Nimesikitika sana kuona yanayotokea pale Udart

Sijui kwa nini, ila nina imani kubwa sisi tuna uwezo mdogo wa kufikiri. Hii tabia ya kula ugali/wali mwingi-mboga kidogo imeathiri watanzania karibia wote kwenye uwezo wa kufikiri.
 
Sijui kwa nini, ila nina imani kubwa sisi tuna uwezo mdogo wa kufikiri. Hii tabia ya kula ugali/wali mwingi-mboga kidogo imeathiri watanzania karibia wote kwenye uwezo wa kufikiri.
Uko sawa kabisa ongezea na ugali, tumeshayajadili sana humu, hawa viongozi wanaosimamia hivi vitu by nature hawana asili na usimizi wa vyombo vya moto, sasa mtu kama huyu atawaza nje ya box kuhusu gari fulani niiandalie nini baada ya muda fulani?

Dereva anapeleka tatizo la gari lakini unakuta kiongozi mwingine anasema hiyo gari irudi barabarani hivi mnategemea kweli hiko chombo kitakuwa imara huko barabarani?

Mradi unapesa nyingi sana ni bora kwenda kujifunza kwa watu binafsi wanavyoendesha makampuni yao ya usafirishaji miaka na miaka, vizazi kwa vizazi kampuni hazitetereki zipo tuu.

Hii badili badili bado hawajapata mtu sahihi angalau kwa marehemu David Mgwasa kulikuwa na nafuu na baada ya kuona huko baadae kutaleta shida kutokana na aina ya uendeshaji uliokuwa unaelekea akakaa pembeni.
 
DART ni mmiliki na msimamizi wa miundombinu ya mwendo kasi na UDART ni kampuni ambayo inamiliki mabasi ya mwendokasi na kuendesha Biashara ya usafirishaji kwenye miundombinu ya DART.

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…