DOKEZO Nimeshinda Sh 27M kwenye kubet, Kampuni inataka kunipa Sh 3M, Gaming Board hainisaidii

DOKEZO Nimeshinda Sh 27M kwenye kubet, Kampuni inataka kunipa Sh 3M, Gaming Board hainisaidii

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mwenzako anajadili kwa mantiki wewe unajadili kihisia. Ungekuwa unasoma terms and conditions za hayo makampuni ya kubeti usingeuliza haya maswali.

Siku nyingine bashiri fixed match, shinda alafu kosa hela uende mahakamani uone kama utapewa.
Huwezi tumia mihemko kisha umzidi anayetumia logic, common sense na maarifa.
Hata kama sijui kubeti na sijui terms and condition the fact kwamba tayari kampuni ilikuwa tayari kutoa fedha kidogo na si yote tayari suala la uhalali wa betting si hoja, hoja ni kiasi. Utapeli haufai usitee, unless useme kuna sehemu mleta mada ni muongo kwa kusema ukweli unaoufahamu wewe.
 
Mkuu mbona kama story yako Kuna sehemu inakosekana! Why ushinde 27M kihalali then ukubali kupunguza ushindi wako? Kuna sehemu utakuwa umecheat ndio maana, either ulikuwa matokeo ya hizo team mapema au ulicheza na mfumo wakati server zikiwa down.

Kama Kuna udanganyifu umefanya chukua hiyo 3M.
Kama alikuwa na matokeo hawezi kulipwa
 
Mbona kasema waliomba achukuwe fedha kidogo? Ingekuwa hivyo wangelipa? Atafute mwanasheria
Hapa tumeskiliza upande mmoja. Pigabet watu wanapiga hadi milion 600 hapo the grand casino na wanalipwa waje washinde kulipa milion 27? kwanza kwa sheria za kampuni za betting hawawezi kuruhusu wewe kuweka mkeka wa kiwango ambacho hawawezi kukilipa. Trust me ku sehem kuna shida jamaa aweke wazi
 
Mi ndo sitaki kabisa kusikia mambo ya jackpot, maana hiyo pesa wanayotangazwa nayo washindi hupati yote.

Kuna jamaa naemjua alishinda jackpot ya sportpesa million 200+ walienda kumuweka hotel serena for 5 days wana bargain nae tu, mwisho wakafikia compromise jamaa hakusema exactly walimpa kiasi gani ila alikubali kufanya tangazo la hundi ya milion 200+, in return wakampa gari yenye thamani ya milion 30 na undisclosed amount of money..

Kiufupi hajafanya lolote la maana mpka sasa mana maisha yake ni yale yale tunayoyajua ila still gari anayo.
Hela ya betting ufanye la maana? Labda watu wakushika na uache kubeti. Ukishinda milion 300 leo ndani ya miezi kadhaa umesharudisha pesa yao 🤣 ukidhani utashinda tena kwahiyo huyo jamaa yako utamlaumu bure
 
Hiyo milioni 3 ndiyo kodi ya serikali. Ila hili suala ndiyo linatufumbua macho kwamba zile zawadi zinazotangazwa siyo za kweli ni utapeli na ni njia ya kushawishi wengine zaidi. Kweli hatuna serikali wala mahakama. Hii CCM ni kwamba hakuna chama mbadala vinginevyo CCM ni sehemu ya wezi, majambazi, waonevu, wanyanyasaji wa raia wa nchi hii. Ni ngumu serikali hii kumsaidia mnyonge, huyo Makonda ndiyo jizi kubwa na tapeli anayeishi kwa njia za giza. Kwa serikali hii hii JF haiwezi kukusaidia hakuna anayejali na tatizo kubwa ni mkuu wa nchi.
Enzi la Magufuli kiongozi akipata habari km hizi haraka sana huyu jamaa angeshatafutwa mpaka na waziri kabla Rais hajaiona. Ila kizuri hakidumu! Kwa huyu mswahili wanyonge watateseka sana!
Japo mi sijui mambo ya Bet, ni wewe ndio unaisema hivyo serikali?

Wewe si ni chawa na mtetezi wa serikali?
 
Hapa tumeskiliza upande mmoja. Pigabet watu wanapiga hadi milion 600 hapo the grand casino na wanalipwa waje washinde kulipa milion 27? kwanza kwa sheria za kampuni za betting hawawezi kuruhusu wewe kuweka mkeka wa kiwango ambacho hawawezi kukilipa. Trust me ku sehem kuna shida jamaa aweke wazi
Ok. Nakubali ni maelezo ya upande mmoja na hayawezi kutufanya tuamue ni nani mkosefu. Swali: kwa nini wewe unataka tukuamini kwa haya haya maelezo ya upande mmoja? Yaani unaongea kama wewe ndiye hii kampuni! Kuna kitu unajaribu kuficha? Nina wasiwasi sana kwa sababu unavyotetea siyo kawaida. Kwa taarifa yako kulipa malipo ya waliopiga mil 600 siyo kigezo cha kuwa lazima wawe waaminifu. Anyways, nadhani ni vizuri mwanzisha thread atafute mwanasheria amsaidie.
 
Naitwa Silas John Charles. Nina malalamiko yangu dhidi ya kampuni ya Pigabet ambayo yamechukua muda mrefu bila kupata uamuzi, hali inayoninyima haki yangu ya kupata fedha ninazodai kiasi cha Shilingi milioni 27.7.

Tarehe 30/10/2024, niliweka beti yangu kupitia kampuni hiyo na beti hiyo ilithibitishwa na mfumo, ambapo nilipatiwa betslip pamoja na ujumbe wa mkataba. Baadaye, kampuni ilisimamisha mkeka huo bila kunipa taarifa. Nilikuja kubaini kuwa waliingia kwenye akaunti yangu na kuufuta (cancel) mkeka huo, jambo ambalo ninaamini ni kinyume na General Terms and Conditions zao wenyewe pamoja na Sheria ya Michezo ya Kubahatisha.
Tarehe 6/11/2024, niliandika barua kwa Gaming Board kuhusu suala hilo, na tarehe 15/11/2024 nilipokea majibu. Tarehe 13/12/2024, nilialikwa kwenye kikao cha usuluhishi kilichofanyika tarehe 16/12/2024. Katika kikao hicho, kampuni iliahidi kunilipa, lakini makubaliano hayo hayakuwekwa kwenye maandishi. Baadaye, tulipangiwa kikao kingine tarehe 17/1/2025, ambapo bado sikuwa nimepata malipo. Kampuni ilidai kuwa kiasi ninachodai ni kikubwa na kuniomba nipunguze. Nilikubali kushusha madai yangu kutoka milioni 27.7 hadi Shilingi milioni 20, lakini kampuni ilikataa na kusema ilikuwa tayari kunilipa Shilingi milioni 3. Nilikataa kwa sababu sikuona haki kupokea milioni 3 wakati madai yangu kutokana na beti hiyo ni milioni 27.7.

Baada ya hapo, tulisainishwa fomu ya kuonyesha kuwa usuluhishi umeshindwa kufikia makubaliano. Tarehe 18/2/2025, Gaming Board ilinijulisha kuwa imeshindwa kufikia mwafaka kati yangu na kampuni. Niliamua kwenda mahakamani, lakini shauri langu halikuweza kuendelea baada ya Pigabet kuwasilisha pingamizi kwamba Gaming Board haikuwa imetoa uamuzi kuhusu suala hilo, hivyo ikahoji kwa nini nimeenda mahakamani. Mahakama ilikubaliana kwamba Gaming Board ilipaswa kutoa uamuzi rasmi, na si kufanya usuluhishi pekee.
Tarehe 13/5/2026, nilirudi Gaming Board kuomba kuongezewa muda kisheria na kusikilizwa upya. Niliwasilisha barua ya kuomba kusikilizwa upya, ombi ambalo lilikubaliwa, na baadaye niliitwa tena kwenye vikao viwili. Hata hivyo, mpaka sasa Gaming Board bado haijatoa uamuzi wa maandishi. Ninaendelea kuambiwa nisubiri bila kupewa muda maalum wa lini uamuzi utatoka.

Suala hili limeanzia mwaka 2024 hadi sasa mwaka 2026, lakini bado sijalipwa fedha zangu. Wakati huo huo, kampuni ya Pigabet inasisitiza kunipa Shilingi milioni 3 pekee, jambo ambalo silikubali kwa kuwa madai yangu ni Shilingi milioni 27.7. Pia, ninapowasiliana na kampuni hiyo kuhusu suala langu, nimekuwa nikijibiwa kwa lugha ambayo si nzuri.

Naomba mnisaidie kupaza sauti yangu ili mamlaka husika zilifuatilie suala hili na kuishinikiza kampuni ya Pigabet pamoja na Gaming Board kuchukua hatua na kutoa uamuzi wa haki. Nimejaribu kulifuatilia suala hili kwa muda mrefu bila mafanikio, na nina hofu kwamba likiachwa kimya kimya sitaweza kupata haki yangu.
Hauna akili.
 
Huwa mnapata wapi nguvu ya kuweka pesa kwenye kampuni zenye utapeli?
Kuna best yangu kuna kampuni kapiga 58 million aliwekewa hapo hapo automatically yeye mwenyewe ndo akaihamishia halotel Polepole mpaka ikaisha.
Hajaitwa popote wala hajapigwa picha za promotion wala kupigiwa simu.
Sasa million 58 ingekuwa piga bet wangekuteka kabisa.
Nione pm pesa yako utaipata ndani ya siku saba. Ila hiyo m7 iwe yangu wewe ubakiwe na m20
 
Sasa million 58 ingekuwa piga bet wangekuteka kabisa
Itakuwa BetPawa nahisi.
 
Mwenzako anajadili kwa mantiki wewe unajadili kihisia. Ungekuwa unasoma terms and conditions za hayo makampuni ya kubeti usingeuliza haya maswali.

Siku nyingine bashiri fixed match, shinda alafu kosa hela uende mahakamani uone kama utapewa.
Huwezi tumia mihemko kisha umzidi anayetumia logic, common sense na maarifa.
Fixed game ndio zinakuwaje hizo mkuu?
 
Japo mi sijui mambo ya Bet, ni wewe ndio unaisema hivyo serikali?

Wewe si ni chawa na mtetezi wa serikali?
Tena ni poti huyo au kaolewa na Poti labda kama Ke nilipata conclusion hiyo Uzi wa dokta bagonza watu wote tunakemea uonevu wa mapoti yeye na wenzake wa3 wakawa wanasapoti. I stand 2 be corrected.
 
Huwa mnapata wapi nguvu ya kuweka pesa kwenye kampuni zenye utapeli?
Kuna best yangu kuna kampuni kapiga 58 million aliwekewa hapo hapo automatically yeye mwenyewe ndo akaihamishia halotel Polepole mpaka ikaisha.
Hajaitwa popote wala hajapigwa picha za promotion wala kupigiwa simu.
Sasa million 58 ingekuwa piga bet wangekuteka kabisa.
Nione pm pesa yako utaipata ndani ya siku saba. Ila hiyo m7 iwe yangu wewe ubakiwe na m20
Unadhihirisha watu sa system aka machawa mlivo wabadhilifu kudadeki zenu hovyo sana
 
Back
Top Bottom