Nimetapeliwa zaidi ya Tsh. 45,000,000 kwa kuuziwa kiwanja feki

Nimetapeliwa zaidi ya Tsh. 45,000,000 kwa kuuziwa kiwanja feki

Hebu weka mkasa mzima mkuu na sisi tujifunze! Ilikuwaje hiyo! Mimi mwenzio nilitapeliwa 2m lakini nilijidharau karibia wiki nzima, nawaza tu nilivyotapeliwa kiboya (ingawa kwangu niliona kuna nguvu za giza zilitumika). Sasa wewe 45m si unaweza kuchizika kabisa?
napambana nao hawa kimafia najua lazma watanifidia
 
Wengine kumuita wakili wanaona gharama.
Hawajui kuwa wakili ndo mtetezi wako hata ikitokea matatizo anayekwenda mahakamani kufuatilia kesi NI yule hakimu .
Wakati wewe unaendelea na Mambo yako
UTAPELI wa ardhi Mara nyingi huwa una mkono mrefu mpaka ardhi.

Unaweza kumtumia wakili ukapewa mpaka hati kutoka Ardhi lakini ukapige.
 
UTAPELI wa ardhi Mara nyingi huwa una mkono mrefu mpaka ardhi.

Unaweza kumtumia wakili ukapewa mpaka hati kutoka Ardhi lakini ukapige.
Tata document zangu zote zimepita kwa wakili, na baadhi ya wengine walipita kwa wenyeviti wa mtaa na mtendaji na bado tumepigwa.

Lakini naenda nao kimafia wote wako mikononi mwa sheria bado mmoja ambae ni Diwani mstaafu huyu ndio injini wa mtandao huu wa utapeli na lazima tumpate.
 
Unataka kusema tapeli anashirikiana na wakili?
UTAPELI wa ardhi Mara nyingi huwa una mkono mrefu mpaka ardhi.

Unaweza kumtumia wakili ukapewa mpaka hati kutoka Ardhi lakini ukapige.
 
huyo wakili ulimtafuta wewe au muuzaji?
Tata document zangu zote zimepita kwa wakili, na baadhi ya wengine walipita kwa wenyeviti wa mtaa na mtendaji na bado tumepigwa.

Lakini naenda nao kimafia wote wako mikononi mwa sheria bado mmoja ambae ni Diwani mstaafu huyu ndio injini wa mtandao huu wa utapeli na lazima tumpate.
 
Mkuu kwenye sheria ya ardhi, hao hawatambuliki kabisa kwenye kuuziana , labda kama ni ardhi ya kijiji.
Anayetambulika ni hakimu, na mawakili tu, ndio wanaoweza kusimamia mauziano hayo na yakawa na nguvu ya kisheria.zile hati za serikali za mtaa ni makaratasi tu, ambayo kisheria hayana nguvu kabisa.Ukiwa nalo hilo halafu akaja mtu akauziwa hicho kiwanja chako tena na akawa na hati ya mauziano yaliyosimamiwa na wakili, huwezi kushinda hiyo kesi kwa kuonyesha hizo karatasi.
Nimejifunza jambo hapa... Nasoma comments mkuu.
 
Haya mambo yasikie tu.

Nina siku ya nne leo tangu nigundue kwamba nimepigwa, hata kula vizuri siwezi, nawaonea wivu wenzangu walionunua maeneo madogo kwa bei za 15m kushuka chini. Naona hasara yao ni ndogo kuliko yangu.
Wapi huko mkuu
 
Nitafutie mbuzi weusi watatu, ng’ombe mmoja awe wa kisasa jike wa maziwa awe amezaa mara moja ndio dawa itashika, kuku wawili mmoja jogoo na jike, nitafutie na mchele wa kyela ndoo mbili kubwa ili kutoa kafara kwa wazee, na vitenge vitatu was original vya kufunikia dawa halafu hela usinipe yoyote ukifanikiwa utarudi kushukuru.
Unataka kufanya ufugaji[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ninaamini kabisa kuwa utapeli upo lakini kuna namna huwa watu tunaweza kuchukua tahadhari na kupunguza visa vya kutapeliwa.
KWA VIWANJA VILIVYOPIMWA:
[emoji91]Baada ya kuwa umeoneshwa kiwanja husika na mmekubaliana bei, hakikisha kuwa unampa wakili kazi ya kusimamia mauzo hayo maana ni lazma atafanya search katika mamlaka husika kujua mmiliki halali ama kama kuna attachment yoyote juu ya kiwanja husika
[emoji91] Hakikisha unajua marital status ya muuza kiwanja, kama atakwambia wameachana hakikisha anakuonesha hati ya talaka ama ya kutengana iliyotolewa na MAHAKAMA na sio vinginevyo.
[emoji91] Endapo ametengana kienyeji na mwenza wake hakikisha huyo mwenza anajaza fomu maalumu (spousal consent) ya kuridhia mauzo ya kiwanja husika yaani hata kama wamenuniana hakikisha mwenza amejaza hiyo form yeye mwenyewe.
[emoji91] Kama kutakua na wasiwasi wowote wa vipimo vya kiwanja husika vile vya kwenye nyaraka na uhalisia hakikisha mnaitumia mamlaka ya ardhi eneo husika kisha kuwakutanisha na majirani wako ili kuweka sawa suala hilo.

KWA VIWANJA/MAENEO AMBAYO HAYAJAPIMWA:
[emoji91]Hakikisha kuwa unawapata watu wote wa pande zote ambazo eneo hilo mnapakana na wakuoneshe na mkubaliane wote mipaka halisi ya eneo unalotaka kununua na hawa ndio watakua mashuhuda wa mjataba wako.
[emoji91]Hakikisha mauziano hayo yanasimamiwa na wakili ambaye atakuongiza katika kufanya search na taratibu sahihi.
[emoji91]Hakikisha mwenza wa anayekuuzia eneo husika anajaza form maalumu ya kuridhia mauzo hayo na kama wameachana hakikisha unapata nyaraka ya mahakama kuthibitisha hili.

KWA MAENEO YA UKOO/FAMILIA/URITHI.
Hapa ndio kuna kivumbi na wanunuzi hupoteza sana pesa hapa.
Kuna wakati ambapo mzazi/mmiliki wa eneo akifariki basi familia haifungui mirathi mahakamani bali hukaa kikao na kuamua kutoaiuza ardhi lakini wakagawanya vyumba ama hisa katika nyumba husika mfano, huweza kugawana vyumba hivyo kila mmoja akawa na mpangaji wake ama wakaipangisha kisha kila kodi ikitolewa basi wanagawana.
Sasa endapo unataka kununua ardhi ya mazingira ya namna hii unatakiwa kuwa makini sanaaa na endapo nyumba ni ya familia hakikisha kuwa wale wanafamilia woooote yaani namaanisha WOTE sio wengi hapana, nasema WANAFAMILIA WOTE wahaohusika na ardhi ama nyumba husika ndipo muweze kuendelea na mauzo. Hii ni kwa sababu endapo ikatokea mmoja ama sehemu ya wanahisa wa hiyo ardhi ya familia hakuridhia basi utakua umepigwaaa(rejea kilichomkuta S. H. Amon hapo Kariakoo)
Iwapo nyumba inamilikiwa na Ukoo yaani vizazi hata viwili ama vitatu yaani nyumba alikua anamiliki babu yangu ambaye alikua na watoto nane na wote hao walikua na familia, wakafariki 4 na watoto wa babu wakazaa tukatokea sisi na baadhi yetu tumeshafariki lakini tumeacha watoto wetu ambao wana haki kupitia baba na babu zao aisee mimi NINAKUSHAURU USINUNUE ARDHI HIYO hakikisha kabla ya kununua au kulipia hata sh mia unawasiliana na wakili wako.


Kiukweli wakuu ukitapeliwa kwenye kiwanja kilichopimwa ni lazma wewe mnunuzi kuna mahali ulizembea kwenye utaratibu mzima wa manunuzi maana kwa upande wa hivi viwanja vilivyopimwa utaratibu upo wazi sana.
Nilichogundua ni kuwa wengi wana mazoea na kukalili taratibu za kizamani zisizotambuliwa kisheria yaani mtu anaona kutoa 2M kwa wakili asimamie mchakato mzima wa mauziano ya 50M anamuamini dalali ambaye atalipwa 10% na mtedaji/mwenyekiti halafu anatoa hela[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

HAKIKISHENI MNAFUATA MIONGOZO YA WANASHERIA KUPUNGUZA KUTAPELIWA
Umenipanua ubongo, kwa kuelewa mambo ambayo kabla ya hii topic sikuyaelewa hasa hili la "mwenza", dah! Isee ubarikiwe sana.
 
Mkuu kwenye sheria ya ardhi, hao hawatambuliki kabisa kwenye kuuziana , labda kama ni ardhi ya kijiji.
Anayetambulika ni hakimu, na mawakili tu, ndio wanaoweza kusimamia mauziano hayo na yakawa na nguvu ya kisheria.zile hati za serikali za mtaa ni makaratasi tu, ambayo kisheria hayana nguvu kabisa.Ukiwa nalo hilo halafu akaja mtu akauziwa hicho kiwanja chako tena na akawa na hati ya mauziano yaliyosimamiwa na wakili, huwezi kushinda hiyo kesi kwa kuonyesha hizo karatasi.
Jamani nyie! Mnazidi tu kunigusa roho! Ad nakosa raha mie.
 
Mkuu matapeli ni noma mimi mwaka jana nimetapeliwa katika ishu moja hivi yan mpka nakuja kujua kua nimetapiliwa aisee nilteseka sana na ile hali ubaya wa matapeli wanakwalua kiasi chote hadi akiba yako wanachukua na hawana huruma mi nasema tapeli ni mmbaya kuliko mwizi
 
Umenipanua ubongo, kwa kuelewa mambo ambayo
kabla ya hii topic sikuyaelewa hasa hila la "mwenza", dah! Isee ubarikiwe sana.
Mkuu nisikufiche wala sijisifii, ila hii post niliyotoa kuna watu wanapata hiyo consultation kwa wakili kwa kuilipia hata 2M au hata zaidi, ila hapo nimeamua kuitoa for free na usishangae mtu akasoma hapo na bado asichukue tahadhari na akapigwa akarudi hapa analia anahitaji tena ushauri 😂😂😂
Barikiwa kama umeongeza kitu kwa andiko hilo.
 
Jamani nyie! Mnazidi tu kunigusa roho! Ad nakosa raha mie.
Pole mkuu, sio kwamba ninazidi kukuumiza ila ni somo tunalolitoa juu ya mambo ya ardhi kwani wengi yanawakuta kutokana na kutojua, na kibaya zaidi hao viongozi wa mitaa/vijiji ndio wanachangia kwa kiasi kikubwa, na linapotokea la kutokea hawana msaada wowote.
 
How is this possible?
Kwani mkuu , mbona watu wamelizwa sana!!mtu una hati original, anazunguka mtu mwenye pesa yake anaenda anatoa rushwa inatolewa hati nyingine, tena inarudishwa nyuma kuliko hata hiyo yako!!ila kwa sasa imepungua sana kama sio kuisha.
 
Back
Top Bottom