Hii tabia ya kumsimanga Zitto, na kutaka kumtumia tu pale mnapodhani Chadema itanufaika kisha baada ya hapo mnaleta dharau na kejeli dhidi yake ni jambo baya sana
Hawa wasiomwamini Zitto na kumshushia kila aina ya shutuma kuwa sijui haaminiki hawasemi lolote juu ya Mashinji, Kafulila, Waitara, Dr Slaa, Mollel, Silinde, Lijualikali, Katambi waliounga mkono juhudi. Once upon a time mlikuwa mkiwaona watu hao kama makamanda wa ukweli, wapinzani wa ukweli kuliko Zitto lakini Je leo wako wapi?
Kuanzia mwaka 2017 hadi 2020 June mwaka buu kabla Lissu hajarudi ni Zitto ndiye aliyebeba jukumu la kubeba tochi ya upinzani dhidi ya CCM na Magufuli, na aliupa upinzani lifeline ya kutosha baada ya Magufuli kuweka kibano kikali kwa upinzani kwelikweli.
Leo Lissu karudi na anaonekana kupata umaarufu basi mnaleta nyodo kwa Zitto
Acheni mambo yenu nyinyi, Bila ACT na Membe kumuunga mkono Lissu, Mikoa ya kusini na Zanzibar Lissu hawezi kutoboa!. Hivi nyie hamlionk hili?.
Zitto anajaribu kusacrifice kupoteza opportunity ya kuijenga ACT nchi nzima kwenye msimu huu wa kampeni kwa ajili ya kumng'oa Magufuli na CCM halafu bado mnaongea shombo dhidi yake?
Mimi namshauri Zitto, kama Chadema wataweka ubinafsi mbele, basi ACT songeni kivyenu, hamkuanzisha chama ili muwe wabeba viatu wa vyama vingine