Elections 2010 Nimeshinda Kura za maoni Kuipepersuha Bendera ya CHADEMA

Elections 2010 Nimeshinda Kura za maoni Kuipepersuha Bendera ya CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Kwa wale ambao hatufahamu wasifu wa GS jee utatusaidiaje? I will donate kwa mtu yoyote wa chama chochote ambaye ni mjumbe wa mabadiliko. Tunaomba CV ili na sisi tuchangie. Sambamba na CV pia nina maswali yangu mawili matatu naomba unitanabaishie.

a) How will Kilombero benefit from you?
b) Jee ni jambo gani ambalo limekuwa chachu ya maamuzi yako?
c) Jee ni sehemu gani zinaitaji madaliko in Kilombero and why?
d) WHY YOU?? Kwa nini Watanzania tukuamini wewe? Why?


Thanks.
 
Mtu akishaanza kujikojolea kwenye serawili zaidi ya mara moja wkati anawahutubia mkutanoni huhitaji hata kujua sana historia yake ili kujua kwamba hafai.

Historia ni muhimu, lakini anachoweza kufanya sasa hivi ni muhimu zaidi. Hawezi mjadala, si umemuona kakimbia anajua akija hapa atasulubiwa.

Kwanza anatakiwa kuomba msamaha kwa jumuiya ya wabeba box kwa kuwakashifu.

Huyu dada amekabili hoja vizuri sana. Kikwete alidondoka jukwaani hukumshambulia kama huyu mgombea wa ubunge. Halafu nani aliwahi kujikolea jukwaani? Mkuu Kiranga naona umeamua kuwa na mtazamo hasi wa namna alivyojibu hoja. Mtazamo wako hasi haumaanishi kuwa wengine wanaona kama unavyoona wewe. Kwa hiyo unaona hasi kwenye maelezo yake, wengine wengi wanaona chanya namna alivyojibu hoja.
 
Kwa wale ambao hatufahamu wasifu wa GS jee utatusaidiaje? I will donate kwa mtu yoyote wa chama chochote ambaye ni mjumbe wa mabadiliko. Tunaomba CV ili na sisi tuchangie. Sambamba na CV pia nina maswali yangu mawili matatu naomba unitanabaishie.

a) How will Kilombero benefit from you?
b) Jee ni jambo gani ambalo limekuwa chachu ya maamuzi yako?
c) Jee ni sehemu gani zinaitaji madaliko in Kilombero and why?
d) WHY YOU?? Kwa nini Watanzania tukuamini wewe? Why?


Thanks.

Maswali yako ni mazuri sana lakini namshauri Mbunge huyu asiyajibu mpaka NEC watangaze kwamba kampeni zimeanza.
 
Wakuu,

Jana tulikuwa na mchakato wa kura za maoni jimboni kwetu. Tulikuwa wagombea wawili katika chama chetu. Nimefanikiwa kushinda kura za maoni kwa kishindo na kumuangausha mpinzani wangu, hivyo kuipeperusha bendera ya CHADEMA katika jimbo hili.

Nimeandika historia kwa kuwa kijana wa kwanza kugombea kwenye jimbo hili tangu kurudi kwa mfumo wa vyama vingi kwa vyama vyote vilivyowahi kusimamisha wagombea ubunge kwenye jimbo hili. Ni mtaji kwangu..

Tuko pamoja...Hakuna kulala mpaka kieleweke.

Tafadhali naomba msiniulize nagombea jimbo gani. Ni jimbo moja la Mkoani, Wilaya yenye jimbo moja.. Zaidi ya hapo usiniulize.

Alunta continua

Kila la heri mama. Nakutakia mafanikio tele katika kampeni zako. Nakuomba katika kampeni zako umsaidie pia kumfanyia kampeni Shujaa wa Watanzania Dr Slaa. Kwenye Kampeni zako usisahau kuyasema maovu yote ya CCM yakiwemo ufisadi, nchi kukosa maendeleo, Wafanyakazi kuwa na vipato ambavyo haviendani na gharama za maisha, Utajiri mkubwa tuliojaliwa na Mungu (rasilimali zetu) kuwanufaisha wageni badala ya Watanzania. Rushwa iliyokithiri kila kona ya nchi yetu, mashule na mahospitali yetu kutokuwa na madawati, madarasa, walimu, vitanda, madawa na vifaa muhimu.

Na pia usisahau kuziweka wazi sera za CHADEMA na nini mnategemea kukifanya katika miaka mitano ya kwanza ya kuwa madarakani. Kila la heri. YES WE CAN!

Alutta Continua


 
Kila La Kheri Regia...Ni wazi kwamba azma yako ya kutumikia watu wa Kilombero itafanikiwa,kuwa muangalifu katika kujibu maswali na kuleta Mada hapa.Si kila aliyepo hapa anapenda/ Azma yako ya kutaka kuwatumikia watu wa Kilombero kwa wadhifa wa Ubunge.Kumbuka upo hapa kwa jina lako kamili,inabidi uwe wewe!Jibu maswali na jieleze bila uoga,ignore maswali ya upuuzi au yenye lengo la kukudhalilisha.Tupo pamoja katika "Harakati hizi za kuleta Mabadiliko ya kweli".Stay safe!
 
kitu ambacho nakushauri dada yangu uwe tayari kwa maswali ya below the belt
maswali yakiwa below the belt yajibu kwa ukarimu wote
 
kitu ambacho nakushauri dada yangu uwe tayari kwa maswali ya below the belt
maswali yakiwa below the belt yajibu kwa ukarimu wote

Hayo ndiyo maswali gani? naomba utafsiri kwa lugha ya Taifa sikukuelewa.
 
Ukosoaji wa Regia sasa umevuka mipaka. Mimi pia niliona alikosea pale mwanzoni aliposema asiulizwe anagombea jimbo gani na mengineyo yahusuyo ugombeaji wake. Angeweza kabisa kusema kitu kama 'nitarudi baadae kutoa maelezo zaidi kuhusu ugombeaji wangu na kujibu maswali yenu'kama mtakuwa nayo '. Angesema kitu kama hicho sidhani kama tungefika hapa tulipofika sasa. Sijui ni nani alimshauri aseme hivyo au inawezekana hakuomba ushauri wa yeyote wa jinsi gani aweke tangazo lake hapa. Alikosea kusema kusema asiulizwe. Angetupiga tarehe tu na kutuambia atarudi baadae.

Lakini licha ya kukosea huko sasa amejirudi na kuja kuweka wazi utambulisho wake na jimbo analogombea. Hapo mimi nilimpa alama ya 'vyema' na ugomvi wangu ukaisha. Ila yaelekea kuna wengine ambao bado wanalia nae. Wanakosoa kila neno, kila sentensi, kila aya, na kila wawezalo kukosoa tena kwa lugha kali zisizo za kiungwana. Hata kama ni 'constructive criticism', sidhani kama mlengwa atachukulia hivyo. Kuna namna ya kumkosoa mtu kwa kumjenga. Maneno yana maana sana. Lengo la ukosoaji linaweza kuwa jema kabisa lakini maneno unayoyatumia na jinsi unavyoyapanga yanaweza kuharibu kabisa lengo ulilokusudia. Kuna msemo Kiingereza usemao 'It's not what you say but how you say it'. Huu msemo unaweza ukawa ni cliche lakini unabeba maana nzito sana katika mawasiliano yetu ya kila siku. Kwa hiyo ni vizuri pia kuzingatia namna na jinsi tunavyosema yale tunayosema hasa kama lengo letu ni kujenga na kusaidia.

Sasa kwa vile kampeni ndio zimeshaanza (ingawa hazijaanza rasmi), tumpe muda huyu dada yetu. Kuanza kumhukumu kuwa hata kushinda hataweza si vizuri. Akija kushinda je tutafanyaje? Tutayala maneno yetu wenyewe na kumwomba radhi ama? Tumuunge mkono (ingawa si lazima kufanya hivyo, ila binafsi namuunga mkono), tumtie moyo, tumkosoe kwa lugha za kiungwana zinazojenga na si zinazomfanya mtu amenyuke (react) kwa hisia na kujibu kwa aina (in kind).

Mwisho, usivunjike moyo Regia. Haya yote yanakuja na mazingira yake (they come/go with the territory). Yaliyo mema na mazuri yachukue na yafanyie kazi. Ya kijinga na kipuuzi yaache hivyo hivyo kama yalivyo. Usiache hizi kelele zikufanye upoteze lengo (lose focus). Keep your eyes on the prize and I am with you all the way to Dodoma.

Kweli itakuwa imekugusa kwani sijawahi kuona umeandika post ndefu kiasi hiki but on top of that it is well said.
 
Hongera sana dada. kampeini zikianza rasmi, nitumie PM nikuletee mchango wa kusaidia kampeini. Mimi hutumia westernunion na monyegram tu, kwa hiyo usinitumie namba ya benki kwa vile siwezi kutuma TT
 
Napinga dhana ya kumbembeleza mtu aingie kwenye siasa au uongozi kama CHADEMA walivyofanya na Dr. Slaa. Subiri mwenyewe atamke, aape, kuwa ana moyo na nia ya dhati ya kuingia siasa.


Kiranga habembelezwi hapa, anaambiwa tu kuweka his reputation na money where his mouth is ... kwenye siasa za bongo
 
Nadhani Regia ameweza kuhimilia ukosoaji wa humu atakuwa ni kiongozi mzuri tu maana wengine wangekuja kwa hasira. Amepitia Tanuru la Kiranga.. and survived.. she will be able to handle anything coming her way. Keep it up na usije ukajikuta unamshyrose mtu! Unless it is absolutely necessary! You go girl! Got my support!

Huo wakati ambao ni absolute necessary kumshyrose mtu ndo upi?
Hebu tusaidie hapo
 
Huyu hata haelewi tofauti ya principles na siasa, tofauti ya "public service" na "politics" huy haielewi.

Mimi naamini katika "public service" wala si katika siasa, na ili kufanya public service huhitaji kujikita katika siasa za uchaguzi.


Wewe ndiye unajichanganya kabisaaa, mara useme hutaki kabisa siasa (politics), kisha unasema kuwa itakuwa beyond your life span, na kisha unataka kuwa kwenye public service wakati huo huo hutaki kufanya siasa za uchaguzi (kabla na baada ya hapo ukitoa ushauri wa namna ya kufanya siasa za uchaguzi) na wakati huo huo , hata nimesahau nilikuwa wapi kwenye kufuatilia hata unachokiongelea hapa ni nini hasa.

Ohh, nimekumbuka, unasema kwa hakika kuwa huyu dada kakosea, kachemsha, ni dhaifu, hafai kabisa kuwa kwenye siasa, na kila aina ya uozo unaoweza kuutoa. Kwa kushirikiana na yule mwanachama wa chama cha mafisadi hapo juu, mmeanza kuipondea chadema kuwa ni extension ya uozo wa huyu dada.... sijui kama bado unaongelea public service au siasa (za uchaguzi).

Unachotakiwa kufanya hapa, ni kuonesha ukomavu, umakini, na uwezo wako wa kisiasa (ambao ni mara mia ya dada Regia kwa maoni yako) kwa kuingia kwenye siasa (just in case umetoka maana inaonekana wewe na siasa ni damu damu) ili kuonesha namna ya kurun campaign na kupanga strategy bora kabisa za kugombea majimbo yote ya Tanzania.

Nakuhakikishia kuwa ukiingia kwenye chama cha upinzani, bado sitaweka bet kuwa utashinda (achilia mbali kukuuliza wewe ujiwekee bet ya kushinda hiyo nafasi).
 
Acha zako hizo wewe Camelion, hivi huu utoto utaacha lini? grow up ujinga huu

Ona huyu naye, leo mmechapa viboko wangapi ambao hawajavaa kininja? mmekata wangapi mikono kwa wizi wa kuku huko somalia (wakati mkiachia Kikwete na wenzake wakiitia nchi kwenye umasikini)?
 
Wakuu,

Jana tulikuwa na mchakato wa kura za maoni jimboni kwetu. Tulikuwa wagombea wawili katika chama chetu. Nimefanikiwa kushinda kura za maoni kwa kishindo na kumuangausha mpinzani wangu, hivyo kuipeperusha bendera ya CHADEMA katika jimbo hili.

Nimeandika historia kwa kuwa kijana wa kwanza kugombea kwenye jimbo hili tangu kurudi kwa mfumo wa vyama vingi kwa vyama vyote vilivyowahi kusimamisha wagombea ubunge kwenye jimbo hili. Ni mtaji kwangu..

Tuko pamoja...Hakuna kulala mpaka kieleweke.

Tafadhali naomba msiniulize nagombea jimbo gani. Ni jimbo moja la Mkoani, Wilaya yenye jimbo moja.. Zaidi ya hapo usiniulize.

Alunta continua
Hongera sana kwa kuingia ktk mchakato wa kuomba ridhaa ya wana -kilombero.Nakutakia Kila La kheri!Mema ya kwenye hili jamvi yachukue na mabaya tuwachie,Usisoneke kwa vigongo vya baadhi yetu bali hii ikupe picha kamili ya ni aina gani ya watu utakutana nao (nikimaanisha utakutana na watu wa aina mbalimbali huko viwanja kama ilivyo hapa jamvini.Kila la kheri !
 
Hayo ndiyo maswali gani? naomba utafsiri kwa lugha ya Taifa sikukuelewa.
ngumi nim mchezo ambao unapata point kwa kumpiga mwenzio juu, ukimpiga chini sehemu za mapumbu ni foul play.

maswali ya below the belt ni maswali ni maswali ambayo hayahusiani na hile hoja na yanadhumuni la kukuzalilisha. wewe ni mfanyabiashara wa k... nk
 
Nadhani Regia ameweza kuhimilia ukosoaji wa humu atakuwa ni kiongozi mzuri tu maana wengine wangekuja kwa hasira. Amepitia Tanuru la Kiranga.. and survived.. she will be able to handle anything coming her way. Keep it up na usije ukajikuta unamshyrose mtu! Unless it is absolutely necessary! You go girl! Got my support!

Asante sana Mkuu....
 
GS huyu dada Suzan Kiwanga anagombea wapi? Ama ndiye uliyeshinda kwenye kura za maoni?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom