Nimeshangaa sana nilipokutana na hii kitu kwenye website ya Muhimbili National Hospital

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Muhimbili ambako maiti zinazuiwa kwasababu aliyekufa alipokuwa mgonjwa hajamalizia malipo.
Muhimbili ambako mgonjwa anakaa wiki nzima hajapata huduma kwakuwa hajalipia pesa ya kipimo hivyo madaktari hawawezi kumuhudumia mpaka apimwe . Na vipimo hajalipia bado.
Muhimbili ambako huduma bei yake iko juu kana kwamba ni mahali pa biashara.
Nao wanaomba michango na misaada kutoka kwa wahisani wa ndani na nje ya nchi.
This is madness
Screenshot_20241116-162407_1.jpg
 
Unachokisema ni kweli kama wiki mbili au tatu zilizopita Jirani yetu mmoja alifiwa na kijana wake kwa ugonjwa wa Leukemia hapo MNH na mwili ulikataliwa kabisa kutolewa bila mil 3 na ndugu wa huyo marehemu wana uwezo duni wa kifedha hivyo walijichanga na kufika kama laki 3 hivi na kupeleka aisee walipewa maneno magumu na kuambiwa wakajichange. Ndipo ndugu hao wakamtafuta mwenyekiti wa mtaa kuomba msaada ili asaidie maana siku zilikuwa zimepita kama mbili na ni waislamu ndipo alipomtafuta mkoa wa mkoa na kuingilia kati mpaka kupata mwili kuzika. RC Chalamila alionyesha utu sana aisee!
 
Mimi nauliza tu kwahiyo kama kila maskini atakuwa anamwendea RC au waziri mkuu au Rais kuomba msaada itakuwaje?
 
Pamoja na gharama zake ila pia walala hoi wengi wanatibiwa bure pale bila malipo yoyote.
Sijawahi kusikia mtu katibiwa bure pale , lakini pia wanapokea fungu kubwa la ruzuku hivyo pesa hizo za ruzuku zitibu hao walala hoi unaowasema maana sisi na ndugu zetu tukienda pale bili tunayolipa ni kubwa
 
Changamoto kubwa kwenye Afya sio tu Muhimbili hata kwenye Zahanati ni posho za watumishi. Serikali imejitoa kwenye hizi posho na kuziacha kwenye kituo husika. Hivyo ili posho ipatikane kwa madaktari na wahudumu wengine lazima hospitali ikusanye mapato. Hapo kwenye kukusanya Sasa ndipo kazi ilipo. Utaambiwa maiti anadaiwa milioni 2 inawezekana walimuekea drip ya 1500 na kumpa paracetamol za buku mtu akafa utathibitisha vipi hizo gharama?
Kuna mtu alipata ajali akapelekwa hospitali usiku saa 3, ndugu wakapigiwa simu kufika pale wakaambiwa anahitaji upasuaji hivyo gharama laki 5. Wamejichanga wamelipa, saa 5 usiku wanaambiwa amefariki. Upasuaji haujafanyika, hela mmelipa na mtu amefariki. Hapo inaingia bili nyingine ya motuary na dawa ya kuhifadhi maiti nje ya ile laki 5 waliotoa
 
Unachokisema ni kweli kama wiki mbili au tatu zilizopita Jirani yetu mmoja alifiwa na kijana wake kwa ugonjwa wa Leukemia hapo MNH na mwili ulikataliwa kabisa kutolewa bila mil 3 na ndugu wa huyo marehemu wana uwezo duni wa kifedha hivyo walijichanga na kufika kama laki 3 hivi na kupeleka aisee walipewa maneno magumu na kuambiwa wakajichange. Ndipo ndugu hao wakamtafuta mwenyekiti wa mtaa kuomba msaada ili asaidie maana siku zilikuwa zimepita kama mbili na ni waislamu ndipo alipomtafuta mkoa wa mkoa na kuingilia kati mpaka kupata mwili kuzika. RC Chalamila alionyesha utu sana aisee!
Jambo zuri sana kama RC alisaidia,
Lakini sasa iwe kila mtanzania wa hali ya chini ni mpaka apate huruma ya RC, vipi akimkuta RC siku hiyo ana stress za kunyimwa tendo na mwenzie.

Serikali iweke utaratibu, kila mmoja afaidike, asaidike kirahisi.
 
Mimi nauliza tu kwahiyo kama kila maskini atakuwa anamwendea RC au waziri mkuu au Rais kuomba msaada itakuwaje?
Haiwi kitu. Maana ulichokiwaza pia hakiwezi kuja kutokea kamwe. Cha zaidi sana serikali kupitia wizara ya afya inatakiwa kufanya namna ya kusaidia wananchi kupata huduma za afya kwa gharama nafuu.
 
Changamoto kubwa kwenye Afya sio tu Muhimbili hata kwenye Zahanati ni posho za watumishi. Serikali imejitoa kwenye hizi posho na kuziacha kwenye kituo husika. Hivyo ili posho ipatikane kwa madaktari na wahudumu wengine lazima hospitali ikusanye mapato. Hapo kwenye kukusanya Sasa ndipo kazi ilipo. Utaambiwa maiti anadaiwa milioni 2 inawezekana walimuekea drip ya 1500 na kumpa paracetamol za buku mtu akafa utathibitisha vipi hizo gharama?
Kuna mtu alipata ajali akapelekwa hospitali usiku saa 3, ndugu wakapigiwa simu kufika pale wakaambiwa anahitaji upasuaji hivyo gharama laki 5. Wamejichanga wamelipa, saa 5 usiku wanaambiwa amefariki. Upasuaji haujafanyika, hela mmelipa na mtu amefariki. Hapo inaingia bili nyingine ya motuary na dawa ya kuhifadhi maiti nje ya ile laki 5 waliotoa
Huu ni wizi
 
Taifa lako litajengwa na wewe mkuu chukulia huo mfuko ukitanuka kutakuwa na shida think positive
 
Weee
Nchi ilivyojaa rushwa hii ni mwehu tu atachangia kirahisi hivyo
Au mwenye pesa za majini na ujambazi.
Pale kama mlalahoi uko ICU unaweza kutolewa mpira wa oxygen akawekewa mjomba wake Nape ili ufe chap
 
Back
Top Bottom