Elections 2010 Nimeshinda Kura za maoni Kuipepersuha Bendera ya CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Kwa wale ambao hatufahamu wasifu wa GS jee utatusaidiaje? I will donate kwa mtu yoyote wa chama chochote ambaye ni mjumbe wa mabadiliko. Tunaomba CV ili na sisi tuchangie. Sambamba na CV pia nina maswali yangu mawili matatu naomba unitanabaishie.

a) How will Kilombero benefit from you?
b) Jee ni jambo gani ambalo limekuwa chachu ya maamuzi yako?
c) Jee ni sehemu gani zinaitaji madaliko in Kilombero and why?
d) WHY YOU?? Kwa nini Watanzania tukuamini wewe? Why?


Thanks.
 

Huyu dada amekabili hoja vizuri sana. Kikwete alidondoka jukwaani hukumshambulia kama huyu mgombea wa ubunge. Halafu nani aliwahi kujikolea jukwaani? Mkuu Kiranga naona umeamua kuwa na mtazamo hasi wa namna alivyojibu hoja. Mtazamo wako hasi haumaanishi kuwa wengine wanaona kama unavyoona wewe. Kwa hiyo unaona hasi kwenye maelezo yake, wengine wengi wanaona chanya namna alivyojibu hoja.
 

Maswali yako ni mazuri sana lakini namshauri Mbunge huyu asiyajibu mpaka NEC watangaze kwamba kampeni zimeanza.
 

Kila la heri mama. Nakutakia mafanikio tele katika kampeni zako. Nakuomba katika kampeni zako umsaidie pia kumfanyia kampeni Shujaa wa Watanzania Dr Slaa. Kwenye Kampeni zako usisahau kuyasema maovu yote ya CCM yakiwemo ufisadi, nchi kukosa maendeleo, Wafanyakazi kuwa na vipato ambavyo haviendani na gharama za maisha, Utajiri mkubwa tuliojaliwa na Mungu (rasilimali zetu) kuwanufaisha wageni badala ya Watanzania. Rushwa iliyokithiri kila kona ya nchi yetu, mashule na mahospitali yetu kutokuwa na madawati, madarasa, walimu, vitanda, madawa na vifaa muhimu.

Na pia usisahau kuziweka wazi sera za CHADEMA na nini mnategemea kukifanya katika miaka mitano ya kwanza ya kuwa madarakani. Kila la heri. YES WE CAN!

Alutta Continua


 
Kila La Kheri Regia...Ni wazi kwamba azma yako ya kutumikia watu wa Kilombero itafanikiwa,kuwa muangalifu katika kujibu maswali na kuleta Mada hapa.Si kila aliyepo hapa anapenda/ Azma yako ya kutaka kuwatumikia watu wa Kilombero kwa wadhifa wa Ubunge.Kumbuka upo hapa kwa jina lako kamili,inabidi uwe wewe!Jibu maswali na jieleze bila uoga,ignore maswali ya upuuzi au yenye lengo la kukudhalilisha.Tupo pamoja katika "Harakati hizi za kuleta Mabadiliko ya kweli".Stay safe!
 
kitu ambacho nakushauri dada yangu uwe tayari kwa maswali ya below the belt
maswali yakiwa below the belt yajibu kwa ukarimu wote
 
kitu ambacho nakushauri dada yangu uwe tayari kwa maswali ya below the belt
maswali yakiwa below the belt yajibu kwa ukarimu wote

Hayo ndiyo maswali gani? naomba utafsiri kwa lugha ya Taifa sikukuelewa.
 

Kweli itakuwa imekugusa kwani sijawahi kuona umeandika post ndefu kiasi hiki but on top of that it is well said.
 
Hongera sana dada. kampeini zikianza rasmi, nitumie PM nikuletee mchango wa kusaidia kampeini. Mimi hutumia westernunion na monyegram tu, kwa hiyo usinitumie namba ya benki kwa vile siwezi kutuma TT
 
Napinga dhana ya kumbembeleza mtu aingie kwenye siasa au uongozi kama CHADEMA walivyofanya na Dr. Slaa. Subiri mwenyewe atamke, aape, kuwa ana moyo na nia ya dhati ya kuingia siasa.


Kiranga habembelezwi hapa, anaambiwa tu kuweka his reputation na money where his mouth is ... kwenye siasa za bongo
 

Huo wakati ambao ni absolute necessary kumshyrose mtu ndo upi?
Hebu tusaidie hapo
 
Huyu hata haelewi tofauti ya principles na siasa, tofauti ya "public service" na "politics" huy haielewi.

Mimi naamini katika "public service" wala si katika siasa, na ili kufanya public service huhitaji kujikita katika siasa za uchaguzi.


Wewe ndiye unajichanganya kabisaaa, mara useme hutaki kabisa siasa (politics), kisha unasema kuwa itakuwa beyond your life span, na kisha unataka kuwa kwenye public service wakati huo huo hutaki kufanya siasa za uchaguzi (kabla na baada ya hapo ukitoa ushauri wa namna ya kufanya siasa za uchaguzi) na wakati huo huo , hata nimesahau nilikuwa wapi kwenye kufuatilia hata unachokiongelea hapa ni nini hasa.

Ohh, nimekumbuka, unasema kwa hakika kuwa huyu dada kakosea, kachemsha, ni dhaifu, hafai kabisa kuwa kwenye siasa, na kila aina ya uozo unaoweza kuutoa. Kwa kushirikiana na yule mwanachama wa chama cha mafisadi hapo juu, mmeanza kuipondea chadema kuwa ni extension ya uozo wa huyu dada.... sijui kama bado unaongelea public service au siasa (za uchaguzi).

Unachotakiwa kufanya hapa, ni kuonesha ukomavu, umakini, na uwezo wako wa kisiasa (ambao ni mara mia ya dada Regia kwa maoni yako) kwa kuingia kwenye siasa (just in case umetoka maana inaonekana wewe na siasa ni damu damu) ili kuonesha namna ya kurun campaign na kupanga strategy bora kabisa za kugombea majimbo yote ya Tanzania.

Nakuhakikishia kuwa ukiingia kwenye chama cha upinzani, bado sitaweka bet kuwa utashinda (achilia mbali kukuuliza wewe ujiwekee bet ya kushinda hiyo nafasi).
 
Acha zako hizo wewe Camelion, hivi huu utoto utaacha lini? grow up ujinga huu

Ona huyu naye, leo mmechapa viboko wangapi ambao hawajavaa kininja? mmekata wangapi mikono kwa wizi wa kuku huko somalia (wakati mkiachia Kikwete na wenzake wakiitia nchi kwenye umasikini)?
 
Hongera sana kwa kuingia ktk mchakato wa kuomba ridhaa ya wana -kilombero.Nakutakia Kila La kheri!Mema ya kwenye hili jamvi yachukue na mabaya tuwachie,Usisoneke kwa vigongo vya baadhi yetu bali hii ikupe picha kamili ya ni aina gani ya watu utakutana nao (nikimaanisha utakutana na watu wa aina mbalimbali huko viwanja kama ilivyo hapa jamvini.Kila la kheri !
 
Hayo ndiyo maswali gani? naomba utafsiri kwa lugha ya Taifa sikukuelewa.
ngumi nim mchezo ambao unapata point kwa kumpiga mwenzio juu, ukimpiga chini sehemu za mapumbu ni foul play.

maswali ya below the belt ni maswali ni maswali ambayo hayahusiani na hile hoja na yanadhumuni la kukuzalilisha. wewe ni mfanyabiashara wa k... nk
 

Asante sana Mkuu....
 
GS huyu dada Suzan Kiwanga anagombea wapi? Ama ndiye uliyeshinda kwenye kura za maoni?
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…