Nimeshuhudia wizi wa ajabu huku kwetu

Kuna wamasai waliiba monitor (screen) wakaacha CPU, Zilikuwa tano.
 
Yale yaleee Gari kupata ajali huko Morogoro Watu wanakimbilia kuiba Battery! Ndipo uwezo wetu wa Kufikiri ulipofikia.
 
Kama hii niliwahi ona sehemu za Endasaki_Hanang wezi wanamwaga mahindi chini wanasepa na mifuko.
 
Dahh.. si bora wangeomba jamaa akimaliza kujenga awape
 
Umenikumbusha TANGA.
Kuna mlinzi alikua analinda duka kubwa sasa kila wezi wakija wanamkuta mlinzi Yuko ngangari.
Kuna siku yule mlinzi alipitiwa na usingizi wezi wakaja kumvua nguo zote na kuondoka nazo. Halafu hawakuiba kitu. Waliiba nguo za mlinzi mpaka boxer. Asubuhi mlinzi anakurupuka anajikuta Yuko Kama alivyozaliwa.
Baada ya hapo mlinzi alikabidhi upinde na rungu kwa mwenye duka na kutokomea kusikojulikana.
Watu walikua wanajiuliza, Kama Hawa wahuni walimvua nguo zote huyu mbana wakati hajielewi, inawezekana Kuna utundu walimfanya sema hakusema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…