Tetesi: Nimesikia Lumumba wanasema kwa wabunge "10 Yatosha"

Tetesi: Nimesikia Lumumba wanasema kwa wabunge "10 Yatosha"

Kabisa, tangu nakua mpaka leo nina ndevu kuna watu nawasikia ni wabunge tu,10 yatosha kabisa kabisa.
 
Nafikiri hapa Dr wa Sayansi anataka ku apply law of equillibrium! Wanapunguziwa miaka wabunge na anaongezewa yeye. Sasa hao waluokuwa wanapiga kelele kuwa aongezewe miaka sijui wataishia wapi? Waingereza wana kajimsemo chao wenyewe, " Be careful what you wish for"
 
Mimi huwa sijawahi kumwelewa Rais anapochagua watu wenye miaka Zaidi ya 70 kuwa mawaziri au mabalozi. Sasa ubunge ndio sielewi kabisa
 
Hata kwenye rasimu ya Warioba maoni yetu sisi wananchi ilikuwa mwisho wa ubunge iwe ni miaka 10, lakini wabunge wa ccm wakachezea rasimu ile, na kulazimisha eti mbunge aendelee kukaa madarakani mpaka wananchi wachoke. Kama wameamua hivyo hata ile tabia ya kupitisha sheria za kipuuzi itapungua bungeni.
Hapo Chadema Grace Kihwelu ana miaka 20 bungeni sema tu ametangaza kustaafu!
 
Lah, Mzee wa vijicenti mali ganyanja!! Finally!!
 
Hiyo kauli ya "kumi yatosha" nilishawahi msikia Makonda anaitoa, na yeye aliegemea kwenye kutumia ubunge kama nafasi ya ajira, ukishapata mtaji muachie mwenzako nae ale.

Binafsi sioni tija ya hiyo kauli hasa kwenye kubadilisha mindset ya wabunge wa CCM wakiwa bungeni, siku zote wataendelea kuweka maslahi ya chama chao mbele zaidi ya maslahi ya nchi.
 
...
IMG_20200617_092428.jpeg
 
Wazo zuri Ila tubalance ili kuhakikisha hatukosi na wazoefu wa kuwakimbilia kwa ushauri na kushirikiana nao.
 
Wawe wazi tu haya ni madhara ya kusajili mamluki na wala si kitu kingine na hii ni mbinu ya kuwapunguza maana wote wamejazana CCM.

kama wako serious,kwanini wasiliweka kikatiba wakati wao ndio wengi ndani ya Bunge ili liwe la kitaifa na si la kichama?

Anyway,wamesubiri Bunge limeisha sasa wanaanza kuwageuka baada ya kuwa wamepetisha Bajeti na sheria za kuwalina watukufu.

Fufueni mchakato wa katiba ya mzee Warioba haya yote yamo kama sikosei.

Mwaka huu lazima tu mvurugane.
 
Ndugai keshamaliza miaka 10 ni nani atamtoa wakati keshamhakikishia Mkuu kuwa ataibadili Katiba kupitia bunge!
 
walafi wa madaraka ambao ndio wengi sana ccm kamwe hawawezi kukubali
 
Nancy Pelosi ana miaka mingapi?Kwanini wamarekani wanamwamini zaidi? Sio tu kuwa mbunge bado ni spika.
Experience is the best teacher.
 
Back
Top Bottom