Nimesikitika sana kuona muhitimu wa degree ya TEHAMA (ICT) hajui kutumia Google Map

Nimesikitika sana kuona muhitimu wa degree ya TEHAMA (ICT) hajui kutumia Google Map

KING MIDAS

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2010
Posts
8,589
Reaction score
16,936
Nikiwa dukani kwangu napitia mahesabu ya mapato na matumizi ya wiki iliyopita, akaja mteja anataka madawa fulani, madawa hayo ni slow moving items hivyo huwa yanakaa store, hayapangwi dukani.

Basi nikaona si mbaya huyo mteja akiwa anahudumiwa (akisubiri dawa zake) aje ofisini kwangu anywe walau kikombe cha kahawa.

Mdada akaja ofisini, nikamwambia tea girl amwandalie kahawa mgeni. Baada ya muda mfupi akaletewa kahawa na story zikaendelea.

Tukawa tunaongea mengi, na akaniambia anauhitaji wa kazi kwani kasoma IT.

Basi kwenye story akanijulisha kuwa dawa anazituma Karatu, na ameagizwa azitume kwa basi la Dar Express. Akasema yeye hajui ofisi zilipo, mimi nikamwambia naijua ofisi yao ya Kisutu.

Akaniuliza kama Shekilango wana ofisi, nikamwambia sina uhakika, ila kwanini usicheki kwenye Google Map?

Nikapigwa na butwaa aliponiambia hajui kutumia Google Map. Yaani na degree yake ya IT hajui kutumia app hiyo muhimu? Nikajiuliza sasa nikimchukua huyu, atakuwa amekuja kujifunza kazi au kufanya kazi?

Anasema amesoma visual basic, java, na C++, kasoma networking na troubleshooting ahh, hamu ya kuendelea kumsikiliza ikakata kabisa.

Mzigo wake ulipokuwa tayari, nikamuaga na.kumuongezea 10,000 ya nauli.
 
Shida ya kusoma vitu usivyokua na passion navyo, wapo wengi tu wenye upuuzi huo. Kiukweli mimi sijasoma IT lakini nina passion nayo na mpaka saizi ile basic ya IT ninayo, vitu vidogodogo havinipigi chenga.
 
Kuna ile kasumba ya mazoea au uelewa wa kuuliza ili swali "eti hivi ofisi za taasisi fulani ziko wapi?" Wakati mtu ameshika smartphone...Google map ni ugonjwa wa wengi usiwe suprise sana..kuna wahitimu fulani walikuja wanatafuta ofisi za shirika fulani nikawaambia hebu fungueni google map niwaonyeshe na walifika hizo ofisi kwa msaada wa simu zao....bado matumizi ya smartphone kwa wengi hata wasomi ni tatizo....si ajabu kukuta wasomi wanabishana eti kutoka Ubungo kwenda Mbezi na kutoka Ubungo kwenda karikoo wapi mbali? Wakati wameshika smartphone zenye map ...
 
Back
Top Bottom