HOJA Nimetapeliwa Milioni 5 na Tapeli wa Forex, watu wajihadhari. Mamlaka zichukue hatua

HOJA Nimetapeliwa Milioni 5 na Tapeli wa Forex, watu wajihadhari. Mamlaka zichukue hatua

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Hivi hizi IDs za anonymous zipo ngapi humu jukwaani? Maana sio kwa malalamishi hayo yanayotolewa na hizo IDs
 
Kuna tatizo la watu hawa wanaojifanya matajiri kupitia Forex na kuigiza maisha ya kifahari?

Ukweli ni kwamba kuna mmoja alituaminisha sana. Mimi na rafiki yangu tukachanga shilingi milioni 5 na kumtumia, tukisubiri faida kama alivyotuahidi.

Baadaye akaunti yake ya Instagram ikatoweka ghafla. Hali hiyo ilisababisha mgogoro kati yangu na rafiki yangu, kwani alidhani nimemfanyia utapeli.

Baadaye aliwasiliana na Jackan FX, ambaye alimwambia atume fedha nyingine ili aweze kurudishiwa mara mbili ya kile alichowekeza.
Wewe unabahati umepoteza mil 5, miaka kama mitano au sita nilipoteza $25,000/- kwa mambo hayo ya online business za Forex, ndipo nikaamini hakuna short cut kwenye mafanikio, kila kitu kina mchakato wake.
 
Kwani FOREX ni nini?
FOREX ni kifupi cha Foreign Exchange.
Foreign Exchange ni biashara ya kununua na kuuza fedha. Unanunua mzigo wa wa fedha fulani katika soko fulani na kwenda kuuza huo mzigo wa fedha kwenye soko fulani. Mara nyingi ni fedha za kigeni kwa fedha za kigeni. Au fedha ya kigeni kwa fedha ya nchi yako.

Je ulinunua mzigo wa fedha? Au ulimpa tu pesa bila kupewa mzigo wa fedha.
Hapo ni sawa na kumtafuta mtu mtandaoni anaye uza nyanya na kumtumia pesa ili akutumie mzigo na kuamua kutokomea na pesa.

Lakini FOREX ni biashara yenye faida kubwa sana ndio biashara ambayo inazipa utajiri bank zetu. Wote hao CRDB, NMB, NBC wanafanya FOREX.
 
Kwanza unatokea wapi ? itabidi siku moja niwapte darasa la utapeli wote ..Nikupe pole tu , hauwezi kumfanya chochote wakati yule Gavana anaongelea hizo ishu haziko regulated , mnajifanya mko mbele ya muda .

Mdogo wangu , mimi hiyo forex naijua tangu mwaka 2015 , na hizo crypto nimetumia na kina Mallybitoin, frankkasonso na Jordan , enzi za lovcalbitcoin . sijui kama hizo platfom ipo ila niliacha hizi ha za kusadikika mwaka 2020 na sina time nazo.

Mtaendelea kupigwa sana , kwa vile hata wewe hujuilizi hiyo ndiyo biashara pekee watu wake wanaonesha mafanikio, kuna makini kuna dogo anajiita richlit , anauza sura sana kuwa makini sana . kuna yule Magnettic anataka kurudi tena mjini baada ya kuwapiga watu ,amekuja na interview mpya ya kujisafisha
Kwani FOREX ni nini. Au kinachowatapeli ni masoko ya uongo wanayo jiingiza. Sidhani kama FOREX ina tatizo.
 
Kwani FOREX ni nini?
FOREX ni kifupi cha Foreign Exchange.
Foreign Exchange ni biashara ya kununua na kuuza fedha. Unanunua mzigo wa wa fedha fulani katika soko fulani na kwenda kuuza huo mzigo wa fedha kwenye soko fulani. Mara nyingi ni fedha za kigeni kwa fedha za kigeni. Au fedha ya kigeni kwa fedha ya nchi yako.

Je ulinunua mzigo wa fedha? Au ulimpa tu pesa bila kupewa mzigo wa fedha.
Hapo ni sawa na kumtafuta mtu mtandaoni anaye uza nyanya na kumtumia pesa ili akutumie mzigo na kuamua kutokomea na pesa.

Lakini FOREX ni biashara yenye faida kubwa sana ndio biashara ambayo inazipa utajiri bank zetu. Wote hao CRDB, NMB, NBC wanafanya FOREX.
Forex inayo zungumziwa hapa ni tofauti na hiyo forex ya ununuaji na uuzaji wa fedha halisi.

hii forex ni algorithm tu, ndio maana ukitazama ubadilikaji wake, ni tofauti na wa soko la fedha
 
Back
Top Bottom