Nimeshangaa kumuona Profesa mmoja maarufu wa pale UDSM akisali sala ya Bikira Maria

Nimeshangaa kumuona Profesa mmoja maarufu wa pale UDSM akisali sala ya Bikira Maria

Yohana 14:13
[13]Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana.

Yohana 16:24
[24]Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu.

Yohana 16:23-24
[23]Tena siku ile hamtaniuliza neno lo lote. Amin, amin, nawaambia, Mkimwomba Baba neno lo lote atawapa kwa jina langu.
[24]Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu.
 
Yani nina masters na sasa ni mwanafunzi wa PhD na ninampenda sana Mama Bikira Maria japo siwezi Kumzidi Yesu. Ninamuomba na ananisaidia sana, hakuna binadamu kama Yeye. Mungu kujimwilisha ndani yake wafanya mchezo? sala zake hazikataliwi huyo Mama. Tena subiri niandae rosary yangu nifanye meditation. Kwanza huwa napata amani ya ajabu nikisali rosary. Na sina mpango wa kuacha leo wala kesho.
 
Ngoja niweke kapicha cha kusindikizia uzi , watu wanaacha kuabudu Mungu wa kweli Kazi kuabudu viumbe wenzao #InasikitishaSanaView attachment 2465677

Nb: Huyo picha siyo mtajwa katika uzi bali ni mfano tu jinsi gani watu wanavyoabudu kivyao kama content ya uzi unavyosema.
Ukweli hata mie hili jambo huwa laniacha hoii
Hivi inakuaje mwana damu anatengeneza kinyago kisha anakiabudu?? Anaamini kabisa kitamsaidia
Daaaaaaah mambo ya imani bhanaaa saa ingine ni kama uchizi flani hiviii
 
Moja kati ya mambo ambayo yapo wazi kabisa katika biblia ni maelekezo ya namna maombi yanatakiwa kufanywa. Agizo la maombi lipo very open.

Yesu Kristo alisema mara nyingi sana kwenye injili ya Yohana kwamba tuombe kwa jina lake. Mtume Paulo ameandika tufanye yote katika jina la Yesu Kristo.

Sasa profesa ambaye ameandika paper kibao na amefanya literature review za kutosha ameshindwa kusoma biblia kufahamu tunapaswa kuomba kwa jina gani?

Hakuna sehemu hata moja mitume waliomba kwa jina la Maria. Yule Maria mama wa Yesu alikaa pamoja na mitume na walijazwa Roho Mtakatifu pamoja na wakanena kwa lugha.

Maria alimzaa Yesu lakini hakumzaa Mungu. Kuna tofauti kati ya Yesu na Kristo. Maria sio mama wa Mungu bali ni mama yake Yesu. Yesu ni mwanadamu na Kristo ni Mwana wa Mungu.

Hivyo Yesu Kristo ni Mungu na mwanadamu kwa wakati mmoja. Asomaye na afahamu.
Kila mtu ana Imani yake na uhuru wa kuabudu anachokiamini. Usimuamlie. Yaani kila mtu ashinde mechi zake.
 
I'm doubting about the invisible man in the sky, who loves you too much still he needs your money. Think twice!
 
Kwani wewe unadhani kwakua amefanya tafiti nyingi atakua ametafiti hata biblia?

Hata kama ni profesa lakini sio kwenye biblia. Kila mtu ana alipozidiwa haijalishi anajua nini
 
Yani nina masters na sasa ni mwanafunzi wa PhD na ninampenda sana Mama Bikira Maria japo siwezi Kumzidi Yesu. Ninamuomba na ananisaidia sana, hakuna binadamu kama Yeye. Mungu kujimwilisha ndani yake wafanya mchezo? sala zake hazikataliwi huyo Mama. Tena subiri niandae rosary yangu nifanye meditation. Kwanza huwa napata amani ya ajabu nikisali rosary. Na sina mpango wa kuacha leo wala kesho.
Natumia rosary kila asubuhi for meditation, kwasababu yoga ilinishinda...The best decision ever!
 
Moja kati ya mambo ambayo yapo wazi kabisa katika biblia ni maelekezo ya namna maombi yanatakiwa kufanywa. Agizo la maombi lipo very open.

Yesu Kristo alisema mara nyingi sana kwenye injili ya Yohana kwamba tuombe kwa jina lake. Mtume Paulo ameandika tufanye yote katika jina la Yesu Kristo.

Sasa profesa ambaye ameandika paper kibao na amefanya literature review za kutosha ameshindwa kusoma biblia kufahamu tunapaswa kuomba kwa jina gani?

Hakuna sehemu hata moja mitume waliomba kwa jina la Maria. Yule Maria mama wa Yesu alikaa pamoja na mitume na walijazwa Roho Mtakatifu pamoja na wakanena kwa lugha.

Maria alimzaa Yesu lakini hakumzaa Mungu. Kuna tofauti kati ya Yesu na Kristo. Maria sio mama wa Mungu bali ni mama yake Yesu. Yesu ni mwanadamu na Kristo ni Mwana wa Mungu.

Hivyo Yesu Kristo ni Mungu na mwanadamu kwa wakati mmoja. Asomaye na afahamu.
Acha wivu kwa Mama Bikira Maria.Ulitaka uombwe wewe?.Kaa kwa kutulia wewe kila mtu na anavyoamini.
 
Kumshangaa MTU anamwabudu mama maria mtakatifu ni sawa kumshangaa MTU anamsujudu Muhammad aliyekuwa na totoz kibao.Mi naona kila MTU asimamie imani yake
Acha kumfananisha Mama Bikira Maria na vitu visivyoeleweka bhana.
 
Leo tunasherekea Bikira Maria mama wa Mungu. Watu wanafikiri tukisema habari za Bikira Maria tunamuinua yeye kumbe Yesu ndiye anayehubiriwa! Mfano kama unaamini Yesu ni Mungu na alivaa mwili kupitia Bikira Maria huoni kuwa huyo mama ni mama wa Mungu? Unafikiri kama si kuwa mama wa Mungu angekuwa kama watakatifu wengine tu.

Kama ni kuokoka tunaweza kusema Bikira Maria ndiye binadamu wa kwanza kumpokea Yesu maana kwa utii wake neno wa Mungu akafanyika ndani yake baada ya kufunikwa na Roho Mtakatifu!

Watu wanapaswa kujua kwanini Wakatoliki huomba intercession ya watakatifu kabla ya kumshambulia maombezi kwa Bikira Maria. Ukielewa mahusiano yetu na watakatifu wa mbinguni then ukajua nafasi ya Bikira Maria hutochanganyikiwa tena.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
Umeeleza vizuri sana mkuu.Safi sana
 
Unaposoma kitabu tunategemea unapata maarifa na baadaye kutumia maarifa hayo ili kukurahisishia maisha yako. Hatutegemei ufuate yale tu uliyoyoyasoma bila kuwa na ongezeko lolote ulilolipata (maarifa) kutokana na kusoma kitabu hicho. Vinginevyo utakuwa hujaelewa ulichokisoma; utakuwa umekariri.

Tumwomba au kusali kwa kulitaja jina la Yesu Kristo, lakini pia tunaongezea maombi hayo kwa kumuomba Bikira Maria atuombee kwa mwanae. Ni sawa tu wewe unaweza kumuomba kitu baba yako, halafu ukamuomba mama yako amsihi baba yako akupe hicho unachohitaji!

Tusikariri mambo, tulipewa akili ili kuweza kujiongeza. Sio kwakuwa Biblia ilisema hivi, basi tuishie pale pale tu, hapana, tunyambulishe mambo!
Barikiwa sana mtumishi.
 
Mambo ya kiimani ni magumu sana hasa kama uelewi vizuri. Wao si wapumbavu wasali vile..
Ivi ushawishi jiuliza kwa jicho la tatu kwanini wanamtaja sana Maria.?
Nakupa hom work hiyo Mkuu.

Wewe uko sahihi na wao wako sahihi kutokana na maandiko waliyosoma..
Jibu la Kifalsafa hili.Big up sana.
 
Mkuu waliopo nje ya Kanisa Katoliki hawaelewi yaliopo ndani ya Kanisa hilo wamekaa kulishambulia tu badala ya kufanya analysis.

Wakatoliki tunamuomba Bikira Maria atuombee kama wao wanavyokwenda kwa Mchungaji wao na kumuomba wawaombee hata ile sala ya salamu Maria ipo ndani ya Biblia ni maumkuzi ya Malaika Gabriel aliyetumwa na Mungu kumpasha Maria kuwa atamzaa Yesu ''Salamu;uliyepewa neema;Bwana yu pamoja nawe"(Soma Luka 1:28)pia ni maneno ya Elizabeti aliyetamka maneno baada ya kujazwa na Roho Mtakatifu alipokuwa ametembelewa na Bikira Maria''Umebarikiwa wewe katika wanawake naye naye mzao wa tumbo lako amebarikiwa" (Soma Luka 1:42)
[emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]
 
Mama Maria Malkia wa Amani...Utuombee

Roman Catholic inawatesa sana halafu ajabu sisi hatuna shida naye i mean hatutaki kufahamu ya nyie mnaojihesabia Haki.

Kupitia Imani yangu ya Romani kusali rozari kwa Mama Bikira, kuabudu Ekaristi, kuhudhuria Misa Takatifu, kuwaombea Marehemu hakuna nliloomba Mwenyezi Mungu akaninyima

Kifupi wewe endelea kuamini huko kwako ndugu yangu

Ya waromani mtuachie waromani
[emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]Asante sana,Umeisimamia imani yako vizuri kabisa.
 
Niaze kwa kuomba radhi kwa waumini wa RC.Hapa ndipo huwaga nadhani waliotengeneza dhehebu la RC Kuna codes hazikusomana vizuri.
Mama Maria aliyemzaa Yesu alibaki kuwa mke wa Yusuf afterward na alifariki kama mwanadamu wa kawaida.So hapa ni kupoteza muda kumwambia marehemu akuombee.Ni kweli hatujui kuomba itupasavyo lakini,kazI ya kutuombea ni ya ROHO MTAKATIFU (Rumi 8:26).Mahusiano ya Mama maria na Yesu kristo ni mahusiano ya Mtu na Mungu wake.Unaweza usitake kuamini,ila ukweli ni kwamba Yesu kristo alishakuwako kabla sana hata ya kuzaliwa kwa Bikira Maria(Ndiyo maana ya utatu mtakatifu). Alichokizaa Maria ni mwili tu wa kibinadamu wa Yesu.

Hapa usipokuwa makini tunaweza tukamfanya mama Maria ni nafsi ya nne. Yaani kuna Mungu baba, Mungu Mwana,Mungu Roho Mtakatifu na Bikira Maria.
Luka 8.21(Mama yangu na ndugu zangu ni hao wanao lisikiliza neno la Bwana).

Sahamani lakini.kama kuna neno katika biblia linalothibitisha hili mnaweza kutusaidia.Ila kama ni logic tu za kibinadamu kwamba kwa kupitia kwa mama,mwana anaweza kukusikiliza maombi yako kirahisi ni upotoshaji.Ni bora ukaenda kwa mtumishi wa Mungu ukamuomba akuombee.
Wewe nenda tu kwa Gwajiboy akuombee,lkn mimi Fall Army Worm,nitashika Rozari yangu nitasali nikiomba Msaada wa Maombezi ya Mama Bikira Maria.
 
Back
Top Bottom