Nimesikitika sana kuona yanayotokea pale Udart

Nimesikitika sana kuona yanayotokea pale Udart

Sijui kwa nini, ila nina imani kubwa sisi tuna uwezo mdogo wa kufikiri. Hii tabia ya kula ugali/wali mwingi-mboga kidogo imeathiri watanzania karibia wote kwenye uwezo wa kufikiri.
 
Sijui kwa nini, ila nina imani kubwa sisi tuna uwezo mdogo wa kufikiri. Hii tabia ya kula ugali/wali mwingi-mboga kidogo imeathiri watanzania karibia wote kwenye uwezo wa kufikiri.
Uko sawa kabisa ongezea na ugali, tumeshayajadili sana humu, hawa viongozi wanaosimamia hivi vitu by nature hawana asili na usimizi wa vyombo vya moto, sasa mtu kama huyu atawaza nje ya box kuhusu gari fulani niiandalie nini baada ya muda fulani?

Dereva anapeleka tatizo la gari lakini unakuta kiongozi mwingine anasema hiyo gari irudi barabarani hivi mnategemea kweli hiko chombo kitakuwa imara huko barabarani?

Mradi unapesa nyingi sana ni bora kwenda kujifunza kwa watu binafsi wanavyoendesha makampuni yao ya usafirishaji miaka na miaka, vizazi kwa vizazi kampuni hazitetereki zipo tuu.

Hii badili badili bado hawajapata mtu sahihi angalau kwa marehemu David Mgwasa kulikuwa na nafuu na baada ya kuona huko baadae kutaleta shida kutokana na aina ya uendeshaji uliokuwa unaelekea akakaa pembeni.
 
Nimesikitika tena nimesikitika sana nilipoona clip ikionyesha jinsi mabus ya UDART yalivyoachwa hovyo yakizama kwenye matope kwenye karakana ya UDART kisa uharibifu wa gearbox. Mhe. Waziri Mkuu anagomba kwa uchungu lakini wapi.

UDART unaongozwa na PhD holder aliyetoka TRA na anayejua jinsi ya kukusanya mapato. UDART imefikia hata mfumo wa kukusanya mapato kupelekea kuvurugwa.

Tayari mabus 40 yako juu ya mawe, hawajaagiza mabus mapya sasa yapata miaka mitano. Yamebaki mabus 100 tena mengi yanasuasua. Hata Mtendaji Mkuu aliyepelekwa na Serikali hataweza chochote labda Serikali imtafute mwekezaji wa kuiendesha UDART. Hivi Watanzania tumelogwa na nini?. Kila tunachokabidhiwa hakifaulu. Tujiulize tuna matatizo gani sisi Watanzania?.
DART ni mmiliki na msimamizi wa miundombinu ya mwendo kasi na UDART ni kampuni ambayo inamiliki mabasi ya mwendokasi na kuendesha Biashara ya usafirishaji kwenye miundombinu ya DART.

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom