Elections 2010 Nimeshinda Kura za maoni Kuipepersuha Bendera ya CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Mimi naanzisha petition kwa kiranga kuingia kwenye siasa ili aweke mfano wa nini wanasiasa wanatakiwa kufanya.

Hahahahaaa kuandika na kupiga kelele kwenye mtandao si sawa na kufanya kweli kwenye real world.....wengi wetu humu ni ma armchair strategists, pundits, critics, quarterbacks, n.k tunaoishi kwenye ivory towers...
 
Hahahahaaa kuandika na kupiga kelele kwenye mtandao si sawa na kufanya kweli kwenye real world.....wengi wetu humu ni ma armchair strategists, pundits, critics, quarterbacks, n.k tunaoishi kwenye ivory towers...

Nataka Kiranga aweke his reputation online hapa. Aingie kwenye ulingo ili aoneshe watanzania wote namna ya kuendesha siasa.

I have my predicitions:

1. Hana ubavu wa kufanya hivi
2. Akijaribu, ataingia CCM (hana ubavu wa kuwa mpinzani)
3. Akiingia CCM, atakimbilia kwenye viti maalum (anaweza kusingizia kuwa yeye ni mlemavu) maana hana uwezo wa kugombania jimbo
 

Nimelieleza hili hapo juu kwamba CHADEMA kwa kutuletea mgombea dhaifu inajionyesha na yenyewe dhaifu.

Kuna aina mnne kuu za watu.

1. Hawajui, na hawajui kwamba hawajui - hawa hatari sana, wanaweza hata kugombea ubunge au urais bila ya kufikiri mara mbili. Hawataki hata ushauri kwa sababu hawajui kama wanahitaji ushauri in the first place

2. Hawajui, lakini wanajua kwamba hawajui, hawa wanahitaji kuelimishwa zaidi. Na kwa sababu wanajua kwamba hawajui, ni vigumu kutaka kujitwika mizigo wasiyoiweza. Hawa ingawa hawajui, nawaheshimu kwa sababu wanajua kwamba hawajui, na kujua kwamba hujui ndiyo mwanzo wa kujua.

3. Wanajua, lakini hawajui kama wanajua- sleeping giants, only waiting for a tap on the shoulder to arise like a Phoenix from the ashes.

4. Wanajua, na wanajua kwamba wanajua. Hawa inabidi waelekeze na kuchangia sana.

Sasa huyu dada yupo katika kundi la kwanza, hajui halafu hajui kwamba hajui. In fact, hajui hata kama kujua kunatakiwa, kwa mawazo yake "ubunge si kitu cha ajabu, na mtu yeyote anaweza kuwa mbunge" really ?Kwa ufanisi ule ule ?

Swali lako linaibua swala jingine, je mtu ambaye hajui na hajui kwamba hajui anafaa kulaumiwa ? Hasha, kumlaumu ni kama kumuonea. Ni kama wanavyosema "blaming the victim". Huyu dada ni victim wa mfumo mbaya wa elimu wa Tanzania, kwa hiyo kumlaumu from the onset si sawa.

Lakini tatizo linakuja, mtu ambaye hajui kwamba hajui akielekezwa, huwezi kufanya hivyo utakuwa unajimaliza mwenyewe, na yeye akaleta kiburi, u prima donna, majibu ya kashfa, usiri usiohitajika, ana akawa anazidi kuji expose alivyo hamnazo, je tumuachie tu kwamba huyu hajui kwamba hajui? Hata baada ya kumueleza? Hasha, kuna sehemu personal responsibility inabidi kuanza ku kick in.

Ndiyo hapa tulipo sasa, huyu dada angekuwa responsive angalau tungekuwa na matumaini kwamba anaweza kujifunza mengi haraka - ingawa hii kazi inataka mtu anayeweza kufanya vitu from day one- tungekubali.

Lakini ukimkosoa anakwambia "nenda kabebe box". Ukimwambia huna intitiative na hata kujitaja hapa umejitaja kwa pressure za nje yako, anasema sikujitaja kwa pressure za nje yako, kuna mtu (hata jina la JF hatutajii, anaendeleza usiri kwa hiyo hatuwezi ku verify chochote kama huyu mtu ni hadithi tu au ni kweli) kaja kaajenga hoja kwenye PM ndiye aliyemshawishi, regardless kama unasubiri ushawishiwe kutaja jina lako mwenyewe huko bungeni utaweza kutoa muswada wa maana wewe kweli?

Kwa hiyo chama kina lawama kwa kum nominate, yeye mwenyewe hata kama hakujua kwamba hajui, anapoambiwa anatakiwa kuwa na akili ya kujua kwamba hiki ni kitu kipya.

Unakonipeleka zaidi ya hapo ni kubaya, maana wengine wanawez kusema hapaswi kulaumiwa kwa sababu hayuko capable kujua kabisa hata baada ya kuambiwa asiyoyajua, yaani ni kama kumpigia mbuzi gita na kumtegemea acheze dansi complicatd. Ukitilia manani kuna watu walio na religiously partisan views wanaomtia ujinga ajione anajua.

Inawezekana ndiyo caliber ya wabunge wetuu watarajiwa hiyo, it is not an irrational stretch at all.
 

Ungemfuatilia Kiranga ungefahamu kwamba hana hata dini, wachilia mbali upuuzi wa kujiingiza katika siasa za elected office ambao unataka mtu awe lower than some forms of protozoan life forms ili kujishusha hivyo.

Tatizo watu wanafikiri mchango pekee utatoka katika elected office, top down thinking. Bila grassroots organizations.

Tatizo Solomon anakuja na fikra zile zile nilizozitaja hapo juu za Us vs. Them, mtu akitoa criticism kwa CHADEMA ni CCM.

Wengine tunatoa criticism kwa upinzani kwa sababu tunataka upinzani imara.

Kuongelea walemavu katika hiyo context, hususan katika thread ambayo muhusika mkuu ni mlemavu, ni matusi kwa walemavu.

Kwa hiyo wewe unaona ulemavu ni kichaka cha kutafutia mteremko siyo ? Unajionyesha unavyofikiri mwenyewe.

Wanasiasa mostly ni parasites, mimi sina mpango wa kutafuta elected office.I have an actual trade (as opposed to politricks and gabfesting for a living) that is sustaining me very well, thank you very much.

Kama unaamini huyu dada ana uwezo wa kushinda put your money where your mouth is.

Weka bet hapa, mimi nasema hawezi kushinda, not by this style.
 
Mimi naanzisha petition kwa kiranga kuingia kwenye siasa ili aweke mfano wa nini wanasiasa wanatakiwa kufanya.
Napinga dhana ya kumbembeleza mtu aingie kwenye siasa au uongozi kama CHADEMA walivyofanya na Dr. Slaa. Subiri mwenyewe atamke, aape, kuwa ana moyo na nia ya dhati ya kuingia siasa.

... mimi ni atheist siamini mungu.Wanaweza si tu kukataa kunipigia kura, bali kunipiga mawe pia.Tanzania is not ready for my type right now. Maybe some future time, well beyond my lifespan.
Mwiru?
 
Kiranga sasa unagombea wapi mkuu?

Na katika hayo makundi manne ya watu, wewe uko wapi?

Huhitaji kugombea ili kujua kwamba mgombea ni dhaifu, mimi nina allergy na elected office.Kitu cha kwanza nitakachowaambia wapiga kura ni kwamba mimi ni atheist siamini mungu.Wanaweza si tu kukataa kunipigia kura, bali kunipiga mawe pia.Tanzania is not ready for my type right now. Maybe some future time, well beyond my lifespan.

Hilo swala la mimi ni type gani kati ya hizo nne si langu kulijibu, labda wewe na wana JF wengine mnaweza kusema, mimi nitakuwa biased katika jibu lolote nitakalotoa kuhusu hilo.
 

Kama huamini katika siasa, unachoongelea hapa kwenye siasa unakiamini au ni maneno tu?

Tatizo Solomon anakuja na fikra zile zile nilizozitaja hapo juu za Us vs. Them, mtu akitoa criticism kwa CHADEMA ni CCM.

Wengine tunatoa criticism kwa upinzani kwa sababu tunataka upinzani imara.

Wewe ingia uoneshe mfano maana so far kila wanachofanya wenzako hakifai

Kuongelea walemavu katika hiyo context, hususan katika thread ambayo muhusika mkuu ni mlemavu, ni matusi kwa walemavu.

Kwa hiyo wewe unaona ulemavu ni kichaka cha kutafutia mteremko siyo ? Unajionyesha unavyofikiri mwenyewe.

Nimeonesha vile thinking yako ipo, wewe huamini (au unaamini too much kwenye anything or nothing) sasa katika hili una kigezo kingine cha kugombea zaidi ya kigezo cha ulemavu.

Wanasiasa mostly ni parasites, mimi sina mpango wa kutafuta elected office.I have an actual trade (as opposed to politricks and gabfesting for a living) that is sustaining me very well, thank you very much.

Kama hujagundua bado, uko kwenye wrong trade (as far as unajionesha hapa). Ungeendeleza trade yako vyema kuliko kubaka siasa ambayo sio tu kwamba unasema huiamin, bali pia unasema kuwa huipendi.

Huu ndio ninaita unafiki wa first class

Kama unaamini huyu dada ana uwezo wa kushinda put your money where your mouth is.

Weka bet hapa, mimi nasema hawezi kushinda, not by this style.

Mimi nataka wewe uweke bet kama utaingia kwenye siasa, na uweke ni kiasi gani utaweka kuonesha kuwa utashinda.

Huo mwingine ni unafiki tu bets za kitoto ... mambo ya kupinga tukiwa chekechea, watu mnapinga kama mwalimu monica atawakiss (what a waste of time)

Weka reputation yako na knowledge yako kwenye line hapa JF
 
aa kumbe wabeba box hawatakiwi kuchangia siasa za tanzania? (post iloandika hivyo sikuiona kwa kweli, au labda imeshaondolewa)

siasa bngo bado zina parefu pa kwenda...............ukikosoa utaambiwa una wivu, ukinyamaza kimya utaambiwa diaspora haina mchango kwa tanzania.
 
Ukosoaji wa Regia sasa umevuka mipaka. Mimi pia niliona alikosea pale mwanzoni aliposema asiulizwe anagombea jimbo gani na mengineyo yahusuyo ugombeaji wake. Angeweza kabisa kusema kitu kama 'nitarudi baadae kutoa maelezo zaidi kuhusu ugombeaji wangu na kujibu maswali yenu'kama mtakuwa nayo '. Angesema kitu kama hicho sidhani kama tungefika hapa tulipofika sasa. Sijui ni nani alimshauri aseme hivyo au inawezekana hakuomba ushauri wa yeyote wa jinsi gani aweke tangazo lake hapa. Alikosea kusema kusema asiulizwe. Angetupiga tarehe tu na kutuambia atarudi baadae.

Lakini licha ya kukosea huko sasa amejirudi na kuja kuweka wazi utambulisho wake na jimbo analogombea. Hapo mimi nilimpa alama ya 'vyema' na ugomvi wangu ukaisha. Ila yaelekea kuna wengine ambao bado wanalia nae. Wanakosoa kila neno, kila sentensi, kila aya, na kila wawezalo kukosoa tena kwa lugha kali zisizo za kiungwana. Hata kama ni 'constructive criticism', sidhani kama mlengwa atachukulia hivyo. Kuna namna ya kumkosoa mtu kwa kumjenga. Maneno yana maana sana. Lengo la ukosoaji linaweza kuwa jema kabisa lakini maneno unayoyatumia na jinsi unavyoyapanga yanaweza kuharibu kabisa lengo ulilokusudia. Kuna msemo Kiingereza usemao 'It's not what you say but how you say it'. Huu msemo unaweza ukawa ni cliche lakini unabeba maana nzito sana katika mawasiliano yetu ya kila siku. Kwa hiyo ni vizuri pia kuzingatia namna na jinsi tunavyosema yale tunayosema hasa kama lengo letu ni kujenga na kusaidia.

Sasa kwa vile kampeni ndio zimeshaanza (ingawa hazijaanza rasmi), tumpe muda huyu dada yetu. Kuanza kumhukumu kuwa hata kushinda hataweza si vizuri. Akija kushinda je tutafanyaje? Tutayala maneno yetu wenyewe na kumwomba radhi ama? Tumuunge mkono (ingawa si lazima kufanya hivyo, ila binafsi namuunga mkono), tumtie moyo, tumkosoe kwa lugha za kiungwana zinazojenga na si zinazomfanya mtu amenyuke (react) kwa hisia na kujibu kwa aina (in kind).

Mwisho, usivunjike moyo Regia. Haya yote yanakuja na mazingira yake (they come/go with the territory). Yaliyo mema na mazuri yachukue na yafanyie kazi. Ya kijinga na kipuuzi yaache hivyo hivyo kama yalivyo. Usiache hizi kelele zikufanye upoteze lengo (lose focus). Keep your eyes on the prize and I am with you all the way to Dodoma.
 

Huyu hata haelewi tofauti ya principles na siasa, tofauti ya "public service" na "politics" huy haielewi.

Mimi naamini katika "public service" wala si katika siasa, na ili kufanya public service huhitaji kujikita katika siasa za uchaguzi.
 

My dude, wengine we can do so much with diplomacy, tunaita vitu majina tunayoona yanaelezea vizuri, sio yatakayopokelewa vizuri. Ndio maana tulikua mapema kwamba kupakana mafuta kwa migongo ya chupa kunakotakiwa katika siasa hatukuwezi.

I made my case, I said my peace in this thread. Naona kuna a fundamental difference katika mitazamo. Sitaongeza neno - indeed zaidi ya kujibizana na watu hapa na pale points kubwa nishazitoa- katika mjadala huu mpaka baada ya uchaguzi.
 


NN Asante kwa kumtia nguvu Regia.

Nimevutika sana na maneno haya ya busara ambayo nina hakika ndugu yetu Regia akiyasoma yatampa nguvu kubwa na msukumo kuendelea mbele badala ya kuvunjika moyo.

Regia,
Jua kuna watu wengi wanaokuunga mkono kwa ushujaa uliouonyesha au uthubutu wa kuingia kwenye medani ya siasa na kutumia haki yako ya kikatiba ya kugoombea nafasi za uongozi.Ukiangalia ni wangapi wako kwenye nafasi kama yako ( hata kama hutapata ubunge bado uko juu!) ni wachache. DONT GIVE UP SISTAH!
 

Acha zako hizo wewe Camelion, hivi huu utoto utaacha lini? grow up ujinga huu
 

Asante sana Mutu.Tuko pamoja..
 


kumbe umemuona huyu kibaraka!
 
Nimetoka Jangwani kwa kweli mambo yalikuwa ni mazuri sana..
 
Nadhani Regia ameweza kuhimilia ukosoaji wa humu atakuwa ni kiongozi mzuri tu maana wengine wangekuja kwa hasira. Amepitia Tanuru la Kiranga.. and survived.. she will be able to handle anything coming her way. Keep it up na usije ukajikuta unamshyrose mtu! Unless it is absolutely necessary! You go girl! Got my support!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…