Nimeshuhudia mwisho wa Barcelona

Nimeshuhudia mwisho wa Barcelona

Mchochezi

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2012
Posts
10,962
Reaction score
7,830
Kila jambo huwa lina mwisho wake. Nimeshuhudia timu bora ya wakati wote Barcelona ikitamba katika soka la kisasa. Timu zote imara zilinyanyaswa na Barcelona ya kuanzia mwaka 2008-2012. Kisha Barcelona ya 2013 - 2015.

Wote ni mashahidi jinsi Messi, Xavi na Iniesta walivyoipa timu hii mafanikio. Kisha ikaja MSN nayo ikatamba na kunyayasa vilabu vingi vya Ulaya kama sio Dunia.

Na sasa naona mwisho wao Umefika, ni kama nilivyoshuhudia Mandela akifikia mwisho wake hapa Duniani, ni kama nilivyoshuhudia Ukuta wa Berlin ukidondoshwa mwaka 1990, Ni kama tulivyoshuhudia mwisho wa maisha ya Papa John Paul wa II, Ni kama nilivyoshuhudia mwisho wa Barack Obama kuwa Rais wa Marekani na sasa nashuhudia mwisho wa Timu bora ya wakati wote, Barcelona ikifikia ukingoni. Ni ukweli unaouma laikini hatuna budi kuukubali.

Asante mungu nimeishi katika kipindi cha timu bora ya wakati wote, na mimi nitakuja kuwasimulia wajukuu wangu panapomajaliwa.
 
Mie nakuunga mkono kwenye hili ila sio mwisho wao nadhani watajipanga na kuanza upya kama kipindi cha Rijkaard timu ilifanya vibaya ila baadae walirudi na kufanya vizuri kinachowasumbua kikubwa Barcelona ni ukongwe wa wachezaji wao na ndio naona huyu kocha mpya Ernesto Valverde amekuja na falsafa ya kuwakomaza vijana kama kina Sergi Roberto,Dennis Suarez maana nadhani mtu kama Javier Mascherano umri unamtupa mkono sasa anahitaji mbadala wake Andre Iniesta nae anaelekea huko kwa hiyo itachukua muda kidogo kuwapika hawa vijana ila nina imani chama litarudi tena na kufanya vizuri tujifunze kutokata tamaa ili tufanikiwe.
 
Kizazi cha sasa cha Barcelona kimefikia ukingoni, ni wakati wa Barcelona kuanzisha kizazi kingine.
Jana nilishuhudia Barcelona isiyokua na meno, jana nilimuona Messi akicheza kama namba 8,10,9 alifanya hivi akijaribu kufukia mashimo ya wengine lakini alishindwa.
Kuna wachezaji wengi hawana hadhi ya kuichezea Barcelona, wa kwanza ni Andre Gomes. Uyu jamaa sijui walimuokota wapi?
 
Lucho alituletea falsafa yake ya Direct football akanunua na magarasa yake ambayo hamna kitu yanafanya.
1. Andre Gomes
2. Lucas Digne
3. Alex Vidal
4. Paco Alcacer
5. Jeremy Mathieu
Hawa hawastahili kucheza club kama Barcelona.
 
Shakira jana alikua anamuwaza mpenzi wake tu. Hakuna chochpte alichofanya. Kwenye ndio wakapotezwa kabisa, bora ya Messi kidogo alijitahidi.

Binafsi Madrid pamoja na Zidane ninawaona wakisumbua zaidi ya misimu minne ijayo kama Zidane hataingiliwa katika mipango yake.

Namuona Asensio akiingia katika ushindani wa Ballon d'Or tena bila ya kupepesa macho. Ni wazi wazi.
 
Back
Top Bottom