Nimeshuhudia wizi wa ajabu huku kwetu

Nimeshuhudia wizi wa ajabu huku kwetu

Yale yaleee Gari kupata ajali huko Morogoro Watu wanakimbilia kuiba Battery! Ndipo uwezo wetu wa Kufikiri ulipofikia.
 
Kama hii niliwahi ona sehemu za Endasaki_Hanang wezi wanamwaga mahindi chini wanasepa na mifuko.
 
Kisa cha jana

Huku mtaani kwetu bwana kuna nyumba fulani inafanyiwa finishing. Hakuna aliyehamia bado.

So wamemaliza plasta so wanataka anza skimming na rangi. Wameleta ndoo kibao za rangi kwa ajili ya kuanza kazi. Nyumba ina geti so vifaa vinakaa ndani na fundi pia mmoja hulala humo.

So anaelala alitoka so wazee wa kazi wakaja kumuotea nadhan walimsomea raman ni mzee wa gambe.

Kinachonishangaza ni kitu walichoiba[emoji1787].

Eti wamekuta zile ndoo zina rangi, wao wana shida na ndoo.. so wamemwaga rangi kadhaa wakasepa na ndoo.

Rangi zile nyingine zina kost 130k za nje na zingine ni 32k zile za rangi. Lkn wameiba ndoo ya 2k.
Dahh.. si bora wangeomba jamaa akimaliza kujenga awape
 
Umenikumbusha TANGA.
Kuna mlinzi alikua analinda duka kubwa sasa kila wezi wakija wanamkuta mlinzi Yuko ngangari.
Kuna siku yule mlinzi alipitiwa na usingizi wezi wakaja kumvua nguo zote na kuondoka nazo. Halafu hawakuiba kitu. Waliiba nguo za mlinzi mpaka boxer. Asubuhi mlinzi anakurupuka anajikuta Yuko Kama alivyozaliwa.
Baada ya hapo mlinzi alikabidhi upinde na rungu kwa mwenye duka na kutokomea kusikojulikana.
Watu walikua wanajiuliza, Kama Hawa wahuni walimvua nguo zote huyu mbana wakati hajielewi, inawezekana Kuna utundu walimfanya sema hakusema.
 
Back
Top Bottom