Nimetapeliwa zaidi ya Tsh. 45,000,000 kwa kuuziwa kiwanja feki

Haya mambo yasikie tu.

Nina siku ya nne leo tangu nigundue kwamba nimepigwa, hata kula vizuri siwezi, nawaonea wivu wenzangu walionunua maeneo madogo kwa bei za 15m kushuka chini. Naona hasara yao ni ndogo kuliko yangu.
Fafanua kidogo
Kilikuwa kwenye gunia kama mbuzi au documents feki?
 
Unachanganya kati ya title deed na offer letter. Offer letters ndio zinaweza kutoka zaidi ya mbili. Wanaolewa haya mambo wanalifahamu hili
Tumekusoma mkuu! Wengine wana mahaba Tu kila kitu mwendazake! Wangejua ni marais wote wanafanya kutengua title deeds! Ni mchakato wa kawaida ingawa huwa ni wa muda mrefu!
Hata mwendazake hizo kesi kazikuta zote zina muda mrefu!
 
Mimi naweza kuchallenge Kwa hoja hiyo ya GN na Newspaper na nikashinda, nakuhakikishia
 
Naomba maelezo mkuu,,, nataka kununua kiwanja hapa Dar, ktk haya makampuni yanayojinadi kuwa mteje ana ruhusa ya kulipia kidogo kidogo, na alimaliza anapewa hati... NAOMBA MAELEZO NAMI NISIJE NIKAPIGWA

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
wakuu bado niko kwenye mapambano makali ya kupata haki yangu nikitulia nitatoa mrejesho
 
Wakuu nimetapeliwa na hali bado tete nahisi hili jambo linaweza kuchukua mda mrefu na huku nikiendelea kutumia gharama zingine
 
Habari wakuu, hii post inazidi kusaidia wengi japo kuna watu wamenibeza kuwa natafuta wateja. Ila hadi sasa nina feedbacks kadhaa DM watu wamesaidika na kuepusha kutapeliwa ama kuingia kwenye migogoro ya ardhi mbeleni. Kama bado hujanunua ardhi pitia hapo na umshirikishe mwenzako umpendae.
 
Wakuu nimetapeliwa na hali bado tete nahisi hili jambo linaweza kuchukua mda mrefu na huku nikiendelea kutumia gharama zingine
Ipo hivyo mkuu, hiyo ndivyo haki hupatikana. Kama umewabananisha komaa nao tu maana unajua mwisho wa siku utapata chako hata kama utakua umeingiza hasara kidogo
 
KIWANJA KINAUZWA KIBAHA PANGANI
________________

Maelezo ya ardhi: Matumizi yoyote
_____________________
Kiwanja No: 70
_____________________
Mahali: Kibaha Pangani Mbele kidogo ya Stendi ya Mabasi Loliondo na ni kilomita 3 kutoka barabara ya Morogoro road, Kibaha Pangani, Dar es salaam. Tanzania
_____________________
Ukubwa wa Kiwanja: mita za mraba 698 SQM
_____________________
Bei: Tsh 9,500,000 (Inaweza Jadiliwa)
_____________________
Kwa maelezo zaidi Wasiliana nami kupitia:
Namba ya simu: 0626090873
0652251374 (WhatsApp)
Barua pepe: ismaildasilva92@gmail.com
 
Nashukuru ndugu zangu nimepambana nimeweza kurudishiwa viwanja vingine vya thamani ya tsh 32m, nimeshauriwa kuliko kuwafunga nikose thamani ya pesa iliyobaki ni bora niingie nao makubaliano kisheria ili waweze kunilipa hiyo 13m iliyobaki ambapo tumefanya hivo chini ya dhamana ya watu wao wa karibu walio na mali zisizohamishika ambazo wameweka bond
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…