Nimeshindwa kuvumilia, naomba msaada wenu jinsi ya kuachana na mzazi mwenzangu

Nimeshindwa kuvumilia, naomba msaada wenu jinsi ya kuachana na mzazi mwenzangu

[emoji3]haya mambo bwana

Mwingine huku
Amegombana na mzaz mwenzie tangu mimba iko karibu miez 8

Ajabu ananiambia kelphin mimba yangu imekupenda wewe[emoji23][emoji23]

Yan tabu tupu
 
Huyu mdada kipindu amebeba mimba, alisitisha huduma zote alizokuwa akijihudumia na kusema nimhudumie Mimi coz nimempa mimba, nikakubali. Akahama alikuwa amepanga(vyumba viwili na sebure) akahamia nyumba mzima, Kodi kwangu, nikakubali. Akalazimisha nitoke kazini nikaishi nae au nihakikishe Kila baada ya wiki naenda kumuona kitu ambacho hakiwezekani Kwa mazingira ya kazi yangu. Hapo ndipo mtiti uliopoanza.

Akaanza kwenda Kwa waganga usiku na mchana. Huko akaambiwa Mimi Nina mke na watoto wawili ndio maana siendi kwake muda mwingi nipo Kwa hiyo mke wangu(kifupi Mimi sijawahi kuoa na hiyo mtoto wake ndio mtoto wangu wa kwanza).

Ikafika kipindi akahamia kabisa Kwa huyo sijui ndo ostadh sijui vitu gani Kila siku ni kupigwa Dua ili nirudishe mapenzi kwake niachane na huyo anaedai ni mke wangu. Kwangu nikawa nachukulia Kama ujinga flan tu. Mambo ni mengi mkuu.
Pole
 
Hapa ni kwenda ustawi wa jamii tu.
Utajikuta badala ya kulia 300000 unayoitoa utatoa 75000 tu.
Maana kwenye malezi huwa inataka wewe uchangie na mzazi mwenzio achangie.
Huwa hakuna ya wewe kuwahudumia wote wawili
 
Huyu mdada kipindu amebeba mimba, alisitisha huduma zote alizokuwa akijihudumia na kusema nimhudumie Mimi coz nimempa mimba, nikakubali. Akahama alikuwa amepanga(vyumba viwili na sebure) akahamia nyumba mzima, Kodi kwangu, nikakubali. Akalazimisha nitoke kazini nikaishi nae au nihakikishe Kila baada ya wiki naenda kumuona kitu ambacho hakiwezekani Kwa mazingira ya kazi yangu. Hapo ndipo mtiti uliopoanza.

Akaanza kwenda Kwa waganga usiku na mchana. Huko akaambiwa Mimi Nina mke na watoto wawili ndio maana siendi kwake muda mwingi nipo Kwa hiyo mke wangu(kifupi Mimi sijawahi kuoa na hiyo mtoto wake ndio mtoto wangu wa kwanza).

Ikafika kipindi akahamia kabisa Kwa huyo sijui ndo ostadh sijui vitu gani Kila siku ni kupigwa Dua ili nirudishe mapenzi kwake niachane na huyo anaedai ni mke wangu. Kwangu nikawa nachukulia Kama ujinga flan tu. Mambo ni mengi mkuu.
Hamna mke hapo.
 
Kiongozi i[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Nmecheka kinoma
Ni hatari sana kamkubwa. Sometimes nakaa nawazaaaaa mpaka kichwa kinauma.
 
Miak 23[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] Ukampa na ATM card??? Wew ndo mwenyw matatizoo..
Inawezekana kabisa kamkubwa, katika kujitahidi kuokoa jahazi kumbe nazidi kulizamisha.
 
Habarini za asubuhi waungwana.

Kwanza kabisa nichukue nafasi hii kuwapa HESHIMA ya pekee wale wote mlioko kwenye ndoa.

Turudi kwenye mada, Nimebahatika kupata mtoto na sasa ana miezi miwili, lakini vitimbi ninavyokutana navyo kwakweli nimeshindwa kuvumilia.

Ombi langu kwenu ni hili, nahitaji kuachana kabisa na huyu mzazi mwenzangu, KABISA, isiwepo hata chembe ya mawasiliano.

Je, inawezekana kwa umri wa huyu mtoto? Kama inawezekana naomba ufafanuzi wa hatua za kuchukua ili mtoto awe katika mazingira salama. Pia Kama haiwezekani (DAAH) japo itaniumiza nishaurini cha kufanya sababu nipo mwisho.

NB:
Huyu mtu hatuishi pamoja, anaishi na mtoto na mimi naishi kivyangu ila nahusika kwa kila kitu kuhusu yeye na mtoto.

Ahsanteni.
Duuh
 
Back
Top Bottom