Nimesikitishwa, huzunishwa na kufadhaishwa na uongo wa Kamati ya PAC! Escrow sio fedha za umma!

Kwa mliosikia JK jana, jee bado mnaamini escrow zilikuwa ni fedha za umma?!.

Sisi Watanzani ni mijitu mijinga ajabu!, kosa la Tibaijuka sio kupokea pesa bali ni kitendo cha kujulikana alipokea pesa!.

Hili lidudu IPTL linajulikana fika tangu lilipoanza ni kwa rushwa mwanzo mwisho!. Wakati linafanyiwa lobbying, aliyekuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Patrick Rutabanzibwa, aligoma kupokea rushwa, akaletewa bulungutu la minoti mpaka nyumbani kwake, kwa vile tangu mwanzo alikataa, this time wakamtaim katoka, 'Mzee wa Kazi' akabisha hodi, house boy akafungua, akakabidhiwa mzigo siku ya 24 December, kesho yake ni Krismas!. Ujumbe huo ukaletwa kama 'zawadi' ya Krismas, ukaambatanishwa na kadi ya Krismas!, na kusainiwa na Bwana Mtoa Sadaka!", akitegemea demand za sikukuu na muambo wa January, lazima atashukuru!. Rutabanzibwa aliporudi nyumbani akakabidhiwa zigo lile!.

Kwa jinsi ile ile alivyokabidhiwa, tarehe 27, akalibeba zigo lile vile vile lilivyo na kulirudisha kwa 'mwenyewe". TISS walijua kila kitu, TAKUKURU walijua kila kitu, serikali ilijua kila kitu, they were all well taken care off, why only Tibaijuka?!.

Aliyekuwa Mkuu wa nchi alipokea ile zawadi ya Krismasi, Waziri wake pia alipokea!. 'Mtoa Zawadi' akawaarifu 'wakubwa", Rutabanzibwa alikataa zadi na kuirudisha, na yeye ndiye kikwazo pekee anayekwamisha 'mradi!', huwezi amini kilichotokea!, Rutabanzibwa aliondolewa, na mradi ukapitishwa!. Jee mnamjua waziri wake ilikuwa nani?!.

Nasema Watanzani ni mijitu mijinga, tunapigia kelele tujisenti twa escrow, ambayo sio chanzo ni matokeo tuu!, malipo hayo ya IPTL ynayobishaniwa ni kiwango cha capacity charges tuu, mkumbuke IPTL bado inameza mabilioni kadhaa ya utility kila siku iendayo kwa Mungu!, nobody cares!.

Turudi kwenye mgao wa Escrow, PAP amegawa 'sadaka' kubwa kubwa nene nene, kwa 'wanene' kupitia Stabic Bank, kwa vile majina hayajatajwa, then its ok!. JR amegawa sadaka kubwa kubwa nene nene, kwa 'wanene' kupitia account yake iliyoko Uholanzi, majina yapo na viwango vipo, na wanajulikana!, ila kwa vile hawajatajwa, Watanzania mazuzu tunashangilia Tibaijuka amewajibishwa!.

Nahisi sio wengi wanaojua kuwa IPTL/PAP bado inaidai Tanesco nyingi kuliko fedha zote zilizokuwemo escrow!, na kwa vile bado IPTL inazalisha umeme, deni hilo linaongezeka siku hadi siku, na malipo yake yatafanyika direct kutoka Tanesco into IPTL/PAP kimya kimya!, and life goes on!, nobody cares!, watu wanashangilia ujinga kwa kuangalia tulipoangukia baada ya kujikwaa, badala ya kuangalia tulipojikwaa!.

Pasco.
 

Hii ya Rutabanzibwa imenifurahisha sana kwamba angalau tulikuwa na Wazalendo wa kweli wa nchi hii!.

Leo aliyekuwa Waziri wa Rutabanzibwa ndiye Raisi wa nchi hii, kwa maana kwamba wakati IPTL inaingia nchi hii huyu ambaye ni raisi wa nchi hii kwa sasa kwa ndiye aliyekuwa Waziri mwenye dhamana na Nishati!

Tukifuata haki bin haki bila kumuonea yeyote kama alivyosema yeye mwenyewe Raisi katika hotuba yake ya jana bila shaka na yeye anafaa kuchunguzwa tangu wakati ule alipokuwa na dhamana na Wizara ya Nishati, mpaka leo hii ambapo yeye ni Raisi wa nchi ambapo IPTL wanalipwa mabilioni ya pesa za Escrow.

Hawa akina Tibaijuka japo nao wanastahili adhabu, lakini ni Bangusilo Tu, mzizi wa Tatizo uko toka wakati ule IPTL inaingia nchini.
 
Kubwa ninaloliona hapa ni maandalizi ya kipigo kingine kutoka IPTL. Kuna haja ya kuichimba zaidi hiii kampuni maana in mikono michafu ya watanzania. Kwa kupitia malipo ya mkombozi utagundua harufu mbaya sana ya serekali kumilikiwa na matajiri IPTL ambao watu kivuli wapo ofisi za IPTL na wale halisi wapo kwenye hizi wizara zetu.Raisi kaahidi watatumia gesi na watauza umeme kwa bei ya chini kuliko wenzao. Nilistuka sana kwamba hawa watatuuzia kwa bei ya chini kwa nia gani?Kwamba fedha tuliyolipa escrow acc ilikuwa pungufu na pana 2% kwa kila mwezi kwa hayo mapungufu. Kwa hiyo jamaa wanatudai zaidi ya bilioni mia moja. Hatujui pia kwa sababu ipi TANESCO hawakuwa wakipeleka hizo fedha kwenye hiyo account na je ilikuwa kweli hayo mafungu ya kupeleka kila mwezi yalikuwa hayatoki TANESCO?au yalitoka yakazamishwa?Je serekali nayo ilikuwa ikiweka fedha huko escrow kwa makubaliano gani na taneso? na kwa nini isiwape tanesco walipe wenyewe huko escrow. je katika hizi ambazo hazikulipwa escrow nani mwenye jukumu la kulipa? ni tanesco au serekali? Raisi anasema kwa muamala huuu wa escrow kufanyika sisi tumepata faida maana tulikuwa tunadaiwa tuwekane sawa NI KIPENGELE GANI HICHO KINACHOONESHA IPTL kusamehe/(waver) ya hayo madai? Je ukikokotoa mapunguzo ya gharama za capacity charge kwa mujibu ya amri ya mahakama ya usuluhishi wa mikataba ya kimataifa ukizingatia pia 2% .nilitaraji raisi angalikuja na kiwango halisi IPTL ilichokuwa inadai baada ya mahesabu yote kufanyika nadhani haikuwa hesabu ya kutisha kiasi hicho. Kikubwa hapa bwana Zitto na kamati yake lazma waje na uchunguzi mpya japo nyoka kafurumushwa ingawa kasevu tusiache shimo lake bila kulimwagia sumu. Mimi kama mzalendo nikipita pale IPTL huwa natamani waandmanaji wenye hasira wakaupige mawe ule mtambo kwa zamu kwa siku nzima upondekepondeke . Kwani ni lazima tununue IPTL ?TUUMIE KWA MUDA TUJITOE KWENYE HUU MNYORORO.Hata kama hatutataifisha kwa kukiuka taratibu za kimataifa za usajili wa makampuni kwa nia ovu tuna uwezo wa kusitisha mahusiano na IPTL maana huu ni mrija.Wanatunyonya huku wakidai wana tusaidia.Ndugu wazalendo kina kaka Zitto hebu mutuletee sample ya mwaka mmoja au miwili mutuoneshe ni kiwango gani cha fedha katika mwaka husika cha capacity charge kililipwa bila Tanesco kuzalisha umeme . Hiki kipengele kinawanufaisha sana tanesco kuliko hata umeme wanaouza. Kuna uwezekano mkubwa kuwa tanesco isipozalisha umeme faida ni kubwa kuliko wakizalisha ndo maana vipindi flani walikuwa wanasingizia mitambo .waliweza kukaa kimya kwa maana bado kulikuwa na fedha inayoingia. Serekali ikae na Rugemalila maana kinachoonekana uwepo wa regemalila IPTL uliweka mambo hadharani hivyo imebidi hisa zake zinunuliwe inawezekana kwa bei ya juu sana alimradi asiwepo humo ndani ya hiyo network. Rugemalila ana siri nzito sana jinsi nchi hii inavyoliwa ila kwa kuwa waliwaji wenyewe wanapenda kuliwa akaona bora apige kupitia singasinga asepe. Singasinga anatarajia kuja kwa kasi ya ajabu . Hizo alizowalipa watu Stanbic na hizo alizomlipa rege( hapo ni malipo ya hisa pamoja na kifunga mdomo).Bwana Zitto na Kafulila haya mambo bado yapo kumina nane zetu. Kipigo kijacho kitakuwa kikubwa sana ni mtani jembe---------------
 
This Escrow saga will never go away in peace without Kikwete,I've said it so shall it be,Kikwete will never get away with this.Atleast he won't die in peace without this saga coming back to haunt him.
 
.............
 
Are you serious or joking?
 
Anatania tuu ili thread yake na yeye isomwe na kuchangiwa na watu wengi...umefanikiwa katika hilo kaka hongera Pasco
 
Just Joking!.
P.

Naona tulio wengi tuko chapter one inayojadili kama kuna wizi umefanyika escrow au la na nani awajibishwe. Tayari kuna majibu mengi na wengine tumeyakariri tu .Hoja yangu bwana pasco ipo capter two maelezo yako hajajibu kitu chapter two kwa kuwa umekuja na hadith ya chapter one. Kwa kifupi chapter two inazungumzia way foward kutokana na mambo ya IPTL kuzungukwa na wawingu tena mawingu yaliyosababishwa na mabomu na uchomaji matairi.Kinachopingwa hapa ni kuendelea na IPTL bila kuichunguza vya kutosha.Idea ya IPTL kujifanya ndio wasamaria kwetu hiyo nitaipinga siku zote.Hawa jamaa hawatuibii ila wanatunyonya kupitia vipengele vya mikataba .Bwana pasco ukiacha akili za kuambiwa hebu fikiri kampuni hailipwi direct ,fedha zinaenda escrow kwa miaka saba na inadunda tu ?Nona umechota paragraph kubwa tu ambayo haijibu hoja.Katika hoja zangu sijaona ubaya wa rugemalila kupata fedha na nimesifu namna alivofanya amechukua kwa singa ambaye mkataba wake ni mnono sana.Jana raisi kaomba IPTL wapunguze zaidi bei ya umeme unafikiri kwa nini? Anafahamu kuwa IPTL wanamkataba wenye superprofit.,hilo analijua wazi.Inawezekana sana tu kwamba malipo ya capacity charge yanaiwezesha IPTL kupata faida katika equilibrium price. IPTL inatumia mafuta diesel kujiendesha ,katika upatikanaji wa haya mafuta sifahamu vizuri kama tanesco ama serekali ina role gani katika kuhakikisha yanapatikana .Tunambiwa kuwa hao IPTL watatumia gesi kuzalishia hapo tena watakuwa na mwanya wao wa janjajanja kama hatutabagain nao. Kitu kinachonisikitisha ni pale tunapotumia neno kuomba watupunguzie badala ya kujadili"Japo serekali haichimbi gesi imewezesha gesi ichimbwe na lengo likiwa kupunguza bei ya nishati. Inabidi tuwe na wataalam watakaotathmini hiyo gesi itasaidia kupata punguzo la kiwango gani katika bei ya soko maana kwenye biashara kubwa namna hii hata sent hamsini ya kitanzania kwa wiki ni mamia ya mamilioni.Watu wasafi washiriki kujadili hili si lazima watoke tanesco na wizarani.Shirikisha wataalam wa uchumi,uwekezaji na finance,wanasheria kutoka vyuo vikuu na jambo hili liwe wazi.Narudia tena bwana Pasco kipigo kingine kinaandaliwa kikubwa zaidi ya hiki maana kuna marejesho ya hela seth alizotapanya.
 
Asante nimekuelewa.
Pasco
 
Mkuu Pasco u-mwandishi mwenye uweledi. Nachelea sana watanzania kinachotuponza ni siasa hata kwa mambo yasiyohitaji siasa. Kipengere namba 5 kilitosha kabisa kumaliza hizi hoja lakini safari ya Dar Mwanza badala ya kupita Dodoma tunapita Arusha - Nairobi ndiyo rufike Mwanza.

Ok pesa si za umma lakini mtiririko mzima umejaa rushwa. Sina muda ya kuzinguka hapa, ningekuwa na mamlaka kwanza Edward Hosea ningemuweka kizuizini kwa kushindwa kufanya kazi yake na kulisababishia taifa hasara.

Bodi ya tanesco iliyomaliza muda wote wangeshitakiwa kwa kulitia taifa hasara.

Viongozi wote wa umma waliopokea fedha toka kwa JR bila ku-declare conflict of interest kwa mujibu wa sheria ya maadili ya utumishi wa umma wote wangepigwa chini na kiasi walichopokea kutaifishwa.

Washauri wa Rais wote ningepiga chini maana hawana msaada, na kama walimshauri Rais naye akakataa kwa sababu azijuazo mwenyewe wangeomba kukaa pembeni kama wafanyavyo wenzetu wenye demokrasia ya wastani ili kulinda heshima zao.

Baada ya kumshughulikia Hosea najua ningepata na mengine mengi ambayo ningeendelea kuyafanyia kazi. Tofauti na hapo Tanzania hatuendi kokote na kwa style hii ya viongozi kuendelea kulindana ikifika mwaka 2025 Watanzania tutakuwa wapangaji ndani ya nchi yetu wenyewe
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…