Mchochezi
JF-Expert Member
- Feb 29, 2012
- 10,962
- 7,830
Kila jambo huwa lina mwisho wake. Nimeshuhudia timu bora ya wakati wote Barcelona ikitamba katika soka la kisasa. Timu zote imara zilinyanyaswa na Barcelona ya kuanzia mwaka 2008-2012. Kisha Barcelona ya 2013 - 2015.
Wote ni mashahidi jinsi Messi, Xavi na Iniesta walivyoipa timu hii mafanikio. Kisha ikaja MSN nayo ikatamba na kunyayasa vilabu vingi vya Ulaya kama sio Dunia.
Na sasa naona mwisho wao Umefika, ni kama nilivyoshuhudia Mandela akifikia mwisho wake hapa Duniani, ni kama nilivyoshuhudia Ukuta wa Berlin ukidondoshwa mwaka 1990, Ni kama tulivyoshuhudia mwisho wa maisha ya Papa John Paul wa II, Ni kama nilivyoshuhudia mwisho wa Barack Obama kuwa Rais wa Marekani na sasa nashuhudia mwisho wa Timu bora ya wakati wote, Barcelona ikifikia ukingoni. Ni ukweli unaouma laikini hatuna budi kuukubali.
Asante mungu nimeishi katika kipindi cha timu bora ya wakati wote, na mimi nitakuja kuwasimulia wajukuu wangu panapomajaliwa.