Nimesikitika sana kuona CHADEMA wanalishambulia Bunge kwa kuisimamia Serikali

Yani hiki chama hawajielewi hata, kimejaa ushabiki kuanzia wanachama mpaka viongozi. Hakuna lolote la maana wamewahi kulisimamia mpaka mwisho.

Hivi unawapaje nchi hawa watu wasiojielewa.
 
Chadema wakisubiri njia za kisitaarabu kwa kufanya siasa za kistaarabu eti ndio washike dola watasubiri miaka 1000.

Ni kweli Wananchi wamelala na ni waoga lakini nani wa kuwatoa katika usingizi huo??? ,wanatakiwa wa force vitu litakalo tokea litokeee uone kama kesho tu hawataingia Ikulu.

Sasa wamebaki Kumuomba mtesi wao SAMIA amwachie Mbowe,weka mikakakti ingia mtaani Fanya matukio mpaka SAMIA amwachie Mbowe kwa kutokupenda.
 
Ndugai ni spika wa bunge na amemkosoa rais ambaye ni kiongozi wa serikali.

Chadema mmeona kafanya kitendo kibaya mmemtukana matusi ya nguoni.
Ndugai hajaikosoa serikali
Amemuropokea Samia
Utaratibu wa vikao vya bunge na namna yakupeleka hoja bungeni inafahamika.

Huku nje hajaongea kama Spika, ameongea kama mchapa bakora mhuni.

Hoja yake ina msingi Ila imekaa kinafiki, hata kwenye hansard za bunge haijaingia.
 
Wewe kumbe ni Zuzu ee? Ndugai anaweza kuisimamia serikali akiwa nje ya bunge? Yaani Ndugai kakusanya ndugu zake hicho Kikao ndo kitumike kuisimamia serikali?
 
Spika ametimiza wajibu wake wa kikatiba wanafiki mtupishe
 
Kwani wamesemaje??? unaeza tupia walichosema pia...

Tusije kuwa tunapika majungu
 
Tofautisha maoni ya speaker wa bunge na maazimio ya bunge. Speaker kaongea hayo at individual capacity . Maana kwa kanuni za bunge maamuzi yanafanyika kwenye Chambers. Kwa mfano, Speaker wa bunge Job Ndugai aliposema atamlazimisha Magufuli aongeze muda wa urais apende asipende lilikuwa bunge au maoni ya speaker. Bunge linatakiwa liwe na mamlaka ya kupitisha kiwango Cha kukopa nje na sio kulalamika na kurusha madongo Kama anavyofanya Speaker Ndugai.
 
Ndugai ni spika wa bunge na amemkosoa rais ambaye ni kiongozi wa serikali.

Chadema mmeona kafanya kitendo kibaya mmemtukana matusi ya nguoni.
Wamemtukanaje tena hayo ya nguoni, happy hebu tumegee japo mawili waliotukana.. tuone!
 
Chadema mmewaangusha sana wananchi wapenda demokrasia....mnatukana bunge kuisimamia serikali!!😭😭😭😭
Nia yako sio demokrasia Wala Nini Bali lengo lako ni kutaka kuingiza CHADEMA kwenye maujinga ya CCM . Pesa mnakopa Kila siku na tozo mnachukua, muda ukifika mnaanza kuumbuana wenyewe kuwa nchi itapigwa mnada. Endeleeni kuangaika na mizigo yenu achaneni na CHADEMA.
 
Ni lini CHADEMA imetoa official statement ya kwamba inapinga maoni ya Ndugai?. Jifunze kutofautisha kauli ya chama na kauli ya mwanachama.
 
Chadema kimejionesha ni chama cha matukio na kipo kinaangalia upepo wa kula ruzuku.
Wewe nimekusoma mrengo wako. Umetoka kwenye kulitukana bunge mpaka kwenye ruzuku. Naona moyo wako hauna amani kabisa, baada ya yote mliyoifanyia CHADEMA bado ipo hai, Sasa umebakia kuokoteza vimaneno visivyo na maana na kuisingizia CHADEMA. Hautapata amani mpaka utubu.
 
Kwa hiyo Spika akiikosoa serikali Chadema mnaita ni uhuni?
 
Kwa hiyo Spika akiikosoa serikali Chadema mnaita ni uhuni?
 
Hivi tuna bunge kweli? Au vikao vya wanafiki wanaoitumia ukumbi wa bunge?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…