Nimeshuhudia ajali asubuhi hii, Julai 11, 2024 barabara ya Airport Mwanza jirani na Rock City mall

Nimeshuhudia ajali asubuhi hii, Julai 11, 2024 barabara ya Airport Mwanza jirani na Rock City mall

Sometimes hawa bodaboda ni kufa nao, huwezi kumkwepa mtu mmoja ukaenda kuua raia wengine wengi wasio na hatia
 
Hawa boda na bajaj ni mtihani sana
Tena haswaaa!! Huwa nawaza zina nn hizi, yaan mtu hata awe smart vipi. Akianza kuwa dereva boda au bajaji lazima abadilike sijui wanakuajee hata. Lol
 
Sheheee bodaaa hakwepekii huyoooo oooh m napitagaa naooo kilmojaaa wengine mapepo jny imejaa kwenye mfumoo
Siku ukigonga boda ndio utajua kuwa hujui,wana umoja sana hao watakuzingua mbaya
 
Asubuhi hii barabara ya kuelekea Airport Mwanza jirani kabisa na Rock city mall, Isuzu Journey imeacha barabara na kuingia kwenye moja ya nyumbani zilizo jirani na Mall.

Chanzo ni boda asiye na side mirror aliyetaka kuhama lane na dreva kumkwepa kitu kilichopelekea dereva kushindwa kulimudu gari kuhama na kufungua break ndani ya mojawapo ya nyumba.

Vifo na majeruhi sikupata muda nilikuwa nawahisha mtu somewhere urgent. Bodaboda mjinga sana maana baada ya kuona amesababisha ajali alisepa fasta.
Hapo sasa njia nne ajali inatokeaje bora angemgonga boda
 
Tukisema mnatuona makatili, siwezi kuhatarisha maisha yangu na abiria wangu kisa mpumbavu mmoja asiejua thamani hata ya uhai wake. akijichanganya siingii mtaroni, sigongi kingo wala nini napita nae kama hakuwepo. Trust me wakiona mtu hana dalili ya kumkwepa huwa wanaingia wenyewe mtaroni au vichakani. Sasa wewe endelea kujidai msamaria mwema uingie mitaroni au bondeni ufe halafu wao wanakucheka.
 
Boda akiwa mbele yako usimwamini,Chukua tahadhari mapema.
 
Ndugu muandishi wa habari kwanini Tatizo kila siku ni 'site mirror' kwa hao bada boda duh.
97% ya bodaboda zote huwa hazinaga "site mirror". Ukiwauliza wanasema site mirror zinazuia kupaki pikipiki karibu-karibu hapo kijiweni, site mirror zinaibiwa kirahisi, zinavunjika hovyo ukianguka kwa bahati mbaya na huko madukani haziuzwi moja-moja bali zinauza mbili kwa pamoja na sio rahisi kupata original, ila wapo wanaosema ukweli kwamba wanaziondoa makusudi.
 
Boda akiwa mbele yako usimwamini,Chukua tahadhari mapema.
Kabisa aisee. Wale jamaa akili zao zinawatosha wao wenyewe. Anapiga indicator kukuonesha anaelekea/anaingia kushoto lakini paap! anaingia kulia.
Ck hizi wamefunga Hazard na anaweka hazard mwanzo-mwisho na hakuna kitu cha tahadhari mbele yake. Hao jamaa! we acha tu. Chukua tahadhari kweli.
 
Boda boda asiye na side mirror hapaswi kuhurumiwa, angemsaga kichwa tu.
 
Back
Top Bottom