Wanabodi,
Kwa waliosoma fasihi, kitabu cha "An Enemy of the People" by Henrik Ibsen mnaweza kuniita mimi Pasco wa JF, kuwa ni "an enemy of the people!", Fedha za Escrow, Sio Fedha za Umma!, hizo Bilioni 320 zilizokuwa kwenye account ya Escrow, hazijaibiwa!, bali zimetumika kulipia umeme!.
Inawezekana PAP amenunua kampuni hewa, amefanya utapeli kuinunua IPTL toka kwa wamiliki halali, hayo hayatuhusu, bali malipo ya Tanesco kwenye account ya escrow ni kulipia capacity charges ya mitambo ya IPTL ambayo ni mitambo kweli sio mitambo hewa!, na pia Tanesco inalipia malipo ya huduma za umeme kweli unaokuwa genereted na mitambo ya IPTL, ni umeme kweli na sio umeme hewa!, na imeelezwa kuwa Tanesco bado inadaiwa!.
Ukiwa mkweli sana wa type ya ukweli huu, pia lazima uwe tayari to pay the price!.
Niko tayari to pay the price of expresing my opinion kuwa Nimesikitishwa!, Huzunishwa!, na Kufadhaishwa na Uongo wa Kamati ya PAC!-Escrow Sio Fedha za Umma!.
Pasco.