Nimesikitishwa, huzunishwa na kufadhaishwa na uongo wa Kamati ya PAC! Escrow sio fedha za umma!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,

Kwa waliosoma fasihi, kitabu cha "An Enemy of the People" by Henrik Ibsen mnaweza kuniita mimi Paskali kuwa ni "an enemy of the people!", Ibsen anasema, the strongest man on earth is the man who can stand alone!", hivyo na mimi, katika jambo ambalo nina uhakika nalo na ninaamini ni ukweli, nitasimama nalo, hata kama nitabaki peke yangu!.

Fedha za Escrow, Sio Fedha za Umma!, hizo Bilioni 320 zilizokuwa kwenye account ya Escrow, hazijaibiwa!, bali zimetumika kulipia umeme! kwa kumlipa mfua umeme, IPTL, hivyo sio fedha za umma!

Inawezekana PAP ni matapeli, na amenunua IPTL kitapeli, hivyo IPTL chini ya PAP ni kampuni ya kitapeli, Singasinga amefanya utapeli kuinunua IPTL kitapeli, toka kwa wamiliki halali, that is pure business hayatuhusu, bali malipo ya Tanesco kwenye account ya escrow ni kulipia capacity charges ya mitambo ya IPTL ambayo ni mitambo kweli sio mitambo hewa!, na pia Tanesco inalipia malipo ya huduma za umeme ambao sio umeme hewa, bali ni umeme kweli unaokuwa generated na mitambo ya IPTL, na imeelezwa kuwa Tanesco bado inadaiwa!. Kwa lugha rahisi, hata baada ya PAP kulipwa fedha zote zilizoko ndani ya escrow account, bado Tanesco inadaiwa!.

Ukiwa mkweli sana wa type ya ukweli huu, pia lazima uwe tayari to pay the price!. Mimi ni mkweli wa kihivi, niko tayari to pay the price of expressing my opinion and I have always been paying the price kwa kuusema ukweli mchungu, hivyo na sasa nasema tena ukweli mchungu mwingine kuwa Nimesikitishwa!, Huzunishwa!, na Kufadhaishwa na Uongo wa Kamati ya PAC!-Escrow Sio Fedha za Umma!.

Kwenye issue hii ya fedha za Escrow kama ni za umma au la, the authority ni ofisi ya GAG na Ripoti ya CAG ndio wakweli, Fedha za Escrow sio fedha za umma!

Paskali

Ufafanuzi unapatikana hapa kwa Mkuu Ng'wamapalala.


Hoja za Kamati ya PAC zinavyokinzana kuhusu Escrow akaunti kama ni fedha ya umma


Mkuu Mwalimu, Prof. Kitila Mkumbo, kwanza hongera kupata uprofesa, maana hatujakutana humu jukwaani kwenye thread yangu yoyote tangu umekuwa prof, bado nimekuzoea zaidi kama Dr. Kitila Mkumbo hivyo nimefarijika sana, kunitembelea kwenye uzi huu, it's an honor to me and to my thread, kama nilivyofarijika nilipo tembelewa na Wakuu Mchambuzi na Nguruvi 3.

Kwenye posti yako ume raise hoja 12 za msingi, mwanafunzi unapoulizwa maswali na mwalimu, unaamini kabisa mwalimu anajua, ila anakuuliza tuu ili kukupima ufahamu wako, inapotokea mwalimu anaomba kueleweshwa na mwanafunzi, then mwanafunzi huyo anakuwa more than glad kumuelewesha mwalimu wake, na hapa mwanafunzi atajisikia sasa yeye mwanafunzi ndio mwalimu, na mwalimu ndio amegeuka mwanafunzi wake, hivyo mwanafunzi wangu, Mwalimu Kitila, karibu katika darasa langu utulie kama mwanafunzi wangu kwa jinsi ile tunavyotulia kwenye darasa lako.
  1. Mimi ni mkweli daima hivyo mara kadhaa huanzia kwa kuweka "the end" na kisha ndipo na "justify the means". The end product hapa "pesa za escrow ni za nani?", naanza kwenye kumtaja mwenye pesa ndipo tuje kuhalalisha kwa nini sio pesa za umma!. Pesa za Escrow sio fedha za umma . Kuna hoja za mijadala, na kuna hoja sio za mijadala ni straight forward, final na conclusive!. Ingekuwa hoja yangu ni mjadala, ningeuliza "Jee Fedha za Escrow ni za Umma?", ili watu walete michango, mwisho tufikie hitimisho kama ni fedha za umma au laa!. Hapa kuna ukweli na uongo!, kuna kuaminishana uongo kwa kudanganyana kuwa fedha za umma zimeibiwa!, zimechotwa, zimekapuliwa, hivyo wananchi wamehamanika, kuwa wanaibiwa, sasa ukichanganya na huu umasikini uliotopea, wananchi wanaposikia wameibiwa, wanakuwa na hasira sana, ingekuwa Rugemalila anaishi uswazi, huyu ni dumu la mafuta na kibiriti kitambo!, wakati ukweli wenyewe halisi ni kuwa fedha hazikuibiwa bali zimelipwa!. Mtindo wangu wa kutoa hitimisho final and conclusive sikuanza leo, tulipoanza tuu huu mchakato wa katiba, nilisema tutapata "bora katiba". Kabla kura hazijapigwa kuipitisha nilisema humu "kura zisipotosha, zitatosheshwa!". Sasa watu wanapigia chapuo kura za hapana, nikasema wazi huko ni kujifurahisha kwa sababu kura za ndio "zitatosheshwa!", na kwenye siasa pia mara kibao nimeweka conclusive remarks humu hata "2015 ni CCM tena!" kwa sababu hatuna any serious opposition, Ukawa mimi nauita ni just a "married of convenience!", conveniences zikiisha kila mtu atashika njia yake!. Escrow sio fedha za umma!.
  2. Hapa tuko wote, ndani pesa za account ya escrow zimechange forms mara tatu, au zime change hands mara tatu, kutoka fedha za umma, fedha za wote, fedha binafsi. Kuna mtu anaitwa depositor, ambaye yeye ni Tanesco, fedha zilipokuwa mikononi mwa Tanesco, ndio zilikuwa fedha za umma, kitendo cha Tanesco kuzitoa ndani ya account ya Tanesco kuzi deposit kwenye escrow account, kumezichange form hizi fedha from kuwa pesa za umma, into pesa za depository, ambaye yeye ni custodian tuu wa fedha hizo hadi mgogoro utakapokwisha!, hivyo wakati fedha zikiwa kwenye safe custody ya custodian, escrow account chini ya BOT, fedha zile sii za umma wala sii za binafsi, some zingeweza kuwa za umma na kurudishwa Tanesco, some zingeweza kuwa za IPTL with a unique options ya possibility with "uncertainties" that "only some" "could" be fedha za umma, za Tanesco's, kutokana na overcharging, but with definite certainty that some are IPTL's with possibility ya all the money ni za IPTL!. Ukijua ni nini kilichotokea kuhusu madai ya Tanesco na ni nini kilikubalika?!. Tanesco wali give in, na kukubali wanadaiwa more than kiwango kilichopo ndani ya escrow account, that na wakaweka schedule of repayment na ndipo Tanesco waka authorize pesa zote zilipwe kwa IPTL!, and that is when all the money zili change form kutoka kuwa fedha za wote na kugeuka fedha za binafsi, and during withdrawal by the time fedha za Escrow zinalipwa IPTL zilikuwa tayari zime change hands, sio fedha za umma!.
  3. Ni kweli Tanesco ilikuwa overcharged hugely hivyo tulikuwa tunaibiwa!, ila wizi wenyewe ni kwa mujibu wa mkataba na tulikubali, kama tulivyokubali kununua radar, ndege ya rais, vifaa vya kijeshi na sasa bomba la gesi na mikataba ya gesi, tunaibiwa kwa kupenda kupitia mikataba mibovu, nenda kanisome hapa Gesi asili: Is it "day light robbery?!"- watanzania tunaibiwa ...Tetesi: Bomba la Gesi Mtwara:A "20 -Year Grace Period" ni Kiini Macho!. Hivyo kama ni kuwa overcharged, kila siku tunakuwa overcharged, overpriced, na huge kick backs!.
  4. Nashukuru kuwa kumbe unajua tulipewa hii nafasi jee unajua tuliitumiaje?!. Hii ndio conversion process ya kuachia fedha za umma zilizoibiwa na kugeuka fedha binafsi!.
  5. Hatukushindwa!, this is where the deal is!, PCCB ni nothing!, Hosea is nothing!, kitu kinachoitwa usalama wa Taifa is nothing!, tangu mwanzo IPTL ni rushwa mwanzo mwisho, what did we do?!. Bodi ya Tanesco ilipata "ganzi!" ya ajabu!, wakaridhia kwa maandishi pesa zote ni za IPTL!. Ruge na Singasinga ni wapiga dili, kama pesa zilikuwa zetu, then kikulacho kii nguoni mwetu!, tusitafute mchawi!, wala tusimbebeshe msalaba mtoto wa Mkulima, wezi wetu tunawajua na ni wale wale toka Richmond, Dowans hadi Simbioni!. Tungekuwa na akili laiti mgelijua huyo Simba mwenye 50% ya PAP ndipo angalau mngenielewa!.
  6. "Mwenye kisu kikali ndiye anaekula nyama!", "fimbo iliyoko mkononi ndiyo uiwayo nyoka!", "the end justify the means!", "Aliyeshika usukani wa gari ndiye dereva" regardless gari ni la nani!, hivyo as long as pesa iko mikononi mwa JR as private money, what he does with his monies!, is none of our businesses!. Private money is none of our business!.
  7. Kumbe sasa tatizo ni kugawa?!, Ukimuondoa Bakhresa, please don't talk of Mengi and Rostam, kwao this is "missed opportunity!", masikini JR angejivutia na kujinyamazia kimya, haya yote yasinge fumka!. Siku zote wenzetu wahindi huwa wanapiga dili hizi na kujituliza tuli!, lakini masikini wakipata.... Kuna DCP walipiga wahindi watupu wakatulia haikubumburuka!, EPA wahindi walikuwa wanaipiga long time, huku wametulia, Waswahili walipoingia tuu, wanasafiri 1st class, wananunua Vogue custom made kutoka UK, wanasafirisha kwa air cargo, gari zinafika zina kuwa cleared by cash on the spot!, mtaani mbona tulikomaje?!, si ndio dili ikabumbuluka!, wangejinyamazia tuu kama walivyo wahindi yote haya yasingetokea!.
  8. As long as sio hela ya umma, haijalishi nani amegaiwa na kwa huduma gani, ndio maana nikasema PCCB is nothing!, mnaangalia waliogaiwa pesa, haya ni matokeo tuu!, mnaacha kuangalia chanzo cha jinamizi hili la IPTL na kila kitu kiko wazi!, Rutabanzibwa alikataa hongo ya dola laki mbili na akahamishwa!, unamjua waziri wake alikuwa nani?, kama KM alimegewa dola laki mbili, jee aliyekuwa waziri alipewa ngapi?, unamjua ni nani?. Pesa zikiisha kuwa zako, you are free kuzigawa utakavyo bila kuvunja sheria yoyote!. Hakuna sheria inayokataza kugawa pesa wala jinai yoyote kupokea pesa yoyote kwa kazi yoyote au hata bila kazi yoyote!. Hata mimi kuna wakati "huwapitia wale" na kukubaliana bei, then nikifika huko, ninachange mind, lakini bado nalipa mtu bila kufanya chochote, its my money!.
  9. When the money is yours, you are free to use it as you please!, kwa wingine, umasikini ni laana, hivyo badala ya kuwagawia maskini unamuomba Mungu, maskini wote bora wajifie tuu na umasikini wao, na kumfuatilishia Mungu kuwa mwenye nacho, ataongezewa!, asiye nacho atanyang'anywa hata kidogo alichonacho!, mzee wa vijisenti, kapewa katiba, ndiye mwenyekiti wa kamati ya bajeji na ndie mshauri wa JR wa mambo ya kisheria na umeona consultancy fee yake!.
  10. Yes ni sawa kabisa na amini usiamini, hata mimi Paskali nikiwa nazo, huwa nagawa!, tofauti ni kiwango, kwa uwezo wangu huwa nagawa ten ten, jelo jelo hadi buku buku!, kila nikienda bush, nahakikisha nina kama just 1.M tangu bank naiomba in small denominations, nikitua bush!, kijiji kizima kinajua leo mtoto wa mama fulani ameingia kijijini, kuanzia pombe hadi hizo ten ten, jero jero na buku buku, its my money, I do with them whatever I wish to please myself!. Kwenye ule mgao kuna kick backs, kuna asante, kuna just sadakalawe kuwa "ninazo" kuna genuine charity na kuna sadaka!.
  11. Sio nchi za wenzetu hata sisi tunayo FIU pale BOT, miamala yote ya more than 10.m lazima taarifa ziende FIU ndio maana siku hizi hakuna kutoa malipo more than that bila kupitia BOT, the only exception ni same bank transactions ndio maana recipients wote walilazimishwa lazima wafungue account the same bank!. Nawaombeni sana msibabaishwe na huto tujisenti kwenye account za Mkombozi, the real transactions zimefanywa kwenye account yake iliyoko nchi Uholanzi, naamini "wanene" wamepewa asante zao zimehifadhiwa kule "Credit Suisse" transactions zinafanywa kwa "codes" only!, hata bank manager, hawezi kujua jina la account holders!.
Natumaini mwalimu utakuwa umenielewa!.

Ni wako mwanafunzi mtiifu
Paskali
 
Kama si za umma kwanini mwanasheria mkuu wa serikali-werema ndiye alikuwa akitoa maelekezo hadi kwa gaavana nduru na zaidi ya yote alihitaji hata maamuzi ya rais ili hizo pesa zitoke,

hizo pesa za tanesco zilipowekwa katika account zilikuwa za nani? Tanesco wanatengeneza pesa?

Pesa binafsi raisi anaingiaje, au pinda anaingiaje mkuu? hadi ahusike kukopiwa barua??
 
pasco,

kwa mtazamo wako, nini maana ya "fedha za umma".

kaka umemaliza kabisa!

Hayo ndiyo maswali niliyomuuliza hapo juu post 3, pasco nini maana ya fedha za umma, ndio maana nimemuuliza tanesco wanatengeneza pesa?

nchii hii tutaendelea kuwa maskini mpaka siku ya mwisho;

PASCO UMENISIKITISHA SANAAAA..
 
Pasco wa JF
Hata Pilato alimuuliza YESU "Ukweli ni Kitu Gani"..Yesu alikaa kimya. Maana yake ni kuwa,Ukweli na Uongo its a subjective. Hivyo Wewe Pasco endelea kuamini Ukweli wako.
Hongera.
 
Last edited by a moderator:
Pasco,
Labda unamaanisha siyo za "UMMA" kwa maana ya kuwa hakuna nchi au Taifa linaloitwa "UMMA" Na badala yake unataka waseme ni pesa za "WATANZANIA"?

Pasco hata kodi iliyopaswa kulipwa (Kodi ya ongezeko la mtaji na kodi zingine) kweli siyo za "UMMA"?
 
NCHII HII SIJUI TUMEKUWAJE JAMANI, YAANI PESA ZA TANESCO ZINAZOTOKANANA NA MAKUSANYO YA KODI ZETU SIYO ZETU TENA??

PESA ZA MTU BINAFSI WAZIRI MKUU, RAISI, WAZIRI WA FEDHA et al ANAJULISHWA ILI IWEJE??
 
Hujui kweli au unafanya kusudi kwa maslahi yako binafsi? akili yangu haitaki kuamini kwa kiwango cha ujuvi wako Ujiaminishe eti Escrow sio pesa za Umma....Sasa naanza kuamini kweli na wewe ni miongoni mwao wale waitwao wachumia tumbo...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…