee mwenzangu.Hapo utakuta kuna mjanja zaidi yako anapelekewa kipochi manyoya we unaumiza akili zako
 
Mkuu pole sana. Ahirisha shughuli zako kwa muda. Nenda Chamwino kwa surprise. Zipo dalili utajionea zitakupa akili ya pili.
 
Dodoma, Chamwino zipo mbili, kule ikulu ambako ni kwa wagogo na Ile ya mjini ambayo wamejaa warangi, kama ni mrangi huyo atarudi, Ila ujiandae kukaaaa, kama ni mgogo huyo sahau kesha olewa teyari
Mkuu,umenivunja mbavu sana!
 
Mkuu pole sana. Ahirisha shughuli zako kwa muda. Nenda Chamwino kwa surprise. Zipo dalili utajionea zitakupa akili ya pili.
Kama dalili zipi?na jee hata wakwe nisiwadokeze ujio wangu?
 
Back
Top Bottom