Nimeshangazwa kukamatwa kwa Ali Kamwe badala ya kijana Godi Yanga!

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
64,960
Reaction score
111,265
Nimeshangazwa sana kukamatwa na kushikiliwa katika kituo cha polisi kwa Ali kamwe kwa kile kinachodaiwa kutoa kauli za kudhalilisha viongozi.

Nimesikiliza hizo kauli za Ali Kamwe sijaona kauli yoyote ya kufanya akamatwe na polisi, wakati namsikiliza Ali Kamwe nimeweza kukutana na video nyingine ya kijana anayeitwa Godi Yanga akiwa katika shamra shamra za timu yake na mahojiano na mwandishi wa habari.

Katika mazungumzo hayo huyo Godi Yanga anasema msemaji wa timu ya Tabora anataka kuolewa na Ali Kamwe halafu anawauliza mashabiki wenzake kama anafaa au hafai kuwa shemeji yao kisha wote kwa pamoja kwa vifijo na nderemo wakakubaliana wamemchunguza na hafai kuwa shemeji yao.

Mimi kwangu hii ndio kauli ya udhalilishaji zaidi.
 
Una uhakika unaijua sheria kwamba hamna kosa alilofanya ?
 
Yanga mechi zifuatazo ni dhidi ya Coastal na Azam. Kuna mkakati unaongozwa na Mwambie Karihe kuwatoa mchezoni Ili wafungwe, warudi kucheza dabi!
 
Una uhakika unaijua sheria kwamba hamna kosa alilofanya ?
Kwani laazima niijue sheria kujua hii ni kauli ya udhalilishaji au sio?
Sheria ya udhalilishaji inahusika na viongozi tu?
 
Kwahiyo unasemaje Ali Kamwe ana kosa kisheria au hana kosa kisheria au haujui kama kavunja sheria?
 
Nimeshangazwa sana kukamatwa na kushikiliwa katika kituo cha polisi kwa Ali kamwe kwa kile kinachodaiwa kutoa kauli za kudhalilisha viongozi.

Nimesikiliza hizo kauli za Ali Kamwe sijaona kauli yoyote ya kufanya akamatwe na polisi, wakati namsikiliza Ali Kamwe nimeweza kukutana na video nyingine ya kijana anayeitwa Godi Yanga akiwa katika shamra shamra za timu yake na mahojiano na mwandishi wa habari.

Katika mazungumzo hayo huyo Godi Yanga anasema msemaji wa timu ya Tabora anataka kuolewa na Ali Kamwe halafu anawauliza mashabiki wenzake kama anafaa au hafai kuwa shemeji yao kisha wote kwa pamoja kwa vifijo na nderemo wakakubaliana wamemchunguza na hafai kuwa shemeji yao.

Mimi kwangu hii ndio kauli ya udhalilishaji zaidi.
Unajua maana ya kudhalilisha,
Lazima uwe na status katika jamii,sasa huyo dada ana status gani kwenye jamii
 
Msemaji wa timu hana status kwenye jamii??
 
Kwani laazima niijue sheria kujua hii ni kauli ya udhalilishaji au sio?
Sheria ya udhalilishaji inahusika na viongozi tu?
Hakuna udharirishaji hapo kusema hafai Ndio kosa gani?
 
Chokochoko alizianzisha rc wa tabora reaction ya Ali kamwe plus kufungwa imemtibua na kuamua kutumia mamlaka yake ya urc

Tangu lini kiongozi mkubwa wa serikali anazungumzia ushabiki mpaka kusababisha kuanza kutupiana vijembe na klabu ya Mpira?

Kama wewe ni mlezi na ni kiongozi mkuu kaa kimya toa ahadi kimyakimya

Hatutaki siasa katika michezo yetu.

Umasikini mmetupa nyie,tumehamia katika Mpira kujifariji Napo mnatuingilia tukimbilie wapi Sasa

Au twende Burundi???
 
Mkuu wa mkoa kazidiwa mapigo ya kishabiki kaamua kuleta za kuleta. Wakuu wa mikoa wakome kujiingiza kwenye ushabiki watalishwa za uso halafu iwe taabu
 
Kwani ww ni kiongozi mpk uone izo kauli?
Utani bila mipaka sio utani sw.
KAZI ni kipimo cha utu
 
Back
Top Bottom