Nimesikitika sana kuona watu wanafurahia wamachinga kufukuzwa mjini

Nimesikitika sana kuona watu wanafurahia wamachinga kufukuzwa mjini

Kipunga

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2021
Posts
264
Reaction score
590
Inasikitisha sana kuona Mtanzania mwenzio anabaguliwa kwamba yeye hafai kukaa mjini akakae huko mbali ajifiche na mjini ni kwa watu wenye uwezo fulani halafu wewe unafurahia eti sababu haikuhusu, imeniuma sana.

Viongozi acheni ulimbukeni hata Ulaya machinga wapo. Pia katika hao machinga wengine ni wasomi wakubwa ila hawana ajira.

Ujumbe wangu kwa wewe mnafki wa JamiiForums, acha kufurahia shida za wamachinga kwani hawakupenda kuwa wamachinga ila ni mifumo isiyofaa ya hii nchi.

Kinacho nishangaza JF kila mtu msomi, tajiri, ana gari, anaishi mjini, mjuaji, meneja, ana nyumba nzuri. Hahahahahahahaha JF bwana


KIPUNGA
 
Tunakosea Sana hawa Kuwaita machinga tuwaite Tu wafanya biashara wenye mtaji mdogo.


Machinga ni neno lililotokana na neno la kiingereza hasa kutoka marekani wakiitwa matching nigga ( machinga)
Maana yake ni wafanya biashara wanaotembeza

Sasa anayejenga kibanda siyo machinga maana hatembezi uisipokuwa wateja wanamkuta hapo

Hawa ni wafanya biashara wadogo
 
Acha kupotosha,sio kweli kwamba hawatakiwi mjini bali wanatakiwa wafanye biashara maeneo stahiki na sio kukaa barabarani, kwenye njia za watembea kwa miguu na kuziba mifereji ya maji taka,kodi fremu ufanye biashara.
 
Unasema machinga hata Ulaya wapo uko sahihi, lakini kuna utaratibu wa kufanya biashara si kama ilivyokua Kariakoo,
Mambo mengine umeandika kwa jazba sana.
Nilikua nawafikishia ujumbe wasomi wa jf ambao tangu uhuru hawajafanikiwa kutengeneza hata njiti ya kiberiti
 
Wamachinga hawajafukuzwa,ila wanatakiwa wafanyebiashara kwa kufuata sheria na kanuni,wakafanye biashara maeneo maalumu,kwenye masoko.Na kama wapo wenye uwezo,wawe kikundi kama wanne au wangapi,wachukuwe Frem,wawe wanalipa kodi stahiki.

Hata viwanda,makampuni mengi sio mali ya mtu mmoja,wapo walioshirikiana kuanzisha viwanda ,wapo Wana hisa,.na wanafanyabiashara kwa kufuata sheria na kanuni.

Wapo wamachinga Wana mitaji ya mpaka milioni kumi,wanamiliki majumba,magari,na hawataki kufunguwa Frem. Wakati yupo mtu ana mtaji wa milioni moja,na kafunguwa duka katika Frem,mtaani ya kuuza nafaka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha kupotosha,sio kweli kwamba hawatakiwi mjini bali wanatakiwa wafanye biashara maeneo stahiki na sio kukaa barabarani, kwenye njia za watembea kwa miguu na kuziba mifereji ya maji taka,kodi fremu ufanye biashara.
Sasa huo ndio unafki wenyew enz za magu hamna mtu alie sema hayo matajiri wa jf bana hahahah
 
Back
Top Bottom