DOKEZO Nimeshinda Sh 27M kwenye kubet, Kampuni inataka kunipa Sh 3M, Gaming Board hainisaidii

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Asee nimetetemeka sana...

Naogopa kukwambia huenda hiyo kampuni inashirikiana na watu wa Gaming Board kukutapeli...

Inasikitisha ila ukweli ni kwamba kwa nchi yetu ilipo una nafasi ndogo sana ya kupata pesa yako...

Nakushauri upige kelele kila sehemu, mitandao yote utapata msaada, watu wachafu huogopa kujulikana...

Kila lakheri mpambanaji.
 
Mtu kashinda yanaanza maigizo sijui labda mambo ya fixed game, angeshindwa angerudishiwa pesa sababu ni fixed game? Kamari ingepigwa marufuku tu hahaha.
Ndio fixed game hata ukilost,unarudishiwa pesa yako mkuu. Na kama wakisema waruhusu fixed game zilipwe hii biashara haitawezekana maana mtu atanunua game halafu atatia mpunga wa maana na bado ataisambaza watu maelfu wakitia mpunga wa maana tayari kampuni inafungwa ndio maana ikapitishwa sheria kuwa fixed game hazilipwi )Upangaji wa matokeo)
 
Uthibitisho huwa ni nini kuwa hii imekuwa fixed? Michezo husika ilifutwa matokeo? Acha kutetea utapeli. Janja janja hahaha
 
Hiyo milioni 3 ndiyo kodi ya serikali. Ila hili suala ndiyo linatufumbua macho kwamba zile zawadi zinazotangazwa siyo za kweli ni utapeli na ni njia ya kushawishi wengine zaidi. Kweli hatuna serikali wala mahakama. Hii CCM ni kwamba hakuna chama mbadala vinginevyo CCM ni sehemu ya wezi, majambazi, waonevu, wanyanyasaji wa raia wa nchi hii. Ni ngumu serikali hii kumsaidia mnyonge, huyo Makonda ndiyo jizi kubwa na tapeli anayeishi kwa njia za giza. Kwa serikali hii hii JF haiwezi kukusaidia hakuna anayejali na tatizo kubwa ni mkuu wa nchi.
Enzi la Magufuli kiongozi akipata habari km hizi haraka sana huyu jamaa angeshatafutwa mpaka na waziri kabla Rais hajaiona. Ila kizuri hakidumu! Kwa huyu mswahili wanyonge watateseka sana!
 
Ndio nilikuwa najiuliza hivi hakuna uwezekano wa kutafuta mwanasheria ili wazitapike hizo hela tena na fidia ya kuchelewesha huo mpunga ni mrefu sana sio wa kuuachia kizembe
 
Mkuu mbona kama story yako Kuna sehemu inakosekana! Why ushinde 27M kihalali then ukubali kupunguza ushindi wako? Kuna sehemu utakuwa umecheat ndio maana, either ulikuwa matokeo ya hizo team mapema au ulicheza na mfumo wakati server zikiwa down.

Kama Kuna udanganyifu umefanya chukua hiyo 3M.
 
Mbona kasema waliomba achukuwe fedha kidogo? Ingekuwa hivyo wangelipa? Atafute mwanasheria
 
wewe ndo ulikosea katika mashariti ya usajiri, tatizo la kufanya mambo kwa mazoea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…