Uchaguzi 2020 Nimesimamia uchaguzi, nimetenda haki

Uchaguzi 2020 Nimesimamia uchaguzi, nimetenda haki

swagazetu

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2013
Posts
4,250
Reaction score
1,470
Kimsingi binafsi nilisimamia uchaguzi, jioni msimamizi ngazi ya kata akanipigia simu akauliza nipe matokeo, nikampa, akauliza mbona yako hivi nikamwambia wewe ulitakaje? Akasema mbona matokeo yako hivi nikamuuliza ulitaka ya namna gani, akasema kwani kwenye semina hukuwepo nikamwambia nilikuepo na nilielewa.

Kwa kweli yale mafundisho yaliyokuwa yanatolewa kwenye semina na mashinikizo ya wakurugenzi! Nilifika hatua nikakereka mno.

Baadae msimamizi akaniuliza na mawakala umewapa nakala ya haya matokeo, nikamwambia kila mmoja amepata, akaniambia jaza fomu za matokeo upya nikamwambia hapa nasubiri malipo tu ukiona hayafai endelea, kimsingi niliondoka tulipokuwa. Kiufupi haukuwa uchaguzi.
 
Kwa vile umeamua kuungama hadharani basi kitubio chako ni utaje wazi hapa jukwaani yale mliyo fundishwa kwenye hizo semina za wakurugenzi. Epuka kutaja majina ya watu na mahali kwa usalama wa maisha na ajira yako.
 
1. Kuna chama kimoja ambacho wagombea wake wote hawajawahi kukosea kujaza fomu za kugombea ngazi mbali mbali wakati vyama vingine vimeshindwa mpaka kupelekea chama hicho kupita bila kupingwa.

2. Kuna chama kimoja ambacho mawakala wake wote hawajasumbuliwa kuapishwa na kupewa utambulisho katika vituo vya kupigia kura wakati vyama vingine vikiwa na makosa ya hapa na pale mpaka kuondolewa kwenye vituo hivyo.

3. Kuna chama kimoja kilichokubalika sana na wananchi kila sehemu na kuchaguliwa kwa kishindo na kuangusha ngome zote zilizokuwa sumbufu kwao kwa wakati mmoja.
 
Uchaguzi umeisha wafuasi wa Lissu bado mnaweweseka kwa kipigo kikali mlichokipata.
 
1. Kuna chama kimoja ambacho wagombea wake wote hawajawahi kukosea kujaza fomu za kugombea ngazi mbali mbali wakati vyama vingine vimeshindwa mpaka kupelekea chama hicho kupita bila kupingwa...

Chama hicho lazima kiwe ni chama cha majambazi!

Haiyumkiniki kinaogopwa haswa!
 
Tupe matokeo yalikuwaje basi, maana uhalisia ni kuwa kwenye urais JPM kashinda hata kama wakirudia leo, Lissu anapigwa tu, ukakasi upo kwenye baadhi ya majimbo kura za ubunge kuchakachuliwa.....but not the entire election
 
CHADEMA bana, Kwahiyo kwenye semina mlipewe maelekezo ya kufanya uhalifu ukakubaliana nayo na kuapishwa juu na ukiwa unajua maelezo uliopewa, ...

Aiseee kazi ipo
 
Back
Top Bottom