Nimeshangaa sana nilipokutana na hii kitu kwenye website ya Muhimbili National Hospital

Ccm mbere kwa mbere
 
Pesa za kununua magoli mnazo ila za kuchangia matibabu kwa wananchi muombe mabeberu?
 
Sijawahi kusikia mtu katibiwa bure pale , lakini pia wanapokea fungu kubwa la ruzuku hivyo pesa hizo za ruzuku zitibu hao walala hoi unaowasema maana sisi na ndugu zetu tukienda pale bili tunayolipa ni kubwa

Unafanya kazi MNH? Wagonjwa wanaotibiwa bure kabisa wapo wengi tu. Nenda ofisi ya Ustawi wa Jamii utapata mkeka wote
 
Nashauri ili kuepuka hizi gharama, kila mtu akate bima ya afya
 
Piga simu namba 0715290137
ili kupata huduma ya vibaka watakaoweza kukuibia maiti ikikataliwa Muhimbili.
 
Taifa lako litajengwa na wewe mkuu chukulia huo mfuko ukitanuka kutakuwa na shida think positive
Weee
Nchi ilivyojaa rushwa hii ni mwehu tu atachangia kirahisi hivyo
Au mwenye pesa za majini na ujambazi.
Pale kama mlalahoi uko ICU unaweza kutolewa mpira wa oxygen akawekewa mjomba wake Nape
Kuna mtu pale muhimbili anaitwa mtoa roho maarufu sana kukataza vyakula, huyu jamaa akikutibu jua huponi,
Ahahahahh 🤣 🤣 🤣 🤣
Kwahiyo yeye ni mwendo wa kung'oa watu roho tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…