Nimesikitishwa, huzunishwa na kufadhaishwa na uongo wa Kamati ya PAC! Escrow sio fedha za umma!

Nimesikitishwa, huzunishwa na kufadhaishwa na uongo wa Kamati ya PAC! Escrow sio fedha za umma!

Kwa mliosikia JK jana, jee bado mnaamini escrow zilikuwa ni fedha za umma?!.

Sisi Watanzani ni mijitu mijinga ajabu!, kosa la Tibaijuka sio kupokea pesa bali ni kitendo cha kujulikana alipokea pesa!.

Hili lidudu IPTL linajulikana fika tangu lilipoanza ni kwa rushwa mwanzo mwisho!. Wakati linafanyiwa lobbying, aliyekuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Patrick Rutabanzibwa, aligoma kupokea rushwa, akaletewa bulungutu la minoti mpaka nyumbani kwake, kwa vile tangu mwanzo alikataa, this time wakamtaim katoka, 'Mzee wa Kazi' akabisha hodi, house boy akafungua, akakabidhiwa mzigo siku ya 24 December, kesho yake ni Krismas!. Ujumbe huo ukaletwa kama 'zawadi' ya Krismas, ukaambatanishwa na kadi ya Krismas!, na kusainiwa na Bwana Mtoa Sadaka!", akitegemea demand za sikukuu na muambo wa January, lazima atashukuru!. Rutabanzibwa aliporudi nyumbani akakabidhiwa zigo lile!.

Kwa jinsi ile ile alivyokabidhiwa, tarehe 27, akalibeba zigo lile vile vile lilivyo na kulirudisha kwa 'mwenyewe". TISS walijua kila kitu, TAKUKURU walijua kila kitu, serikali ilijua kila kitu, they were all well taken care off, why only Tibaijuka?!.

Aliyekuwa Mkuu wa nchi alipokea ile zawadi ya Krismasi, Waziri wake pia alipokea!. 'Mtoa Zawadi' akawaarifu 'wakubwa", Rutabanzibwa alikataa zadi na kuirudisha, na yeye ndiye kikwazo pekee anayekwamisha 'mradi!', huwezi amini kilichotokea!, Rutabanzibwa aliondolewa, na mradi ukapitishwa!. Jee mnamjua waziri wake ilikuwa nani?!.

Nasema Watanzani ni mijitu mijinga, tunapigia kelele tujisenti twa escrow, ambayo sio chanzo ni matokeo tuu!, malipo hayo ya IPTL ynayobishaniwa ni kiwango cha capacity charges tuu, mkumbuke IPTL bado inameza mabilioni kadhaa ya utility kila siku iendayo kwa Mungu!, nobody cares!.

Turudi kwenye mgao wa Escrow, PAP amegawa 'sadaka' kubwa kubwa nene nene, kwa 'wanene' kupitia Stabic Bank, kwa vile majina hayajatajwa, then its ok!. JR amegawa sadaka kubwa kubwa nene nene, kwa 'wanene' kupitia account yake iliyoko Uholanzi, majina yapo na viwango vipo, na wanajulikana!, ila kwa vile hawajatajwa, Watanzania mazuzu tunashangilia Tibaijuka amewajibishwa!.

Nahisi sio wengi wanaojua kuwa IPTL/PAP bado inaidai Tanesco nyingi kuliko fedha zote zilizokuwemo escrow!, na kwa vile bado IPTL inazalisha umeme, deni hilo linaongezeka siku hadi siku, na malipo yake yatafanyika direct kutoka Tanesco into IPTL/PAP kimya kimya!, and life goes on!, nobody cares!, watu wanashangilia ujinga kwa kuangalia tulipoangukia baada ya kujikwaa, badala ya kuangalia tulipojikwaa!.

Pasco.
 
Kwa mliosikia JK jana, jee bado mnaamini escrow zilikuwa ni fedha za umma?!.

Sisi Watanzani ni mijitu mijinga ajabu!, kosa la Tibaijuka sio kupokea pesa bali ni kitendo cha kujulikana alipokea pesa!.

Hili lidudu IPTL linajulikana fika tangu lilipoanza ni kwa rushwa mwanzo mwisho!. Wakati linafanyiwa lobbying, aliyekuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Patrick Rutabanzibwa, aligoma kupokea rushwa, akaletewa bulungutu la minoti mpaka nyumbani kwake, kwa vile tangu mwanzo alikataa, this time wakamtaim katoka, 'Mzee wa Kazi' akabisha hodi, house boy akafungua, akakabidhiwa mzigo siku ya 24 December, kesho yake ni Krismas!. Ujumbe huo ukaletwa kama 'zawadi' ya Krismas, ukaambatanishwa na kadi ya Krismas!, na kusainiwa na Bwana Mtoa Sadaka!", akitegemea demand za sikukuu na muambo wa January, lazima atashukuru!. Rutabanzibwa aliporudi nyumbani akakabidhiwa zigo lile!.

Kwa jinsi ile ile alivyokabidhiwa, tarehe 27, akalibeba zigo lile vile vile lilivyo na kulirudisha kwa 'mwenyewe". TISS walijua kila kitu, TAKUKURU walijua kila kitu, serikali ilijua kila kitu, they were all well taken care off, why only Tibaijuka?!.

Aliyekuwa Mkuu wa nchi alipokea ile zawadi ya Krismasi, Waziri wake pia alipokea!. 'Mtoa Zawadi' akawaarifu 'wakubwa", Rutabanzibwa alikataa zadi na kuirudisha, na yeye ndiye kikwazo pekee anayekwamisha 'mradi!', huwezi amini kilichotokea!, Rutabanzibwa aliondolewa, na mradi ukapitishwa!. Jee mnamjua waziri wake ilikuwa nani?!.

Nasema Watanzani ni mijitu mijinga, tunapigia kelele tujisenti twa escrow, ambayo sio chanzo ni matokeo tuu!, malipo hayo ya IPTL ynayobishaniwa ni kiwango cha capacity charges tuu, mkumbuke IPTL bado inameza mabilioni kadhaa ya utility kila siku iendayo kwa Mungu!, nobody cares!.

Turudi kwenye mgao wa Escrow, PAP amegawa 'sadaka' kubwa kubwa nene nene, kwa 'wanene' kupitia Stabic Bank, kwa vile majina hayajatajwa, then its ok!. JR amegawa sadaka kubwa kubwa nene nene, kwa 'wanene' kupitia account yake iliyoko Uholanzi, majina yapo na viwango vipo, na wanajulikana!, ila kwa vile hawajatajwa, Watanzania mazuzu tunashangilia Tibaijuka amewajibishwa!.

Nahisi sio wengi wanaojua kuwa IPTL/PAP bado inaidai Tanesco nyingi kuliko fedha zote zilizokuwemo escrow!, na kwa vile bado IPTL inazalisha umeme, deni hilo linaongezeka siku hadi siku, na malipo yake yatafanyika direct kutoka Tanesco into IPTL/PAP kimya kimya!, and life goes on!, nobody cares!, watu wanashangilia ujinga kwa kuangalia tulipoangukia baada ya kujikwaa, badala ya kuangalia tulipojikwaa!.

Pasco.

Hii ya Rutabanzibwa imenifurahisha sana kwamba angalau tulikuwa na Wazalendo wa kweli wa nchi hii!.

Leo aliyekuwa Waziri wa Rutabanzibwa ndiye Raisi wa nchi hii, kwa maana kwamba wakati IPTL inaingia nchi hii huyu ambaye ni raisi wa nchi hii kwa sasa kwa ndiye aliyekuwa Waziri mwenye dhamana na Nishati!

Tukifuata haki bin haki bila kumuonea yeyote kama alivyosema yeye mwenyewe Raisi katika hotuba yake ya jana bila shaka na yeye anafaa kuchunguzwa tangu wakati ule alipokuwa na dhamana na Wizara ya Nishati, mpaka leo hii ambapo yeye ni Raisi wa nchi ambapo IPTL wanalipwa mabilioni ya pesa za Escrow.

Hawa akina Tibaijuka japo nao wanastahili adhabu, lakini ni Bangusilo Tu, mzizi wa Tatizo uko toka wakati ule IPTL inaingia nchini.
 
Kubwa ninaloliona hapa ni maandalizi ya kipigo kingine kutoka IPTL. Kuna haja ya kuichimba zaidi hiii kampuni maana in mikono michafu ya watanzania. Kwa kupitia malipo ya mkombozi utagundua harufu mbaya sana ya serekali kumilikiwa na matajiri IPTL ambao watu kivuli wapo ofisi za IPTL na wale halisi wapo kwenye hizi wizara zetu.Raisi kaahidi watatumia gesi na watauza umeme kwa bei ya chini kuliko wenzao. Nilistuka sana kwamba hawa watatuuzia kwa bei ya chini kwa nia gani?Kwamba fedha tuliyolipa escrow acc ilikuwa pungufu na pana 2% kwa kila mwezi kwa hayo mapungufu. Kwa hiyo jamaa wanatudai zaidi ya bilioni mia moja. Hatujui pia kwa sababu ipi TANESCO hawakuwa wakipeleka hizo fedha kwenye hiyo account na je ilikuwa kweli hayo mafungu ya kupeleka kila mwezi yalikuwa hayatoki TANESCO?au yalitoka yakazamishwa?Je serekali nayo ilikuwa ikiweka fedha huko escrow kwa makubaliano gani na taneso? na kwa nini isiwape tanesco walipe wenyewe huko escrow. je katika hizi ambazo hazikulipwa escrow nani mwenye jukumu la kulipa? ni tanesco au serekali? Raisi anasema kwa muamala huuu wa escrow kufanyika sisi tumepata faida maana tulikuwa tunadaiwa tuwekane sawa NI KIPENGELE GANI HICHO KINACHOONESHA IPTL kusamehe/(waver) ya hayo madai? Je ukikokotoa mapunguzo ya gharama za capacity charge kwa mujibu ya amri ya mahakama ya usuluhishi wa mikataba ya kimataifa ukizingatia pia 2% .nilitaraji raisi angalikuja na kiwango halisi IPTL ilichokuwa inadai baada ya mahesabu yote kufanyika nadhani haikuwa hesabu ya kutisha kiasi hicho. Kikubwa hapa bwana Zitto na kamati yake lazma waje na uchunguzi mpya japo nyoka kafurumushwa ingawa kasevu tusiache shimo lake bila kulimwagia sumu. Mimi kama mzalendo nikipita pale IPTL huwa natamani waandmanaji wenye hasira wakaupige mawe ule mtambo kwa zamu kwa siku nzima upondekepondeke . Kwani ni lazima tununue IPTL ?TUUMIE KWA MUDA TUJITOE KWENYE HUU MNYORORO.Hata kama hatutataifisha kwa kukiuka taratibu za kimataifa za usajili wa makampuni kwa nia ovu tuna uwezo wa kusitisha mahusiano na IPTL maana huu ni mrija.Wanatunyonya huku wakidai wana tusaidia.Ndugu wazalendo kina kaka Zitto hebu mutuletee sample ya mwaka mmoja au miwili mutuoneshe ni kiwango gani cha fedha katika mwaka husika cha capacity charge kililipwa bila Tanesco kuzalisha umeme . Hiki kipengele kinawanufaisha sana tanesco kuliko hata umeme wanaouza. Kuna uwezekano mkubwa kuwa tanesco isipozalisha umeme faida ni kubwa kuliko wakizalisha ndo maana vipindi flani walikuwa wanasingizia mitambo .waliweza kukaa kimya kwa maana bado kulikuwa na fedha inayoingia. Serekali ikae na Rugemalila maana kinachoonekana uwepo wa regemalila IPTL uliweka mambo hadharani hivyo imebidi hisa zake zinunuliwe inawezekana kwa bei ya juu sana alimradi asiwepo humo ndani ya hiyo network. Rugemalila ana siri nzito sana jinsi nchi hii inavyoliwa ila kwa kuwa waliwaji wenyewe wanapenda kuliwa akaona bora apige kupitia singasinga asepe. Singasinga anatarajia kuja kwa kasi ya ajabu . Hizo alizowalipa watu Stanbic na hizo alizomlipa rege( hapo ni malipo ya hisa pamoja na kifunga mdomo).Bwana Zitto na Kafulila haya mambo bado yapo kumina nane zetu. Kipigo kijacho kitakuwa kikubwa sana ni mtani jembe---------------
 
This Escrow saga will never go away in peace without Kikwete,I've said it so shall it be,Kikwete will never get away with this.Atleast he won't die in peace without this saga coming back to haunt him.
 
Kubwa ninaloliona hapa ni maandalizi ya kipigo kingine kutoka IPTL. Kuna haja ya kuichimba zaidi hiii kampuni maana in mikono michafu ya Tanzania. Kwa kupitia malipo ya mkombozi utagundua harufu mbaya sana ya serekali kumilikiwa na matajiri IPTL ambao watu kivuli wapo ofisi za IPTL na wale halisi wapo kwenye hizi wizara zetu.

Raisi kaahidi watatumia gesi na watauza umeme kwa bei ya chini kuliko wenzao. Nilistuka sana kwamba hawa watatuuzia kwa bei ya chini kwa nia gani? Kwamba fedha tuliyolipa escrow acc ilikuwa pungufu na pana 2% kwa kila mwezi kwa hayo mapungufu. Kwa hiyo jamaa wanatudai zaidi ya bilioni mia moja.

Hatujui pia kwa sababu ipi TANESCO hawakuwa wakipeleka hizo fedha kwenye hiyo account na je ilikuwa kweli hayo mafungu ya kupeleka kila mwezi yalikuwa hayatoki TANESCO? au yalitoka yakazamishwa?. Je serekali nayo ilikuwa ikiweka fedha huko escrow kwa makubaliano gani na Tanesco?, na kwa nini isiwape tanesco walipe wenyewe huko escrow?!.

Je katika hizi ambazo hazikulipwa escrow nani mwenye jukumu la kulipa? ni Tanesco au serekali? Raisi anasema kwa muamala huu wa escrow kufanyika sisi tumepata faida maana tulikuwa tunadaiwa tuwekane sawa NI KIPENGELE GANI HICHO KINACHOONESHA IPTL kusamehe/(waver) ya hayo madai? Je ukikokotoa mapunguzo ya gharama za capacity charge kwa mujibu ya amri ya mahakama ya usuluhishi wa mikataba ya kimataifa ukizingatia pia 2%, nilitaraji raisi angalikuja na kiwango halisi IPTL ilichokuwa inadai baada ya mahesabu yote kufanyika nadhani haikuwa hesabu ya kutisha kiasi hicho.

Kikubwa hapa bwana Zitto na kamati yake lazma waje na uchunguzi mpya japo nyoka kafurumushwa ingawa kasevu tusiache shimo lake bila kulimwagia sumu. Mimi kama mzalendo nikipita pale IPTL huwa natamani waandamanaji wenye hasira wakaupige mawe ule mtambo kwa zamu kwa siku nzima upondekepondeke .

Kwani ni lazima tununue IPTL ?TUUMIE KWA MUDA TUJITOE KWENYE HUU MNYORORO.Hata kama hatutataifisha kwa kukiuka taratibu za kimataifa za usajili wa makampuni kwa nia ovu tuna uwezo wa kusitisha mahusiano na IPTL maana huu ni mrija.Wanatunyonya huku wakidai wana tusaidia.

Ndugu wazalendo kina kaka Zitto hebu mutuletee sample ya mwaka mmoja au miwili mutuoneshe ni kiwango gani cha fedha katika mwaka husika cha capacity charge kililipwa bila Tanesco kuzalisha umeme . Hiki kipengele kinawanufaisha sana tanesco kuliko hata umeme wanaouza. Kuna uwezekano mkubwa kuwa tanesco isipozalisha umeme faida ni kubwa kuliko wakizalisha ndo maana vipindi flani walikuwa wanasingizia mitambo .waliweza kukaa kimya kwa maana bado kulikuwa na fedha inayoingia.

Serekali ikae na Rugemalila maana kinachoonekana uwepo wa regemalila IPTL uliweka mambo hadharani hivyo imebidi hisa zake zinunuliwe inawezekana kwa bei ya juu sana alimradi asiwepo humo ndani ya hiyo network. Rugemalila ana siri nzito sana jinsi nchi hii inavyoliwa ila kwa kuwa waliwaji wenyewe wanapenda kuliwa akaona bora apige kupitia singasinga asepe. Singasinga anatarajia kuja kwa kasi ya ajabu . Hizo alizowalipa watu Stanbic na hizo alizomlipa rege( hapo ni malipo ya hisa pamoja na kifunga mdomo).Bwana Zitto na Kafulila haya mambo bado yapo kumina nane zetu. Kipigo kijacho kitakuwa kikubwa sana ni mtani jembe---------------
.............
 
Are you serious or joking?
Wanabodi,

Kwa waliosoma fasihi, kitabu cha "An Enemy of the People" by Henrik Ibsen mnaweza kuniita mimi Pasco wa JF, kuwa ni "an enemy of the people!", Fedha za Escrow, Sio Fedha za Umma!, hizo Bilioni 320 zilizokuwa kwenye account ya Escrow, hazijaibiwa!, bali zimetumika kulipia umeme!.

Inawezekana PAP amenunua kampuni hewa, amefanya utapeli kuinunua IPTL toka kwa wamiliki halali, hayo hayatuhusu, bali malipo ya Tanesco kwenye account ya escrow ni kulipia capacity charges ya mitambo ya IPTL ambayo ni mitambo kweli sio mitambo hewa!, na pia Tanesco inalipia malipo ya huduma za umeme kweli unaokuwa genereted na mitambo ya IPTL, ni umeme kweli na sio umeme hewa!, na imeelezwa kuwa Tanesco bado inadaiwa!.

Ukiwa mkweli sana wa type ya ukweli huu, pia lazima uwe tayari to pay the price!.

Niko tayari to pay the price of expresing my opinion kuwa Nimesikitishwa!, Huzunishwa!, na Kufadhaishwa na Uongo wa Kamati ya PAC!-Escrow Sio Fedha za Umma!.

Pasco.

Ufafanuzi unapatikana hapa kwa Mkuu Ng'wamapalala.
Hoja za Kamati ya PAC zinavyokinzana kuhusu Escrow akaunti kama ni fedha ya umma

[/LIST]
Mkuu Mwalimu, Prof. Kitila, kwanza hongera kupata uprofesa, maana hatujakutana humu jukwaani kwenye thread yangu yoyote tangu umekuwa prof, bado nimekuzoea zaidi kama Dr. Pili nimefarijika sana, kunitembelea kwenye uzi huu, its an honour to me and to my thread, kama nilivyofarijika nilipo tembelewa na Mchambuzi na Nguruvi 3.

Kwenye posti yako ume raise hoja 12 za msingi, mwanafunzi unapoulizwa maswali na mwalimu, unaamini kabisa mwalimu anajua, ila anakuuliza tuu ili kuujua ufahamu wako, inapotokea mwalimu anaomba kueleweshwa na mwanafunzi, then mwanafunzi huyo anakuwa more than gladi kumuelewesha mwalimu, na hapa mwanafunzi atajisikia sasa yeye ndio mwalimu, na mwalimu ndio mwanafunzi wake, hivyo Mwalimu Kitila, karibu katika darasa langu.

  1. Mimi ni mkweli daima hivyo mara kadhaa huanzia kwa kuweka "the end" na kisha ndipo na "justify the means". The end product hapa "pesa ni za nani?!", naanza kwenye kumtaja mwenye pesa ndipo tuje kuhalalisha kwa nini sio pesa za umma!. Kuna hoja za mijadala, na kuna hoja sio za mijadala ni straight conclusive!. Ingekuwa hoja yangu ni mjadala, ningeiliza Jee Fedha za Escrow ni za Umma?, ili watu walete michango, mwisho tufikie hitimisho!. Hapa kuna ukweli na uongo!, kuna kumaninishana kwa kudanganyana kuwa fedha za umma zimeibiwa!, zimechotwa, zimekapuliwa, hivyo wananchi wamehaminika, wakati ukweli ni kuwa fedha hazikuibiwa zimelipwa!. Mtindo wangu wa kutoa conclusiwe sikuanza leo, tulupoanza tuu huu mchakato wa katiba, nilisema tutapata "bora katiba". Kabla kura hazijapigwa kuipitisha nilisema humu "kura zisipotosha, zitatosheshwa!". Sasa watu wanapigia chapuo kura za hapana, nikasema wazi huko ni kujifurahisha kwa sababu kura za ndio "zitatosheshwa!", na kwenye siasa pia mara kibao nimeweka conclusive humu hata "2015 ni CCM tena!" kwa sababu hatuna any serious opposition, Ukawa mimi nauita ni just a "married of convenience!", conveniences zikiisha kila mtu atashika njia yake!. Escrow sio fedha za umma!.
  2. Hapa tuko wote, ndani pesa za account ya escrow zimechange formas mara tatu, au zime change hands mara tatu, kuna mtu anaitwa depositor, ambaye yeye ni Tanesco, fedha zilipokuwa mikononi mwa Tanesco, ni fedha za umma, kitendo cha kuzitoa ndani ya account ya Tanesco kuzi deposit kwenye escrow, kitendo cha depositing, kumezichange form hizi fedha from kuwa pesa za umma, into pesa za depository, na zimechange hands from mikono ya Tanesco to mikono ya depositor ambaye yeye ni custodian tuu wa fedha hizo hadi mgogoro utakapokwisha!, hivyo wakati fedha zikiwa kwenye safe custody ya custodian, fedha zile sii za umma wala sii za binafsi, some zingeweza kuwa za umma na kurudishwa Tanesco, some zingeweza kuwa za IPTL with a unique options ya possibility with "uncertainty" that "only some" "could" be Tanesco's, but with definite that some are IPTL's with possibility ya all kuwa ni za IPTL!. Unakijua ni nini kilichotokea kuhusu madai ya Tanesco na ni nini kilikubalika?!. Tanesco wali give in, na kukubali wanadaiwa more than that na wakaweka schedule of repayment na ndipo Tanesco waka authorise pesa zote zilipwe kwa IPTL!, and that is when all the money zili change form kutoka kuwa fedha za wote na kugeuka fedha za binafsi, and during withdrawer by the time fedha zinalipwa IPTL zilikuwa sio fedha za umma!.
  3. Ni kweli Tanesco ilikuwa overcharged hugely hivyo tulikuwa tunaibiwa!, ila wizi wenyewe ni kwa mujibu wa mkataba na tulikubali, kama tulivyokubali kununua radar, ndege ya rais, vifaa vya kijeshi na sasa bomba la gesi na mikataba ya gesi, nenda kanisome hapa Gesi asili: Is it "day light robbery?!"- watanzania tunaibiwa ...Tetesi: Bomba la Gesi Mtwara:A "20 -Year Grace Period" ni Kiini Macho!. Hivyo kama ni kuwa overcharged, kila siku tunakuwa overcharged, overpriced, na huge kick backs!.
  4. Nashukuru kuwa kumbe unajua tulipewa hii nafasi jee unajua tuliitumiaje?!. Hii ndio conversion process ya kuachia fedha za umma zilizoibiwa na kugeuka fedha binafsi!.
  5. Hatukushindwa!, this is where the deal is!, PCCB ni nothing!, Hosea is nothing!, kitu kinachoitwa usalama wa Taifa is nothing!, tangu mwanzo IPTL ni rushwa mwanzo mwisho, what did we do?!. Bodi ya Tanesco ilipata "ganzi!" ya ajabu!, wakaridhia kwa maandishi pesa zote ni za IPTL!. Ruge na Singasinga ni wapiga dili, kama pesa zilikuwa zetu, then kikulacho kii nguoni mwetu!, tusitafute mchawi!, wala tusimbebeshe msalaba mtoto wa Mkulima, wezi wetu tunawajua na ni wale wale toka Richmond, Dowans hadi Simbioni!. Tungekuwa na akili laiti mgelijua huyo Simba mwenye 50% ya PAP ndipo angalau mngenielewa!.
  6. "Mwenye kisu kikali ndiye anaekula nyama!", "fimbo iliyoko mkononi ndiyo uiwayo nyoka!", "the end justify the means!", "Aliyeshika usukani wa gari ndiye dereva" regardless gari ni la nani!, hivyo as long as pesa iko mikononi mwa JR as private money, what he does with his monies!, is non of our businesses!.
  7. Private money is none of our business!.
  8. Kumbe sasa tatizo ni kugawa?!, Ukimuondoa Bakhresa, please don't talk of Mengi and Rostam, kwao this is "missed opportunity!", masking JR akajivutia na kujinyamazia, haya yote yasinge fumka!. Siku zote wahindi wanapiga dili hizi na kujituliza tuli!, lakini masikini wakipata.... Kuna DCP walipiga wahindi watupu wakatulia haikubumburuka!, EPA wahindi walikuwa wanaipiga long time, huku wametulia, Waswahili walipoingia tuu, wanasafiri 1st class, wananunua Vogue custom made kutoka UK, wanasafirisha kwa air cargo, gari zinafika zina kuwa cleared by cash on the spot!, mtaani mbona tulikomaje?!, si ndio dili ikabumbuluka!, wangejinyamazia tuu kama walivyo wahindi yote haya yasingetokea!.
  9. As long as sio hela ya umma, haijalishi nani amegaiwa na kwa huduma gani, ndio maana nikasema PCCB is nothing!, mnaangalia waliogaiwa pesa, haya ni matokeo tuu!, mnaacha kuangalia chanzo cha jinamizi hili la IPTL na kila kitu kiko wazi!, Rutabanzibwa alikataa hongo ya dola 200 na akahamishwa!, unamjua waziri wake alikuwa nani?, kama KM alimegewa dola laki mbili, jee aliyekuwa waziri alipewa ngapi?, unamjua ni nani?. Pesa zikiisha kuwa zako, you are free kuzigawa utakavyo bila kuvunja sheria yoyote!. Hakuna sheria inayokataza kugawa pesa wala jinai yoyote kupokea pesa yoyote kwa kazi yoyote au hata bila kazi yoyote!. Hata mimi kuna wakati "huwapitia wale" na kukubaliana bei, then nikifika huko, ninachange mind, lakini bado nalipa mtu bila kufanya chochote, its my money!.
  10. When the money is yours, you are free to use it as you please!, kwa winging umasikini ni laana, hivyo badala ya kuwagawia masking unamuomba Mungu, masking wore bora wajifie tuu na umasikini wao, na kumfutilishia Mungu kuwa mwenye nacho, ataongezewa!, asiye nacho atanyang'anywa hata kidogo alichonacho!, mzee wa vijisenti, kapewa katiba, ndiye mwenyekiti wa kamati ya bajeji na ndie mshauri wa JR wa mambo ya kisheria na umeona consultancy fee yake!.
  11. Yes ni saws kabisa na amini usiamini, hata mimi Pasco wa jf, nikiwa nazo, huwa nagawa!, tofauti ni kiwango, kwa uwezo wangu huwa nagawa ten ten, jelo jelo hadi buku buku!, kila nikienda bush, nahakikisha nina kama just 1.M tangu bank naiomba in small denominations, nikitua bush!, kijiji kizima kinajua leo mtoto wa mama fulani ameingia kijijini, kuanzia pombe hadi hizo ten ten, jeero jero na buku buku, its my money, I do with it what it pleases me!. Kwenye ule mgao kuna kick backs, kuna asante, kuna just sadakalawe kuwa "ninazo" kuna genuine charity na kuna sadaka!.
  12. Sio nchi za wenzetu hata sisi tunayo FIU pale BOT, miala yote ya more than 10.m lazima taarifa ziende FIU ndio maana siku hizi hakuna kutoa malipo more than that bila kupitia BOT, the only exception ni same bank transactions ndio maana recipients wote walilazimishwa lazima wafungue account the same bank!. Nawaombeni sana msibabaishwe na huto tujisenti kwenye account za Mkombozi, the real transactions zimefanywa kwenye account yake iliyoko nchi Uholanzi, naamini "wanene" wamepewa asante zao zimehifadhiwa kule "Credit Sussie" transactions zinafanywa kwa "codes" only!, hata bank manageger, hawezi kujua jina la account holders!.
Natumaini mwalimu utakuwa umenielewa!.

Ni wako mwanafunzi mtiifu
Pasco wa jf!.

 
Anatania tuu ili thread yake na yeye isomwe na kuchangiwa na watu wengi...umefanikiwa katika hilo kaka hongera Pasco
 
Just Joking!.
P.

Naona tulio wengi tuko chapter one inayojadili kama kuna wizi umefanyika escrow au la na nani awajibishwe. Tayari kuna majibu mengi na wengine tumeyakariri tu .Hoja yangu bwana pasco ipo capter two maelezo yako hajajibu kitu chapter two kwa kuwa umekuja na hadith ya chapter one. Kwa kifupi chapter two inazungumzia way foward kutokana na mambo ya IPTL kuzungukwa na wawingu tena mawingu yaliyosababishwa na mabomu na uchomaji matairi.Kinachopingwa hapa ni kuendelea na IPTL bila kuichunguza vya kutosha.Idea ya IPTL kujifanya ndio wasamaria kwetu hiyo nitaipinga siku zote.Hawa jamaa hawatuibii ila wanatunyonya kupitia vipengele vya mikataba .Bwana pasco ukiacha akili za kuambiwa hebu fikiri kampuni hailipwi direct ,fedha zinaenda escrow kwa miaka saba na inadunda tu ?Nona umechota paragraph kubwa tu ambayo haijibu hoja.Katika hoja zangu sijaona ubaya wa rugemalila kupata fedha na nimesifu namna alivofanya amechukua kwa singa ambaye mkataba wake ni mnono sana.Jana raisi kaomba IPTL wapunguze zaidi bei ya umeme unafikiri kwa nini? Anafahamu kuwa IPTL wanamkataba wenye superprofit.,hilo analijua wazi.Inawezekana sana tu kwamba malipo ya capacity charge yanaiwezesha IPTL kupata faida katika equilibrium price. IPTL inatumia mafuta diesel kujiendesha ,katika upatikanaji wa haya mafuta sifahamu vizuri kama tanesco ama serekali ina role gani katika kuhakikisha yanapatikana .Tunambiwa kuwa hao IPTL watatumia gesi kuzalishia hapo tena watakuwa na mwanya wao wa janjajanja kama hatutabagain nao. Kitu kinachonisikitisha ni pale tunapotumia neno kuomba watupunguzie badala ya kujadili"Japo serekali haichimbi gesi imewezesha gesi ichimbwe na lengo likiwa kupunguza bei ya nishati. Inabidi tuwe na wataalam watakaotathmini hiyo gesi itasaidia kupata punguzo la kiwango gani katika bei ya soko maana kwenye biashara kubwa namna hii hata sent hamsini ya kitanzania kwa wiki ni mamia ya mamilioni.Watu wasafi washiriki kujadili hili si lazima watoke tanesco na wizarani.Shirikisha wataalam wa uchumi,uwekezaji na finance,wanasheria kutoka vyuo vikuu na jambo hili liwe wazi.Narudia tena bwana Pasco kipigo kingine kinaandaliwa kikubwa zaidi ya hiki maana kuna marejesho ya hela seth alizotapanya.
 
Naona tulio wengi tuko chapter one inayojadili kama kuna wizi umefanyika escrow au la na nani awajibishwe. Tayari kuna majibu mengi na wengine tumeyakariri tu. Hoja yangu bwana pasco ipo capter two maelezo yako hajajibu kitu chapter two kwa kuwa umekuja na hadith ya chapter one.

Kwa kifupi chapter two inazungumzia way foward kutokana na mambo ya IPTL kuzungukwa na wawingu tena mawingu yaliyosababishwa na mabomu na uchomaji matairi. Kinachopingwa hapa ni kuendelea na IPTL bila kuichunguza vya kutosha. Idea ya IPTL kujifanya ndio wasamaria kwetu hiyo nitaipinga siku zote. Hawa jamaa hawatuibii ila wanatunyonya kupitia vipengele vya mikataba.

Bwana pasco ukiacha akili za kuambiwa hebu fikiri kampuni hailipwi direct ,fedha zinaenda escrow kwa miaka saba na inadunda tu?. Nona umechota paragraph kubwa tu ambayo haijibu hoja. Katika hoja zangu sijaona ubaya wa rugemalila kupata fedha na nimesifu namna alivofanya amechukua kwa singa ambaye mkataba wake ni mnono sana.

Jana raisi kaomba IPTL wapunguze zaidi bei ya umeme unafikiri kwa nini? Anafahamu kuwa IPTL wanamkataba wenye superprofit., hilo analijua wazi. Inawezekana sana tu kwamba malipo ya capacity charge yanaiwezesha IPTL kupata faida katika equilibrium price. IPTL inatumia mafuta diesel kujiendesha ,katika upatikanaji wa haya mafuta sifahamu vizuri kama tanesco ama serekali ina role gani katika kuhakikisha yanapatikana .

Tunambiwa kuwa hao IPTL watatumia gesi kuzalishia hapo tena watakuwa na mwanya wao wa janjajanja kama hatutabagain nao. Kitu kinachonisikitisha ni pale tunapotumia neno kuomba watupunguzie badala ya kujadili" Japo serekali haichimbi gesi imewezesha gesi ichimbwe na lengo likiwa kupunguza bei ya nishati.

Inabidi tuwe na wataalam watakaotathmini hiyo gesi itasaidia kupata punguzo la kiwango gani katika bei ya soko maana kwenye biashara kubwa namna hii hata sent hamsini ya kitanzania kwa wiki ni mamia ya mamilioni. Watu wasafi washiriki kujadili hili si lazima watoke tanesco na wizarani. Shirikisha wataalam wa uchumi, uwekezaji na finance,wanasheria kutoka vyuo vikuu na jambo hili liwe wazi. Narudia tena bwana Pasco kipigo kingine kinaandaliwa kikubwa zaidi ya hiki maana kuna marejesho ya hela seth alizotapanya.
Asante nimekuelewa.
Pasco
 
Mkuu Pasco u-mwandishi mwenye uweledi. Nachelea sana watanzania kinachotuponza ni siasa hata kwa mambo yasiyohitaji siasa. Kipengere namba 5 kilitosha kabisa kumaliza hizi hoja lakini safari ya Dar Mwanza badala ya kupita Dodoma tunapita Arusha - Nairobi ndiyo rufike Mwanza.

Ok pesa si za umma lakini mtiririko mzima umejaa rushwa. Sina muda ya kuzinguka hapa, ningekuwa na mamlaka kwanza Edward Hosea ningemuweka kizuizini kwa kushindwa kufanya kazi yake na kulisababishia taifa hasara.

Bodi ya tanesco iliyomaliza muda wote wangeshitakiwa kwa kulitia taifa hasara.

Viongozi wote wa umma waliopokea fedha toka kwa JR bila ku-declare conflict of interest kwa mujibu wa sheria ya maadili ya utumishi wa umma wote wangepigwa chini na kiasi walichopokea kutaifishwa.

Washauri wa Rais wote ningepiga chini maana hawana msaada, na kama walimshauri Rais naye akakataa kwa sababu azijuazo mwenyewe wangeomba kukaa pembeni kama wafanyavyo wenzetu wenye demokrasia ya wastani ili kulinda heshima zao.

Baada ya kumshughulikia Hosea najua ningepata na mengine mengi ambayo ningeendelea kuyafanyia kazi. Tofauti na hapo Tanzania hatuendi kokote na kwa style hii ya viongozi kuendelea kulindana ikifika mwaka 2025 Watanzania tutakuwa wapangaji ndani ya nchi yetu wenyewe
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom