Nimetapeliwa na muuza mkaa

Nimetapeliwa na muuza mkaa

Ya kweli haya au stress za mafuta kupanda bei yaani kupanda jero tu mnalia je yakifika 7000
 
Hilo gunia Usifungue Mbele ya watoto,Huko mbele Unaweza kuta vifaa vya Guest.Ila tutashuhudia mengi mwaka Tunahumiana wenyewe kwa wenyewe wakati Aliyepandisha mafuta Yupo huko.
Au labda naweza nikakuta nayeye ameficha hela...😜
 
Hyo pcha inazunguka zunguka tu kweny mitandao...naona umeamua kuiwekea script kidogo kupata likes...ila cha ajabu hadi watu wanakupa pole.
Binti ebu uwe umwenye heshima kwanza, mimi sijaja kutaguta like hapa na hata nilizo nazo natafuta pakuzigawa...🤨☹️
 
Nilipotoka tu, nikavamia K-Vant kubwaaaaaaaa.

Kabla sijaimaliza, akapita muuza mkaa "simnajua gesi imepanda bei..!!"

Basi kwa mbwebwe kibwena nikamuagiza apeleke kwa nyumba na pesa nikamlipa kabisa kwa jinsi alivyojua kuujaza hadi kisunzu...[emoji12][emoji12]

Sijakaa muda waifu kapiga simu kusema asante baba watoto, asante mume wangu, asante kwa kujali na kadhalika zote mnazozijua wababa.

Sasa haya ndio yalonikuta, muuza mkaa ameniharibia upendo kabisa wa leo. Na sijui kama wiki hii nitapewa...[emoji55][emoji58]

Dhulmati ni shetani asiye na rangi na anabadili umbile kutokana na mazingira!

Hata hivyo kazi ya kujaza kuni kuni pamoja na vifuu kiroba kizima ni ngumu kuliko kujaza mkaa original!

Na maeneo uliyonunulia hatapita milele hadi kufa kwake, ndiyo taratibu zao.
Pole mkuu.

Me huwa nawashangaa wanaojimwambafy kuwa hawatapeliwi, sasa hapo vipi, kunakukwepa?
 
Back
Top Bottom