Nimetapeliwa zaidi ya Tsh. 45,000,000 kwa kuuziwa kiwanja feki

Nimetapeliwa zaidi ya Tsh. 45,000,000 kwa kuuziwa kiwanja feki

Wanasheria mmejitahidi kutoa elimu nzuri. Watanzania inatakiwa tuelimishwe sana na tusome sana sheria ili tujue haki zetu. Watu wanatoa 10% na hela za udalali alafu ukitokea msala mahakamani hana hata msaada na wewe
Kweli kabisa, hata namimi nimependa jinsi walivyo elezea baadhi ya mambo hapo.

Haya ni mambo ya msingi sana watu kuyafahamu, maana watu wapigwa kila uchao.
 
Iko hivi, sheria haiwatambui, ila wao wakisimamia mauziano hayo ni sawa tu kama umemuita mtu yoyote yule kama shahidi tu, na sio kwa cheo chake!!yeye anachokusaidia ni kukuhakikishia kuwa anayeuza ndio mmiliki wa ardhi hiyo, japo naye anaweza kuwa hana uhakika nalo, kwenye mauziano unaweza kuwa na muuzaji , na mashahidi, na biashara ikafanyika, lakini kisheria kuna watu ambao ndio wamepewa jukumu hilo, hiyo document, ichukue ipeleke kwa wakili akuandalie , document, yenyewe ambayo hata huko mbele ukitokea mgogoro ni rahisi kuwa sehemu salama.Tatizo huwa tunakimbia gharama huko.
Inshu sio kujua background ya ardhi, kwani hao wenyeviti huwa wanakuwa na kumbukumbu tena baada ya kuchukua 10%yao?!labda mgogoro utokee baina ya pande mbili na wote muwe na hayo mavifungashio ya serikali za mitaa, , ndio wataangalia, labda muuzaji sahihi ni nani, nani alikuwa wa kwanza kunununua.
Naomba nikuulize kwa upande mwingine.

Ikiwa mmiliki/mmoja wa wamiliki amedhulumiwa kiwanja anafuta hatua zipi ili kukirudisha?

Mfano kiwanja kinamilikiwa na mke na mume, au familia sasa ikitokea baadhi ya wanafamilia wameuza kiwanja pasi kuwashirikisha wengine, hawa ambao hawajashirikishwa wanafuata hatua zipi za kisheria kukirudisha ikiwa hawajaridhia mauziano? au ndio inakuwa imetoka hiyo?
 
True jini anakupa utajiri nawe unampa jini kafara ya damu.
Damu ni chakula cha majini.
Waganga na wachawi ni matajiri Sana wa pesa lakini masharti yao hayawaruhusu kumiliki mali.Pesa zao wanazitumia kununua vifaa vyao vya Kazi
Upo sahihi, muonekano wa mganga na mazingira yake ni ya hovyo sana watu wakiona vile wanazani mganga Ni maskini hawezi kuvaa vizuri, pale yupo kazini miiko ya kazi inamtaka kuwa vile yale manguo anayovaa na matunguri na zana zingine ndo yanamuwezesha kuingia ulimwengu wa giza kuwasiliana na majini na baada ya kazi anayavua maana Ni mazito balaa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Upo sahihi, muonekano wa mganga na mazingira yake ni ya hovyo sana watu wakiona vile wanazani mganga Ni maskini hawezi kuvaa vizuri, pale yupo kazini miiko ya kazi inamtaka kuwa vile yale manguo anayovaa na matunguri na zana zingine ndo yanamuwezesha kuingia ulimwengu wa giza kuwasiliana na majini na baada ya kazi anayavua maana Ni mazito balaa!

Sent using Jamii Forums mobile app
Pana sasa ni mchungaji zamani alikuwa mganga mwaka 95 alikuwa na bilioni moja cash T shilling,pesa wanakaa nazo ndani huwezi ziona.
Mchawi ni lzm awe na pesa sababu wakati mwingine anaweza akasoma ramani vibaya akapiga radar na kuona njia ipo safi akapita akanaswa kwenye anga za wengine then upigwa faini ya pesa ndipo aachiwe, Ili asiumbuke.
 
Kaka kosa nililofanya ni kutokupitia kwa wenyeviti wa seriklai za mitaa nikamtumia direct mwanasheria lakini wenzangu walionitangulia kununua walipitia huko kwa wenyeviti lakini mambo ndo yamekuwa hivo

So unamaanisha kuwa kupitia kwa Mwanasheria ndo kumesababisha utapeliwe au kuuziwa kiwanja feki..??? Toa maelezo ya namna tukio lako limefanyika and may be I could help you..! Ardhi ni Sehemu ambayo me naifanyia kazi kwa muda mrefu sanaaa
Maelezo yako tu yakishajikanyaga basi ujue haki yako itapotea kirahisi sanaa maana people around take notes of everything katika yale unayoongea na kutafuta weekness point katika matamshi yako.
Kama kweli umetapeliwa 45m kama unavyosema then zipo mamlaka ambazo unaweza pata msaada only if kama ulikua na mashahid wa both sides katika mauziano yako.
Nb: Ardhi ipo na vishoka wengi sana so you better be careful. Na sio ajabu mwenye haki ndo huwa anashidwaga sana kwenye maswala ya Ardhi
 
Mkuu sio kwamba serikali ya mtaa hawakusaidii ila HAWANA MAMLAKA WALA UWEZO WOWOTE WA KUKUSAIDIA KWA LOLOTE KISHERIA. Labda iwe hiyo ni ardhi ya kijiji, ila kama ni ardhi binafsi aisee hao ni sawa na hakuna. Wakili ama hakimu ndio maafisa pekee wanaoruhusiwa kusimamia mikataba ya mauziano ya ardhi.
Serikali za mitaa wana umuhimu wao.kwanza wanakuwa wanajua historia ya eneo.
Pili ni mashahidi wa karibu kabisa ambao wanaweza kusaidia,tofauti na wakili ambaye wakati mwingine anafanya kazi yake akiwa ofisini.

Kutumia wakili kusikufanye ,usiwashirikishe serikali za mitaa kupata taarifa zaidi kuhusu Hilo eneo.
 
Ninaamini kabisa kuwa utapeli upo lakini kuna namna huwa watu tunaweza kuchukua tahadhari na kupunguza visa vya kutapeliwa.
KWA VIWANJA VILIVYOPIMWA:
[emoji91]Baada ya kuwa umeoneshwa kiwanja husika na mmekubaliana bei, hakikisha kuwa unampa wakili kazi ya kusimamia mauzo hayo maana ni lazma atafanya search katika mamlaka husika kujua mmiliki halali ama kama kuna attachment yoyote juu ya kiwanja husika
[emoji91] Hakikisha unajua marital status ya muuza kiwanja, kama atakwambia wameachana hakikisha anakuonesha hati ya talaka ama ya kutengana iliyotolewa na MAHAKAMA na sio vinginevyo.
[emoji91] Endapo ametengana kienyeji na mwenza wake hakikisha huyo mwenza anajaza fomu maalumu (spousal consent) ya kuridhia mauzo ya kiwanja husika yaani hata kama wamenuniana hakikisha mwenza amejaza hiyo form yeye mwenyewe.
[emoji91] Kama kutakua na wasiwasi wowote wa vipimo vya kiwanja husika vile vya kwenye nyaraka na uhalisia hakikisha mnaitumia mamlaka ya ardhi eneo husika kisha kuwakutanisha na majirani wako ili kuweka sawa suala hilo.

KWA VIWANJA/MAENEO AMBAYO HAYAJAPIMWA:
[emoji91]Hakikisha kuwa unawapata watu wote wa pande zote ambazo eneo hilo mnapakana na wakuoneshe na mkubaliane wote mipaka halisi ya eneo unalotaka kununua na hawa ndio watakua mashuhuda wa mjataba wako.
[emoji91]Hakikisha mauziano hayo yanasimamiwa na wakili ambaye atakuongiza katika kufanya search na taratibu sahihi.
[emoji91]Hakikisha mwenza wa anayekuuzia eneo husika anajaza form maalumu ya kuridhia mauzo hayo na kama wameachana hakikisha unapata nyaraka ya mahakama kuthibitisha hili.

KWA MAENEO YA UKOO/FAMILIA/URITHI.
Hapa ndio kuna kivumbi na wanunuzi hupoteza sana pesa hapa.
Kuna wakati ambapo mzazi/mmiliki wa eneo akifariki basi familia haifungui mirathi mahakamani bali hukaa kikao na kuamua kutoaiuza ardhi lakini wakagawanya vyumba ama hisa katika nyumba husika mfano, huweza kugawana vyumba hivyo kila mmoja akawa na mpangaji wake ama wakaipangisha kisha kila kodi ikitolewa basi wanagawana.
Sasa endapo unataka kununua ardhi ya mazingira ya namna hii unatakiwa kuwa makini sanaaa na endapo nyumba ni ya familia hakikisha kuwa wale wanafamilia woooote yaani namaanisha WOTE sio wengi hapana, nasema WANAFAMILIA WOTE wahaohusika na ardhi ama nyumba husika ndipo muweze kuendelea na mauzo. Hii ni kwa sababu endapo ikatokea mmoja ama sehemu ya wanahisa wa hiyo ardhi ya familia hakuridhia basi utakua umepigwaaa(rejea kilichomkuta S. H. Amon hapo Kariakoo)
Iwapo nyumba inamilikiwa na Ukoo yaani vizazi hata viwili ama vitatu yaani nyumba alikua anamiliki babu yangu ambaye alikua na watoto nane na wote hao walikua na familia, wakafariki 4 na watoto wa babu wakazaa tukatokea sisi na baadhi yetu tumeshafariki lakini tumeacha watoto wetu ambao wana haki kupitia baba na babu zao aisee mimi NINAKUSHAURU USINUNUE ARDHI HIYO hakikisha kabla ya kununua au kulipia hata sh mia unawasiliana na wakili wako.


Kiukweli wakuu ukitapeliwa kwenye kiwanja kilichopimwa ni lazma wewe mnunuzi kuna mahali ulizembea kwenye utaratibu mzima wa manunuzi maana kwa upande wa hivi viwanja vilivyopimwa utaratibu upo wazi sana.
Nilichogundua ni kuwa wengi wana mazoea na kukalili taratibu za kizamani zisizotambuliwa kisheria yaani mtu anaona kutoa 2M kwa wakili asimamie mchakato mzima wa mauziano ya 50M anamuamini dalali ambaye atalipwa 10% na mtedaji/mwenyekiti halafu anatoa hela[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

HAKIKISHENI MNAFUATA MIONGOZO YA WANASHERIA KUPUNGUZA KUTAPELIWA

Umenifungua sana mkuu asante
 
Serikali za mitaa wana umuhimu wao.kwanza wanakuwa wanajua historia ya eneo.
Pili ni mashahidi wa karibu kabisa ambao wanaweza kusaidia,tofauti na wakili ambaye wakati mwingine anafanya kazi yake akiwa ofisini.

Kutumia wakili kusikufanye ,usiwashirikishe serikali za mitaa kupata taarifa zaidi kuhusu Hilo eneo.
  • Wana umuhimu wao kwa ardhi ambazo hazijapimwa,
  • Na hao serikali ya Mtaa ndio wameleta mabalaa ya kuuza Ardhi Mara mbili
  • Unasema Wakili amekaa ofisini hivi unajua maana ya neno 'official search'?
 
Haya mambo yasikie tu.

Nina siku ya nne leo tangu nigundue kwamba nimepigwa, hata kula vizuri siwezi, nawaonea wivu wenzangu walionunua maeneo madogo kwa bei za 15m kushuka chini. Naona hasara yao ni ndogo kuliko yangu.
Ilikuaje Mkuu?
 
kuna siku nilisema humu ukitaka kununua kiwanja au shamba jitahidi kuuliza majirani zako watarajiwa kuhusu hicho kitu.
Pili usiwe mvivu kwenda wizara ya ardhi kujiridhisha kuhusu hicho kiwanja Cha Nani na anamiliki Nani.
Nani usifanye malipo bila kuwa na WAKILI
Mfano viwanja vilivyopo uko vikindj ndani ndani je wizara ya ardhi inavijua ama inakuwaje apa?
 
Kama hauja ikopa piga moyo konde ili maisha mengine yaendelee
Unafikiri ni rahisi kihivyo Mkuu
Mbaya zaidi ukute ni mwenzangu na mie hela zenyew za mawazo unaweza kufa kwa pressure
Afadhali kama ni mtu mwenye hela zake nyingi nyingi
 
Mkuu mimi hapa ninaamini na nitazidi kuamini kuwa utapeli katika viwanja kwa zaidi ya 85% unachangiwa na sisi wenyewe wanunuzi. Mkuu mimi ni mwanasheria, ila nikwambie ukweli kabisa kuna wateja hamshaurikiiii hamtaki kusikiliza ya wataalamu na mwisho wa siku mnapigwa.
Mfano, mteja anatafuta kiwanja anaona dalali amepost. Baada ya hapo anaenda kuona kiwanja, dalali anatia maneno ya kuonesha kuwa wengi wanahitaji kiwanja hicho, anamleta mtu ambaye anadai kuwa ndiye mmiliki(kumbe ni msimamizi tu wa familia na sio mmiliki). Mnaenda kwa mwenyekiti wa mtaa anakula 10% dalali anakula % yake halafu mnaandikishana pale kisha mnampelekea wakili makaratasi yenu kuwa 'AWAGONGEE MUHURI' mna laki 5[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] wakili anakuuliza kama umefanya utafiti kuwa hakuna shida yoyote? Unajibu ndioooo na mwenyekiti ametuthibitishia, wakili anakwambia kama umejiridhisha basi hakuna shida(huku akitabasamu) maana hata akikukatalia utaenda kwa mwingine na unaweza kukutana na karani wake akagonga huo muhuri kwa laki 2.
Kinanuka baadae ndio unatambua kuwa dalali na mwenyekiti hawatambuliki kwa namna yoyote katika mikataba ya ardhi binafsi, unamfuata wakili anakukumbusha maswali ya siku hiyo na mwisho wa siku hata kesi yako hawezi kuisimamia mahakamani tena unabaki kumuachia Mungu [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Ukisema hivi unatugusa wengi halafu unatupa na pressure juu.
Mungu atuongoze kwakweli.
 
Unafikiri ni rahisi kihivyo Mkuu
Mbaya zaidi ukute ni mwenzangu na mie hela zenyew za mawazo unaweza kufa kwa pressure
Afadhali kama ni mtu mwenye hela zake nyingi nyingi
mali zinatafutwa tuu, asipo piga moyo konde na ku move on, atahatarisha afya yake mwisho wa siku atapata magonjwa yasiyotibika….
 
Back
Top Bottom