Nimesitisha kutoa mahari

Mh hivi una uhakika kweli ulikuwa na lengo la kupeleka mahari kwao huyo mchumba wako!!? [emoji849]
Hamna kitu hapoo watu tushapitaa huko.. Anamfanya mtoto wa watu boyaaaa tu hakuna Mwanadamu mwenye huruma kiasi hicho dunia ya leooo[emoji1787][emoji1787] Huyo demu atafute jamaa ambae yupo serious naee huyu hamna kitu.
 
Kanywe Pepsi kwa mangi nakuja kulipa,umenikosha
 
Kiongozi unaishi sayari ipi kwanza, kiasi hujui kwamba jamii nyingi hasa za kiafrika kwa asilimia kubwa zimemfavour zaidi mwanaume kuliko mwanamke, hasa kwenye masuala ya mahusiano na ndoa kwa ujumla

Unaniambia habari za malaya tu kana kwamba wanawake wote kwenye jamii ni malaya, ofcourse wapo wanawake walioamua kuignore mitazamo ya jamii japo nao bado mnawasakama, lakini wanaoumia wengi ni wale ambao bado wamefungwa na hiyo mitazamo na pengine wanajiheshimu bado

Simple ili hayo malalamiko yenu yawe valid jamii iache hiyo mitazamo ya hovyo kuhusu ndoa na wanawake kwa ujumla, wanaume muache kulalamika kuwa wanawake wa siku hizi wameharibikiwa wamekuwa malaya na wanawapotezea sana pesa, ili kusudi na wanawake nao wawe huru na wasijione kama huwa wanapotezewa muda
 
Hakuna kitu kama hicho
 
Mfano niliokupa niwakueleweka sana sikutaka kutaja mambo yote, mbona yanajulikana. Unataka kuwa huru, nani kakushikilia, we umeshikiliwa akili na jamii. Hii ndiyo mindset ninayoichukia. Jamii ikuache huru, ninani asemwi katika jamii kwa akili yako. Yaani sijui kwanini hata msome vipi bado akili unashikiwa na watu. Mwanaume kubadilisha wanawake ni umalaya lakini hataacha mpaka apate aliyesahihi na kuitwa majina hainizuii kuishi. Ni sawa na kufikiria nchi itakupa maendeleo wakati hata nchi iwe tajiri kiasi gani kama hujui kujiendeleza utabaki hapohapo. Wewe ni wewe, we jamii itakufanya nini, stop being childish. Eti ikupe uhuru[emoji23][emoji23][emoji23], umewaza kwaakili kweli. Mahusiano na ndoa yamemfavor mwanaume wapi au kujifanya vilema muonewe huruma. Nyinyi kutangaza kama mnasemwa na jamii ndo mnafikiri sisi tunafavor sana. Yaani it's a bogus mindset. Mimi sinahata hamu ya mtoto wala mke muda huu ila unajua ninavyosemwa na kila ndugu na wazazi. Uletwe mwenyewe duniani na ufe mwenyewe ndio useme umeshikiliwa. Just one sentence, Acha kushikiwa akili.
 
Kama unakipenda kitu kiache kiende, kama kitarudi basi kilikuwa chako, kama hakitarudi basi hakikuwa chako.
 
Katika maisha kila mtu ana nafasi yake
Wazazi wana nafasi yao
Mke/mume ana nafasi yake
Marafiki wana nafasi yao
Ndugu wana nafasi yao
Watoto wana nafasi yao
Ikitokea nafasi ya wazazi ukaipeleka kwa mke/mume tayari unakosea au nafasi ya watoto ukaipeleka kwa marafiki pia ni shida, muhimu ni kujifunza kubalance kwa watu wote kwa kuzingatia nafasi zao jamani.
Huyo rafiki yako alikuwa na nafasi yake kama rafiki na mchumba wako alikuwa na nafasi yake kama mke mtarajiwa, umeshindwa kutatua changamoto ndogo kama hiyo ili wote waendelee kubaki katika maisha yako kweli? Huyo mchumba wako katumia hasira tu
 
Mimi sijashikiwa akili mkuu nilishatoka huko, ila nimegundua hapa unajiongelea mtazamo wako binafsi, while mimi naongelea mitazamo ya wanaume wengi kwa ujumla

Tunatamani wanaume wote wangekuwa kama hivyo, but unfortunately haiko hivyo wengi wana mitazamo kama ninayosema, na ndio hao vinara wa kudhalilisha wanawake

Na kibaya zaidi ni kwamba kwenye jamii zetu anayeamua ndoa ni mwanaume, kwahiyo wale wanawake walio desperate na ndoa wakiteleza kidogo tu wanatishiwa kutokuolewa, so inabidi watii ili 'wasitiriwe' na jamii iwaelewe
 
Mwamba, sijamfukuza. Kaamua mwenyewe kwamba ifike mwisho. KARMA hapa nitapataje mkuu??
 
Nadhani hukumpenda kwa moyo wote ndo maana alipokwambia mvunje uchumba ulikubali faster, huo ni mtazamo wangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…