Ndoa yangu ina miaka mingi kidogo sio muda tutafikisha 20 yrs, kumeshakuwepo na ups and down, hata vikombe kwenye kabati kuna wakati vinakwazana but all in all, siwezi kuishi bila ndoa, na siwezi kuishi bila huyu mwanamke. ana mapungufu mengi, ila mazuri mengi zaidi, mimi pia nina mapungufu mengi na mazuri mengi zaidi bila shaka. imefika kipindi tukasomana,tukajuana limits na kujuana namna ya kuishi hadi tumekuwa mwili mmoja. haya ni maisha ya dunia. Mungu anaelekeza wanaume tuwapende wake zetu, na wake zetu zaidi ya kutupenda wanatakiwa watutii. sisi hatutakiwi kuwatii wake zetu kwasababu sisi ni kichwa, tuwapende, ukimpenda mkeo, hautamcheat, hautampiga, hautamwangalia kwa jicho baya, utamvumilia na kuchukuliana na mapungufu yake, utamfichia aibu yake, utamjali na kumtunza kama mtoto wako. naamni jukumu la kuwapenda tulilipewa wanaume ni kubwa zaidi ya lile la wao kututii (though wanatakiwa kututii yale yaliyo mapenzi ya Mungu).
Waebrania 13:4 INASEMA, Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waacherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu.
Nakuasa, ukitaka ufanikiwe katika ndoa yako, HESHIMU NDOA YAKO, linda ndoa yako, usiruhusu uzinzi au uasherati kwasababu uasherati na uzinzi Mungu atakuhukumia adhabu hakika. Pia anaposema malazi yawe safi, hakikisha matendo yenu mnayafanya kwa usafi, achana na matendo ya ndoa machafu, kuna watu wanaangalia kwanga porn ndio waendelee na tendo, kuna watu wanaingiliana kinyume na maumbile, kuna watu wanafanya uzinzi hadi mashindano kwenye ndoa, jueni ya kwamba, malazi yenu lazima yawe safi na kimbia uzinzi na uasherani kuliko chochote, la sivyo Mungu atakuhukumia adhabu. huu ndio ushauri mkubwa ambao naweza kukushauri.
Mkeo hata kama ana mapungufu, ni wako, mtetee, mpambanie, mfichie aibu na madhaifu, kwasababu na wewe sio mkamilifu. pia, jitahidi sana kusamehe ili na wewe usamehewe, ukimkosea, be fair, mwambie hapo nimekukosea nisamehe, na yeye akikukosea, awe fair akuombe radhi, communication is the most important aspect kwenye ndoa, mambo ya kununiana nuniana hayajengi ndoa, ukiwa na dukuduku mwite, mkae mweleze mjadili, pengine ana hoja au pengine wewe una hoja, mnaweza kununiana karibia siku tatu kama watoto wadogo na mkija kukaa na kupeana hoja kwanini imekuwa hivyo, mnajikuta siku ile ile ya kwanza mngepeana opportunity kila mtu kuyamaliza kwa mazungumzo mngeshayamaliza dakika ileile.
ukiishi na mwanamke, usiishi kama yeye ni malaika, ana mapungufu mengi, na anakutegemea, akikosea usifoke, ongea, jadili, samehe, rekebisha kwa maneno sio kwa vitendo, ubabe kwetu sisi wanaume haujawahi kusolve chochote, zaidi sana huwa unaziba midomo ya wanawake wasiwe wazi hata kwa mambo ambayo ungeyajua juu yao. maisha ni rahisi sana hamna haja ya kucomplicate, alimradi tu asikuendeshe as if yeye ndio baba wa familia, na hapo napo panahitaji hekima tu na kuweka mipaka, wala huhitaji ngumi, matusi, visasi, visirani n.k. Mungu awasaidie.