Nimeshuhudia wizi wa ajabu huku kwetu

Hao wezi ni wapumbavu sana, bora wangeiba rangi tu ijulikane tu ila kumwaga inaonyesha hilo eneo unaloishi watu bado wanaishi maisha ya old stone age
Usiwalaumu sana eti ndoo ikiwa na rangi ni nzito ati
 
Hawo wanajifunza kuiba, mabingwa hawaibi vitu vibavyoonekana mizigo.
 
Hao wametumwa kumkomoa huyo mwenye nyumba au walikua na personal issues na mlinzi
 
Aina hii ya wezi huwa wanaitwa "amateur thieves". Hawa wanaweza kuingia ndani nyumbani kwako halafu wakaiba kiatu kimoja cha mguu wa kushoto, wakakuachia kingine kile cha mguu wa kulia. Wao kuiba ni aina ya mchezo fulani wa burudani kama vile mtu kucheza mpira au draft
 

Haah haah,hao watakuwa field wanaipambania coursework mkuu
 
Kwa hiyo soo
Ulitaka soo waibe na rangi soo?
Ulijuaje soo kwamba soo wana shida na rangi soo?
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji119]
Mkuu kula like[emoji106]
 
Vibaka wa uswazi ni wapumbavu sana nakumbuka kuna likizo moja tuliondoka mkoani na familia bila ya kumwacha mtu home basi bana vibaka walivunja ila cha ajabu hawakuiba mifuko ya saruji, pikipiki, tv, wala kitu kikubwa cha thamani.

Ila walichofanya ni kupika msosi wakala na kunywa bia zote zilizopo kwenye friji, waliiba vyombo vya jikoni karibia vyote, mapazia na vyakula vyote vilivyo hifadhiwa kwenye friji na vilivyopo stoo.

Yaani hadi leo hii sifahamu akili zao zilikua zina waza nini hasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…