HOJA Nimetapeliwa Milioni 5 na Tapeli wa Forex, watu wajihadhari. Mamlaka zichukue hatua

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Hivi hizi IDs za anonymous zipo ngapi humu jukwaani? Maana sio kwa malalamishi hayo yanayotolewa na hizo IDs
 
Wewe unabahati umepoteza mil 5, miaka kama mitano au sita nilipoteza $25,000/- kwa mambo hayo ya online business za Forex, ndipo nikaamini hakuna short cut kwenye mafanikio, kila kitu kina mchakato wake.
 
Kwani FOREX ni nini?
FOREX ni kifupi cha Foreign Exchange.
Foreign Exchange ni biashara ya kununua na kuuza fedha. Unanunua mzigo wa wa fedha fulani katika soko fulani na kwenda kuuza huo mzigo wa fedha kwenye soko fulani. Mara nyingi ni fedha za kigeni kwa fedha za kigeni. Au fedha ya kigeni kwa fedha ya nchi yako.

Je ulinunua mzigo wa fedha? Au ulimpa tu pesa bila kupewa mzigo wa fedha.
Hapo ni sawa na kumtafuta mtu mtandaoni anaye uza nyanya na kumtumia pesa ili akutumie mzigo na kuamua kutokomea na pesa.

Lakini FOREX ni biashara yenye faida kubwa sana ndio biashara ambayo inazipa utajiri bank zetu. Wote hao CRDB, NMB, NBC wanafanya FOREX.
 
Kwani FOREX ni nini. Au kinachowatapeli ni masoko ya uongo wanayo jiingiza. Sidhani kama FOREX ina tatizo.
 
Forex inayo zungumziwa hapa ni tofauti na hiyo forex ya ununuaji na uuzaji wa fedha halisi.

hii forex ni algorithm tu, ndio maana ukitazama ubadilikaji wake, ni tofauti na wa soko la fedha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…