Nimetapeliwa elfu hamsini (50,000/-)na huyu dada tuliyeheshimiana sana, nimfanye nini?

Nimetapeliwa elfu hamsini (50,000/-)na huyu dada tuliyeheshimiana sana, nimfanye nini?

Khali gani JF, wanamfungo nawatakia ufungaji mwema,

Jana nimenusurika kuitiwa mwizi na huyu dada,

Niliyemuamini sanaaa, na niliyemheshimu sana,

Alikuja analia nimkope 40k, card yake ya bank ili crack na home walimuambia after 4 days watamtumia hela.


Nikatoa 50k kwa bahati mbaya mfukoni wakati natoa akaona,

Akasema niongeze na hiyo nyingine atanilipa zote,

Zimepita week nne wakati aliahidi siku nne tu,

Akasema wazee wake watamtumia 300k na atanilipa.


Huyu binti sio kuwa kwao hawana hela, wana hela sana tu na hiyo kunikopa ni kutokana na card yake ya bank kupata matatizo,

Basi bhana na kweli after siku nne akatumiwa laki 4,


Na muamala akanionesha kuwa kesho yake atanitumia 50k yangu,


Nikasubiri kesho aitume ukizingatia hata mwenyewe nilikuwa vibaya kiuchumi,


Mpaka saa 4 usiku hakuna muamala, natuma txt hajibu, simu hapokei,


Tunakaa jirani tu si huwa tunaonana sometimes, tukionana salamu hatoi yaani alinichunia,

Nikamfuata hostel kwake, cha ajabu nilipogusia suala la hela na kumuambua nina shida mno, akanibadilikia mpaka sauti,

Na akaanza kunikoromea, uvumilivu ukanishida nikaja juu, akaanza kuita mwizi serious kabisa,


Uzuri nina mbio sana, nikaepuka kisanga kile, akaanza kutangaza kwa watu kuwa mimi jogoo hapandi mtungi.


Na wakati nilimheshimu na tuliheshimiana kama kaka na dada tu,


Nimeumia sana japo ni muda kidogo umepita, kwa nini wema wangu unaniponza?


Nipeni approach nzuri ya kumfanyia umafia(si kumbaka) huyu mtu. Nataka aumie iwe physically au mentally


NB: Sikuwahi kuonesha hisia wala viashiria vyovyote vya kumtaka kimapenzi, tuliheshimiana na tulikuwa na mipaka.
Tafuta hela bwasheee, elfu 50 sio pesa ya kumfanya mwanaume afungue thread JF.
 
Pole mkuu !!! mwanamke ukimuazima hela ye anachukulia umempa io hela samehe anza moja mm nshajiapizq hata nimkute demu hospital anikope pesa qnunue vidonge simpi ata anioneshe cheki ya bank simpi simpiiiiiiiii
Umenikumbusha kuna mmoja aliniomba nimpe 20 atarudisha baada ya siku 2, nikampa 10, ila cha ajabu hata hicho kidogo hakurudisha, mbaya zaidi anataka nimpe pesa nyingine.
 
Mwanamke akopeshwi anapewa fullstop lBda dada ndo unaweza mkopesha, uyo dada ako mmezaliwa wote au shoga ako
Ninadada yangu mtoto wa shangazi huwa nikimkopesha anarudisha na mimi nikipata tatizo ananisaidia hivyo wanatofautiana mkuu.
 
Tafuta polisi uongee nao vizuri wamtikise halafu wamuweke ndani hata weekend moja

20220128_221738.jpg
 
Katika maisha yangu sitakopesha na hata nikikopesha haizidi 10k ili roho isiniume sana atakapo nidhurum, si mwanamke si mwanaume. Mimi ninakasumba moja ya kuwa mwaminifu na hata nikikopa leo kesho au ndani ya wiki narudiaha ila sasa wao wakikukopa hawarudishi na mimi sikopeshi ng'o
 
Back
Top Bottom