Nimesitisha kutoa mahari

Nimesitisha kutoa mahari

Hakutaka kukubali. Mfano, nilimsihi nipeleke mahari tarehe 28 badala ya tarehe ya mwanzo. Tena kwa kunyenyekea sana lakini bado akesema hapana. Nilitumia busara sana ila hakuwa tayari kuelewa.
Usingemwambia juu ya kusaidia rafiki. Ungesema tu kwamba Kwa sabb ya dharura fulani, pesa ya mahari itapatikana tarehe 26 au 27, so utaipeleka 28th
 
Katika maisha kila mtu ana nafasi yake
Wazazi wana nafasi yao
Mke/mume ana nafasi yake
Marafiki wana nafasi yao
Ndugu wana nafasi yao
Watoto wana nafasi yao
Ikitokea nafasi ya wazazi ukaipeleka kwa mke/mume tayari unakosea au nafasi ya watoto ukaipeleka kwa marafiki pia ni shida, muhimu ni kujifunza kubalance kwa watu wote kwa kuzingatia nafasi zao jamani.
Huyo rafiki yako alikuwa na nafasi yake kama rafiki na mchumba wako alikuwa na nafasi yake kama mke mtarajiwa, umeshindwa kutatua changamoto ndogo kama hiyo ili wote waendelee kubaki katika maisha yako kweli? Huyo mchumba wako katumia hasira tu
na alitakiwa aendelee kuongea naye make taarifa ni ya ghafla ukizingatia mtu mwenyewe rafiki nani atakuelewa kwa haraka
 
Unajua kumuona mtu unaemjua vizuri anataabika na changamoto za maisha ni mbaya sana. Ni bora uamue kufanya maamzi magumu.
Sawa.. Lakini kama ungekuwa na uwezo wa kapata hiyo mahari tarehe 28, kwanini huyo rafiki yako usimpange kumpa hiyo tarehe 28, afu mahari ukatoa 20th kama mlivyopanga mwanzo?
 
Nilipomsihi awe na subira, alikataa.
Hakuwa Mtu sahihi kwako,I have a friend ana mchumba wake huyo now ana mtoto wa miaka miwili na ana mimba amejitambulisha Tu ukweni hajatoa hata Mia, anasema ataenda huko mbeleni na wala hawana mgogoro wowote....mwanamke hakuona future kwako,if you have a bright future hamna mwanamke wa kukuacha hata umcheat vipi women are cleverest
 
Tarehe 20 ya mwezi huu niliahidi kwenda kutoa mahari ukweni kiasi cha shilingi milioni mbili na laki tano.

Niliazimia kufanya hivyo baada ya kukaa na mchumba wangu kwa zaidi ya miaka miwili sasa katika mahusiano. Baada ya kutoka safarini wiki iliyopita, nilishikwa na simanzi sana.

Nilimuona rafiki yangu wa karibu wa siku nyingi ambae alikuwa msaada kwangu toka tukiwa shuleni. Physics, chemistry na maths nilifaulu kwa sababu ya uwepo wake.

Nimetafakari mno na hatimaye, jana nilimueleza wazi mchumba wangu kwamba siwezi kuendelea na zoezi la utoaji mahari kwao kwa sababu kuna mtu ambae nahitaji kumshika mkono aondokane na magumu yanayomkabili kwa sasa.

Alisema hakuna shida na kisha kuomba kuvunja uchumba wetu. Sikuchukua muda tena kulifikiria hilo. Nimekubali na kumtakia kila la kheri katika maisha yake mengine.

NITASIMAMA NA RAFIKI YANGU!
What if, siku moja ukamkuta huyu mchumba uliyemkataa ndio mke wa huyo rafiki yako uliyeamua kusimama nae. Hukufanya maamuzi sahihi.
 
Hakutaka kusubiri. Huyu mwamba amekuwa nami katika kila hali kabla mimi sijkaa sawa. Ni mateso kwangu kumuona anahangaika. Ngoja mwanamke aondoke. Muda sahihi ukifika atapatikana mwingine.
Wee jamaa mapenzi hayaji kukusumbua hata siku moja, kati ya mapenzi na urafiki chagua urafiki na kati ya mapenzi na kazi au ndoto zako chagua kazi hata mwanamke awe mrembo vipi
 
Hakutaka kukubali. Mfano, nilimsihi nipeleke mahari tarehe 28 badala ya tarehe ya mwanzo. Tena kwa kunyenyekea sana lakini bado akesema hapana. Nilitumia busara sana ila hakuwa tayari kuelewa.
Hakukupenda huyo!

Mwanamke aliekupenda anakupa option zote as long as anafurahia Maisha mnayoyaishi!!

Wanawake wanaong'ang'aniza NDOA ni kuwaogopa Sana!
 
Sikweli, maana mwamba hakumfukuza wala hakusitisha kutoa mahari bali aliyesitisha ni binti, acha kutishana. Pia achana na maconspiracy theory, mabinti wamelizwa na watu wao uko zamani sana ndio maana hawapo bikra, leo umtupie lawama jamaa.
Utakuwa kundi moja na #kataandoa. Hahahaaa....wadada kazi wanayo.
 
Maisha Ni fumbo kubwa,uliyekuwa unamlia chabo darasani leo hii anakulia chabo mtaani
 
Amini amini nakwambia, siku utapooa huyo rafiki ndio atakumegea mkeo.
 
Mimi sijashikiwa akili mkuu nilishatoka huko, ila nimegundua hapa unajiongelea mtazamo wako binafsi, while mimi naongelea mitazamo ya wanaume wengi kwa ujumla

Tunatamani wanaume wote wangekuwa kama hivyo, but unfortunately haiko hivyo wengi wana mitazamo kama ninayosema, na ndio hao vinara wa kudhalilisha wanawake

Na kibaya zaidi ni kwamba kwenye jamii zetu anayeamua ndoa ni mwanaume, kwahiyo wale wanawake walio desperate na ndoa wakiteleza kidogo tu wanatishiwa kutokuolewa, so inabidi watii ili 'wasitiriwe' na jamii iwaelewe
Ndio maana nakwambia bado unashikiwa akili na jamii. Tell me ndoa inakusitiri vipi kama bado wote ndani ya ndoa mnachepuka, maana ndiyo jamii ilipofikia huku simwanaume au mwanamke. Ishi maisha yako, hiyo desperateness siunajiletea mwenyewe kwakuruhusu kuendeshwa na misemo ya kijamii. Kwani unafikiri wanaume hawatishiwi kuwa ataachwa na huyohuyo mwanamke kama hana pesa za kumtunza. Achana na self centered mind kuwa mwanamke anaonewa, mnaakili na mmesomeshwa hivyo mmeelimika hivyo acha umimi au sisi, ni kitu cha ujinga sana. Mitazamo ya wanaume wengi, how did you come into that conclusion ilihali hujakutana hata na robo ya robo ya wanaume wakitanzania. Don't make accusations ambazo huna evidence nazo, ni kujivictimize. Wewe umeona nimeita wanawake wengi malaya lakini sindio wengi wanajipotray hivyo kwenye social medias. Am still telling you, this is why I hate women of this generation.
 
Utakuwa kundi moja na #kataandoa. Hahahaaa....wadada kazi wanayo.
Bado unaendelea na assumptions. Bro, acha hiyo tabia. Ndoa ni kitu chema ila katu sitatumia tamaa au hisia kufanya hiyo decision, bali tutatumia akili. We are not perfect but big red flags siwezi kuzisahau, mahusiano yatasitishwa tu. Am a serious man basi usitegemee nitabadilika leo kufuata mahisia ili tu nioe. Maana hata leo, jamii imehaaribu maana ya ndoa na kuiteketeza familia basi kuoa kupo tu na kuna wakati wake ila silazima.
 
Huyo rafiki tu au kuna mengine
Maana ma Pungazozo mko kila mahali na mnatokea hukohuko vyuoni
 
Back
Top Bottom